Bernard Membe
R I P
- Oct 19, 2020
- 1
- 52
Watanzania na wapiga kura wenzangu salaam,
Mimi Bernard Kamillius Membe ni mgombea wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha ACT Wazalendo.
Tarehe 28/10/2020 ni siku ya kupiga kura ya kurejesha Uhuru uliopotea tangu awamu ya tano iingie madarakani miaka mitano iliyopita.
Ni siku ya kuchagua mtu anayefaa kuliongoza Taifa, Mtu mwenye uzoefu, Mzalendo na mwenye uchungu na maendeleo ya Nchi yetu.
Puuzeni watu wanaosema nmejiondoa kwenye kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano. Twendeni mkanipigie kura mimi Membe Bernard Kamillius ambaye nmekidhi vigezo vyote. Nipigieni kura tuwe na Serikali ya Kazi na Bata.
Mimi nitafunga Kampeni yangu tarehe 27/10/2020 kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Mkoani Lindi.
Nawakaribisha wote.
Asanteni kwa kunisikiliza
Uchaguzi 2020 - Yaliyojiri kutoka Diamond Jubilee Mkutano Mkuu wa ACT–Wazalendo: Membe apata kura za Ndiyo 410 za Urais Tanzania, Maalim Seif Ndiyo 419 za Zanzibar
Chama cha ACT–Wazalendo leo tarehe 05 Agust 2020 kinafanya Mkutano wake Mkuu Diamond Jubilee–VIP Hall. #MkutanoMkuuACT2020 #KaziNaBata #TheFutureIsPurple ===== UPDATES ====== #UCHAGUZI2020: MEMBE, MAALIM KUPEPERUSHA BENDERA ZA ACT WAZALENDO URAIS TANZANIA NA ZANZIBAR - Chama hicho...
www.jamiiforums.com
Uchaguzi 2020 - Bernard Membe achukua fomu ya kugombea Urais wa Tanzania kupitia ACT Wazalendo
Leo tarehe 17 Julai 2020, Waziri wa Mambo ya Nje Mstaafu na Mwanachama wa ACT Wazalendo Ndugu Bernard Membe atazungumza na waandishi wa habari. Ukumbi: Ofisi ya ACT Wazalendo Magomeni, Dar es salaam. Muda: Saa 8.00 Mchana. Waandishi wote mnakaribishwa. Janeth Rithe, Naibu Katibu wa Habari...
www.jamiiforums.com