Twendeni tu tutafika! (Siasa zetu na Hatma ya Tanzania)

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,247
Mzee alituita vijana wake wote pale nyumbani. Akasema anataka tumfuate tuanze safari. Nakumbuka mdogo wangu alimuuliza "mzee mbona hatujajiandaa na pia unataka twende wapi?"

Mzee alimkazia macho na kumwambia "tunaanza safari muda huu ni safari ya miaka 5. Tunakoenda tutakujua huko huko mbele'

Mdogo wangu aligeuka kunitizama nadhani akitaka nami nichangie kitu. Nlijizoa zoa pale chini na kusimama kama nataka kuongea. Nikaelekea jikoni kunywa maji.

Tukaanza kuondoka. Hatukwenda kuaga majumbani kwetu,hatukubeba nguo,hatukubeba chakula,hatukufanya lolote . Vile tulivyokuwa tumeenda kwenye kikao na mzee ndivyo tulivyoanza safari.

Safari ilikuwa ngumu.mimi kilichokuwa kikinisimamisha mara nyingi ilikuwa ni kuchepuka pembeni kujisaidia haja ndogo. Nlikuwa nmekunywa maji mengi sana. Kuna sehemu katika safari tulikuwa tunakuta njia na kuna sehemu tunapita tu vichakani na maporini.

Mwenzetu mmoja akagongwa na nyoka kichwani. Mzee akatwambia kama amegongwa na nyoka kichwani tumfunge kamba shingoni tukaze sana ili damu yenye sumu isipite kuja moyoni. Tukafanya hivyo. Tulikaza sana mpaka akaanza kukoroma huku ametoa macho.

Tukaona kama sauti inatoka maana yake hatujakaza sana.tukakaza zaidi ili damu yenye sumu isije shuka kuja moyoni. Akaacha kukoroma akawa ametulia.tukaridhika tukamweka chini ya mti apumzike.

tukamuuliza mzee sasa inakuaje kwa huyu ndugu yetu. Akasema "aah nyie twendeni tu tutafika" tukamwacha ndugu yetu aendelee kupumzika halafu atufuate akipata nafuu.hatukumwona tena.

Tuliendelea na safari mpaka tulifikia hatua kumuuliza mzee tunaenda wapi mbona hatufiki. Akajibu "aaah nyie twendeni tu tutafika" hatukujua na hakujua tunaenda wapi. Tungefikaje?

Safari ilizidi kuwa ngumu walitokea watu kadhaa katikati yetu walionekana kuielewa sana safari ya kuelejea kusikojulikana. Wakawa hata wanaanzisha nyimbo za kututia moyo wakiimba na kuruka ruka njia nzima.

Wengine walianza kuugua,kudhoofika na hata kupoteza maisha. Njia ilikuwa ni mbaya,na kuna sehemu hakukuwa na njia.mzee tu ndo alikuwa anatoa maamuzi wapi tupite wapi tupumzike.

Wenzetu wengine wakaanza kubaki nyuma kwa kuishiwa nguvu,udhaifu na njaa. Mzee akasema hao tuwaache.si lazima wote tufike.

Swali likawa anataka tufike wapi?tunaenda wapi? Akawa anajibu "aah twendeni tu tutafika" mimi kaka mkubwa nlikuwa nimenyamaza tu na wakati mwingine nikiwafokea wadogo zangu kuwa kama hawatembei tutawaacha.sikutaka ionekane nami sijui tunakoenda.

Walikuwa wananiuliza "kaka sasa tutajuaje tumefika ikiwa hatujui tunakoenda?" Nami nliwajibu. "Aah twendeni tu tutafika" baba alianza kupatwa na uchovu safarini tulimwona mara kadhaa akichechemea. Lakini tuliamini nayo ni madoidoi au miondoko tu katika safari.

Nlihamasisha wadogo zangu wakazane kutembea. Tulitembea na baadaye nikaanza kuwahamasisha wapunguze mwendo ili kuendana na kasi ya mzee aliyekuwa amedhoofu.

Hatimaye...Mzee alishindwa kuendelea na safari. Akiwa amekaa pembeni ya jiwe chini ya mti akaniita nikamsikilize.nilienda msikiliza.alinambia mwanangu" kule tulipotoka tumeacha vitu vingi na familia zetu....lakini pia tumeacha giza.nataka tutafute mwanga.ila sijui tunapata wapi mwanga"

Mzee akafariki. Nikatakiwa kuchukua uongozi wa msafara. Nligundua watu wengu hawakupenda mwendelezo wa safari ya mzee. Haukuwa na maana.hapo nlianza kuwarudisha moyo uliopotea. Nikaanza kuwatia nguvu.

Safari ikaanza...ila nikiwa sasa nachagua njia za kupita.na kuwapa muda wa kupumzika,kula na kulala.walipokuwa wakiniuliza tunaenda wapi.nliwajibu

"sijui, twendeni tu tutafika" wakafurahi sana. Safari ikawa inaendelea tukiongea njia nzima na kucheka. Tukisimama njiani na kugeuka nyuma kuangalia tulipotoka kwa masaa 5 na kisha tunaendelea na safari kwa saa moja. Tukawa tunapumzika tena kwa masaa 10 na kuanza safari tena kwa masaa 2.

Sikujua tunaenda wapi ila niliamini tutafika tu. Nimemkumbuka mzee yeye alijibu "AHH TWENDENI TU, TUTAFIKA."
 
... zee lako pumbavu sana. Safari isiyo na vision wala mission ni safari ya wapumbavu; ni msafara wa wendawazimu. Mwisho wa siku aliwatumbukiza shimboni na mliobaki mkalizika porini.

Vijana muwe na ujasiri wa kuhoji na kuipinga mizee mipumbavu na mission zao za kichawi! Mchawi huyu alitaka kuwatoa kafara afe na afe tena! Hii stori imeniumiza sana.
 
kama msafara wa nyumbu pale ufipa, yaani yataka akili ndogo sana kuendelea.
 
Ndugu,
Yaonekana wewe ndio umepungukiwa uelewa.
'Wao' wanaosafiri wanafahamu wanakokwenda ni Masai mara. Baada ya muda uliyo ndani ya ratiba yao, huanza safari yao ya kwenda Serengeti/Soronera. Itakuwa ni busara kwako kama utajipa muda lau mdogo na kujiruhusu kujifunza kutoka kwao.
'Nyie' ni siku nyingi mnasumbuliwa na ugonjwa wa kukazania kuonekana TUU kuwa mnasafiri wakati HAMJUI kabisa HATA mnakohitaji kwenda ili kuleta maendeleo ya WATU.
Nyimbo zilezile, vilevile zimesharudi tena. Hata wale walokuwa wameanza kupata japo mwanga wa matumaini, wameanza kuyapoteza vilevile, kwani LILE giza linarudi kwa kasi vilevile.
 
I love this story, ninaamini kabla hujandika hii story ulikuwa na tafari pana sana juu ya taifa letu. Tutafika tu.
 
Ndugu,
Yaonekana wewe ndio umepungukiwa uelewa.
'Wao' wanaosafiri wanafahamu wanakokwenda ni Masai mara. Baada ya muda uliyo ndani ya ratiba yao, huanza safari yao ya kwenda Serengeti/Soronera. Itakuwa ni busara kwako kama utajipa muda lau mdogo na kujiruhusu kujifunza kutoka kwao.
'Nyie' ni siku nyingi mnasumbuliwa na ugonjwa wa kukazania kuonekana TUU kuwa mnasafiri wakati HAMJUI kabisa HATA mnakohitaji kwenda ili kuleta maendeleo ya WATU.
Nyimbo zilezile, vilevile zimesharudi tena. Hata wale walokuwa wameanza kupata japo mwanga wa matumaini, wameanza kuyapoteza vilevile, kwani LILE giza linarudi kwa kasi vilevile.
kwahiyo kila nyumbu anaenda masai mara😁😁.

ukiona umeitwa nyumbu ni kwa sababu hutumii akili wapi pa kupita safarini.anakopita wa kwanza wote wanapita hapo,hata asombwe na maji waliobaki nao wanakwenda kusombwa, sababh tu ni njia wanapitaga.
 
SAwa
Mzee alituita vijana wake wote pale nyumbani. Akasema anataka tumfuate tuanze safari. Nakumbuka mdogo wangu alimuuliza "mzee mbona hatujajiandaa na pia unataka twende wapi?"

Mzee alimkazia macho na kumwambia "tunaanza safari muda huu ni safari ya miaka 5. Tunakoenda tutakujua huko huko mbele'

Mdogo wangu aligeuka kunitizama nadhani akitaka nami nichangie kitu. Nlijizoa zoa pale chini na kusimama kama nataka kuongea. Nikaelekea jikoni kunywa maji.

Tukaanza kuondoka. Hatukwenda kuaga majumbani kwetu,hatukubeba nguo,hatukubeba chakula,hatukufanya lolote . Vile tulivyokuwa tumeenda kwenye kikao na mzee ndivyo tulivyoanza safari.

Safari ilikuwa ngumu.mimi kilichokuwa kikinisimamisha mara nyingi ilikuwa ni kuchepuka pembeni kujisaidia haja ndogo. Nlikuwa nmekunywa maji mengi sana. Kuna sehemu katika safari tulikuwa tunakuta njia na kuna sehemu tunapita tu vichakani na maporini.

Mwenzetu mmoja akagongwa na nyoka kichwani. Mzee akatwambia kama amegongwa na nyoka kichwani tumfunge kamba shingoni tukaze sana ili damu yenye sumu isipite kuja moyoni. Tukafanya hivyo. Tulikaza sana mpaka akaanza kukoroma huku ametoa macho.

Tukaona kama sauti inatoka maana yake hatujakaza sana.tukakaza zaidi ili damu yenye sumu isije shuka kuja moyoni. Akaacha kukoroma akawa ametulia.tukaridhika tukamweka chini ya mti apumzike.

tukamuuliza mzee sasa inakuaje kwa huyu ndugu yetu. Akasema "aah nyie twendeni tu tutafika" tukamwacha ndugu yetu aendelee kupumzika halafu atufuate akipata nafuu.hatukumwona tena.

Tuliendelea na safari mpaka tulifikia hatua kumuuliza mzee tunaenda wapi mbona hatufiki. Akajibu "aaah nyie twendeni tu tutafika" hatukujua na hakujua tunaenda wapi. Tungefikaje?

Safari ilizidi kuwa ngumu walitokea watu kadhaa katikati yetu walionekana kuielewa sana safari ya kuelejea kusikojulikana. Wakawa hata wanaanzisha nyimbo za kututia moyo wakiimba na kuruka ruka njia nzima.

Wengine walianza kuugua,kudhoofika na hata kupoteza maisha. Njia ilikuwa ni mbaya,na kuna sehemu hakukuwa na njia.mzee tu ndo alikuwa anatoa maamuzi wapi tupite wapi tupumzike.

Wenzetu wengine wakaanza kubaki nyuma kwa kuishiwa nguvu,udhaifu na njaa. Mzee akasema hao tuwaache.si lazima wote tufike.

Swali likawa anataka tufike wapi?tunaenda wapi? Akawa anajibu "aah twendeni tu tutafika" mimi kaka mkubwa nlikuwa nimenyamaza tu na wakati mwingine nikiwafokea wadogo zangu kuwa kama hawatembei tutawaacha.sikutaka ionekane nami sijui tunakoenda.

Walikuwa wananiuliza "kaka sasa tutajuaje tumefika ikiwa hatujui tunakoenda?" Nami nliwajibu. "Aah twendeni tu tutafika" baba alianza kupatwa na uchovu safarini tulimwona mara kadhaa akichechemea. Lakini tuliamini nayo ni madoidoi au miondoko tu katika safari.

Nlihamasisha wadogo zangu wakazane kutembea. Tulitembea na baadaye nikaanza kuwahamasisha wapunguze mwendo ili kuendana na kasi ya mzee aliyekuwa amedhoofu.

Hatimaye...Mzee alishindwa kuendelea na safari. Akiwa amekaa pembeni ya jiwe chini ya mti akaniita nikamsikilize.nilienda msikiliza.alinambia mwanangu" kule tulipotoka tumeacha vitu vingi na familia zetu....lakini pia tumeacha giza.nataka tutafute mwanga.ila sijui tunapata wapi mwanga"

Mzee akafariki. Nikatakiwa kuchukua uongozi wa msafara. Nligundua watu wengu hawakupenda mwendelezo wa safari ya mzee. Haukuwa na maana.hapo nlianza kuwarudisha moyo uliopotea. Nikaanza kuwatia nguvu.

Safari ikaanza...ila nikiwa sasa nachagua njia za kupita.na kuwapa muda wa kupumzika,kula na kulala.walipokuwa wakiniuliza tunaenda wapi.nliwajibu

"sijui, twendeni tu tutafika" wakafurahi sana. Safari ikawa inaendelea tukiongea njia nzima na kucheka. Tukisimama njiani na kugeuka nyuma kuangalia tulipotoka kwa masaa 5 na kisha tunaendelea na safari kwa saa moja. Tukawa tunapumzika tena kwa masaa 10 na kuanza safari tena kwa masaa 2.

Sikujua tunaenda wapi ila niliamini tutafika tu. Nimemkumbuka mzee yeye alijibu "AHH TWENDENI TU, TUTAFIKA."
Sawa. Tumetembea kama taifa huru miaka 60 bila kujua wala kufika tuendapo. Tunahitaji katiba mpya ili tujue na kufika tuendapo. Tumuache Mzee CCM apumzike kwa amani.
 
Hilo zee lilofariki njiani halina tofauti na kichaa mwendazske
 
kwahiyo kila nyumbu anaenda masai mara😁😁.

ukiona umeitwa nyumbu ni kwa sababu hutumii akili wapi pa kupita safarini.anakopita wa kwanza wote wanapita hapo,hata asombwe na maji waliobaki nao wanakwenda kusombwa, sababh tu ni njia wanapitaga.
Hata mbuzi au ng'ombe au kuku wote ni wanyama na wote hawana utashi wala akili...

MaCCM nyie si ni makuku kabisa maana mnafugwa ili mchinjwe na mliwe nyama na mfugaji na siku ya kuchinjwa wala hata mnakuwa hamna taarifa. Mtabebwa kama jiwe na kulambwa kisu...
 
SAwa
Sawa. Tumetembea kama taifa huru miaka 60 bila kujua wala kufika tuendapo. Tunahitaji katiba mpya ili tujue na kufika tuendapo. Tumuache Mzee CCM apumzike kwa amani.
Fumbo mfumbie mjinga....

Heri yako wewe umeielewa fasihi na kufumbua fumbo hili....

Kwa kifupi, huhitaji mji maana umefumbua fumbo kwa usahihi kabisa...

Hilo zee la "....twendeni tu, tutafika..", kweli ni li CCM hili lilokwisha zeeka na kujifia porini na kuzikwa huko huko...!
 
Back
Top Bottom