Twende na Taifa Stars Ivory Coast AFCON 2023

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
9,263
9,883
Natamani ifanyike kampeni kubwa ya kuhamasisha timu yetu ya taifa kwenye mashindano ya AFCON 2023 yatakayofanyika Ivory Coast 2023.

TFF na Serekali huu ndiyo wakati wa kuunganisha nguvu kuwashirikisha wadau na wanachi kwa ujumla kwenye kampeni hiyo.

Updates

TIMU ya Taifa Tanzania 'Taifa Stars' imeingia katika hatua ya makundi kwenye fainali za mataifa ya Afrika inayotarajiwa kufanyika 2023 nchini Ivory Coast.

Tanzania na timu zingine 41 (Jumla 42) zitaingia moja kwa moja katika hatua ya makundi huku wakisubiri timu sita kutoka katika raundi ya awali na kuwa timu 48 ambazo zitakuwa katika makundi 12 (A-L).

Stars imepata uhakika wa kuanzia hatua ya makundi baada ya jana kufanyika droo ya raundi ya awali Douala, Cameroon ikisimamiwa na wachezaji wa zamani Emmanuel Amunike (Nigeria) na Rigobert Song (Cameroon) wakisaidiana na mkurugenzi wa mashindano CAF, Samson Adamo.

Droo hiyo ilihusisha timu 12 ambazo zitacheza raundi hiyo ya awali na baada ya hapo zitapatikana wababe sita ambao wataenda kukutana na timu 42 katika hatua ya makundi.

Twende Na Stars Afcon 2023
 
Tumeshindwankuwachangia biashara waingie makundi condederation cup ndio itakuwa kifuzu afcon....
 
Wabongo kila jambo letu la kitaifa tunalikatia tamaa.
Tatizo lipo pahala hasa kule juu kwa watawala wa hii nchi.
 
Natamani ifanyike kampeni kubwa ya kuhamasisha timu yetu ya taifa kwenye mashindano ya AFCON 2023 yatakayofanyika Ivory Coast 2023.

TFF na Serekali huu ndiyo wakati wa kuunganisha nguvu kuwashirikisha wadau na wanachi kwa ujumla kwenye kampeni hiyo.

Updates

TIMU ya Taifa Tanzania 'Taifa Stars' imeingia katika hatua ya makundi kwenye fainali za mataifa ya Afrika inayotarajiwa kufanyika 2023 nchini Ivory Coast.

Tanzania na timu zingine 41 (Jumla 42) zitaingia moja kwa moja katika hatua ya makundi huku wakisubiri timu sita kutoka katika raundi ya awali na kuwa timu 48 ambazo zitakuwa katika makundi 12 (A-L).

Stars imepata uhakika wa kuanzia hatua ya makundi baada ya jana kufanyika droo ya raundi ya awali Douala, Cameroon ikisimamiwa na wachezaji wa zamani Emmanuel Amunike (Nigeria) na Rigobert Song (Cameroon) wakisaidiana na mkurugenzi wa mashindano CAF, Samson Adamo.

Droo hiyo ilihusisha timu 12 ambazo zitacheza raundi hiyo ya awali na baada ya hapo zitapatikana wababe sita ambao wataenda kukutana na timu 42 katika hatua ya makundi.

Twende Na Stars Afcon 2023
Naona unajaribu kuona mbwa kiuno
 
Back
Top Bottom