Twendeni tu tutafika! (Siasa zetu na Hatma ya Tanzania)

Mzee alituita vijana wake wote pale nyumbani. Akasema anataka tumfuate tuanze safari. Nakumbuka mdogo wangu alimuuliza "mzee mbona hatujajiandaa na pia unataka twende wapi?"

Mzee alimkazia macho na kumwambia "tunaanza safari muda huu ni safari ya miaka 5. Tunakoenda tutakujua huko huko mbele'

Mdogo wangu aligeuka kunitizama nadhani akitaka nami nichangie kitu. Nlijizoa zoa pale chini na kusimama kama nataka kuongea. Nikaelekea jikoni kunywa maji.

Tukaanza kuondoka. Hatukwenda kuaga majumbani kwetu,hatukubeba nguo,hatukubeba chakula,hatukufanya lolote . Vile tulivyokuwa tumeenda kwenye kikao na mzee ndivyo tulivyoanza safari.

Safari ilikuwa ngumu.mimi kilichokuwa kikinisimamisha mara nyingi ilikuwa ni kuchepuka pembeni kujisaidia haja ndogo. Nlikuwa nmekunywa maji mengi sana. Kuna sehemu katika safari tulikuwa tunakuta njia na kuna sehemu tunapita tu vichakani na maporini.

Mwenzetu mmoja akagongwa na nyoka kichwani. Mzee akatwambia kama amegongwa na nyoka kichwani tumfunge kamba shingoni tukaze sana ili damu yenye sumu isipite kuja moyoni. Tukafanya hivyo. Tulikaza sana mpaka akaanza kukoroma huku ametoa macho.

Tukaona kama sauti inatoka maana yake hatujakaza sana.tukakaza zaidi ili damu yenye sumu isije shuka kuja moyoni. Akaacha kukoroma akawa ametulia.tukaridhika tukamweka chini ya mti apumzike.

tukamuuliza mzee sasa inakuaje kwa huyu ndugu yetu. Akasema "aah nyie twendeni tu tutafika" tukamwacha ndugu yetu aendelee kupumzika halafu atufuate akipata nafuu.hatukumwona tena.

Tuliendelea na safari mpaka tulifikia hatua kumuuliza mzee tunaenda wapi mbona hatufiki. Akajibu "aaah nyie twendeni tu tutafika" hatukujua na hakujua tunaenda wapi. Tungefikaje?

Safari ilizidi kuwa ngumu walitokea watu kadhaa katikati yetu walionekana kuielewa sana safari ya kuelejea kusikojulikana. Wakawa hata wanaanzisha nyimbo za kututia moyo wakiimba na kuruka ruka njia nzima.

Wengine walianza kuugua,kudhoofika na hata kupoteza maisha. Njia ilikuwa ni mbaya,na kuna sehemu hakukuwa na njia.mzee tu ndo alikuwa anatoa maamuzi wapi tupite wapi tupumzike.

Wenzetu wengine wakaanza kubaki nyuma kwa kuishiwa nguvu,udhaifu na njaa. Mzee akasema hao tuwaache.si lazima wote tufike.

Swali likawa anataka tufike wapi?tunaenda wapi? Akawa anajibu "aah twendeni tu tutafika" mimi kaka mkubwa nlikuwa nimenyamaza tu na wakati mwingine nikiwafokea wadogo zangu kuwa kama hawatembei tutawaacha.sikutaka ionekane nami sijui tunakoenda.

Walikuwa wananiuliza "kaka sasa tutajuaje tumefika ikiwa hatujui tunakoenda?" Nami nliwajibu. "Aah twendeni tu tutafika" baba alianza kupatwa na uchovu safarini tulimwona mara kadhaa akichechemea. Lakini tuliamini nayo ni madoidoi au miondoko tu katika safari.

Nlihamasisha wadogo zangu wakazane kutembea. Tulitembea na baadaye nikaanza kuwahamasisha wapunguze mwendo ili kuendana na kasi ya mzee aliyekuwa amedhoofu.

Hatimaye...Mzee alishindwa kuendelea na safari. Akiwa amekaa pembeni ya jiwe chini ya mti akaniita nikamsikilize.nilienda msikiliza.alinambia mwanangu" kule tulipotoka tumeacha vitu vingi na familia zetu....lakini pia tumeacha giza.nataka tutafute mwanga.ila sijui tunapata wapi mwanga"

Mzee akafariki. Nikatakiwa kuchukua uongozi wa msafara. Nligundua watu wengu hawakupenda mwendelezo wa safari ya mzee. Haukuwa na maana.hapo nlianza kuwarudisha moyo uliopotea. Nikaanza kuwatia nguvu.

Safari ikaanza...ila nikiwa sasa nachagua njia za kupita.na kuwapa muda wa kupumzika,kula na kulala.walipokuwa wakiniuliza tunaenda wapi.nliwajibu

"sijui, twendeni tu tutafika" wakafurahi sana. Safari ikawa inaendelea tukiongea njia nzima na kucheka. Tukisimama njiani na kugeuka nyuma kuangalia tulipotoka kwa masaa 5 na kisha tunaendelea na safari kwa saa moja. Tukawa tunapumzika tena kwa masaa 10 na kuanza safari tena kwa masaa 2.

Sikujua tunaenda wapi ila niliamini tutafika tu. Nimemkumbuka mzee yeye alijibu "AHH TWENDENI TU, TUTAFIKA."
GuDume the philosopher
 
Hahahaa sawa
 
Fumbo mfumbie mjinga....

Heri yako wewe umeielewa fasihi na kufumbua fumbo hili....

Kwa kifupi, huhitaji mji maana umefumbua fumbo kwa usahihi kabisa...

Hilo zee la "....twendeni tu, tutafika..", kweli ni li CCM hili lilokwisha zeeka na kujifia porini na kuzikwa huko huko...!
Wanaccm kinachowapa kiburi ni kodi zetu
 
Mbowe sio gaidi
Screenshot_20210807-014708_1.jpg
 
Kwakweli nilitaka nipite hapa bila kusema kitu lakn kwa maslahi ya taifa langu wacha niseme neno...

Kwa hili la mbowe kiukweli kinatutia doa sisi kama taifa ingawa kama ni madoa tunayo mengi😆sasa napata shida kidogo kuamini kama jambo hili linabaraka za mama🤭ingawa kama nataka kuamini hivi kama linabaraka zake

Kama ni kweli basi mama amefanya makosa na na ndio maana imani kwa mama imeanza kuondolewa ikiwa bado ni mapema mno tangu tulipoanza kuwa na imani nae

Sasa ushauri wangu ni kwamba badala ya mama pamoja na IGP kuendelea kumsweka ndani ni bora wakamuachia then wakawaita hawa wapinzani ili waweze kufanya mazungumzo ya pamoja kujua wanalimalizaje hili la katiba mpya lkn kitendo cha yeye kuendelea kuwapotezea wapinzani kinasababisha haya kuendelea.
 
Nataka nikupe Taarifa kwamba Huyo aliyegongwa na Nyoka mkamfunga Kamba shingoni Kwa amri ya Mzee wenu katili, aliokolewa na wapita njia na kuhudumiwa kienyeji Kwa misaada ya wasio ndugu zake na mpaka Leo kuwa kwake hai ni miongoni mwa miujiza. Yule Kaka yako aliyeshauri mkaze Kamba shingoni mwa mgonjwa ili aache kukoroma kabisa alishafukuzwa na mama yenu na mpaka Leo haijulikani amesimama au amekaa. Mara aonekane Kapernaum akimtafuta mke wa Yesu mara aonekane Canterbury akifagia kanisani, kiujumla kwake siku hizi Moja haikai mbili haikai yaani yupo yupo tu.
 
Safari bado ni yenye mashaka na uelekeo haujulikani mpaka leo. 😔
 
Mwenzetu mmoja akagongwa na nyoka kichwani. Mzee akatwambia kama amegongwa na nyoka kichwani tumfunge kamba shingoni tukaze sana ili damu yenye sumu isipite kuja moyoni. Tukafanya hivyo. Tulikaza sana mpaka akaanza kukoroma huku ametoa macho.
Hatari sana
 
Back
Top Bottom