WilsonKaisary
JF-Expert Member
- Apr 4, 2017
- 392
- 947
Tweet ya naibu waziri wa afya "No country has been able to sustain a rapid transition out of poverty without raising productivity in its agricultural sector"
KILIMO KWANZA ilikuwa ni sera nzuri iliyokosa utekelezaji tu awamu yake yani awamu ya tano ikaja na sera ya UCHUMI WA VIWANDA leo ana-post tweet hiyo.
Kiuhalisia ni kweli sera ya UCHUMI WA VIWANDA hatujaifanyia maandalizi ya kutosha na ni sera itakayodumu kwenye utawala wa Magufuli kama ilivyokuwa kwenye sera ya KILIMO KWANZA, serikali yetu inakosa sera mama ya kukuza uchumi kila raisi na serikali yake anakuja na sera zake jambo ambalo si sawa sana.
Sera ya UCHUMI WA VIWANDA imekosa maandalizi na kwa taifa hili tupo mbele au ilibidi twende nayo kwa awamu maana mpaka hapa hatuna wakufunzi wa kuongoza viwanda hivyo hata kama vitajengwa, watanzania bado hawana elimu juu ya ununuzi wa bidhaa zao za ndani na bado sera ndogo ndogo za kulinda bidhaa zitakazo-zalishwa hapa nchini. mfano uliohai kuna bidhaa zinazalishwa hapa nchini lakini bado kuna bidhaa za kutoka nje ya nchi zinaletwa kwa wingi na bado watanzania hawana imani na bidhaa zetu za ndani. kwa hali hii hata tukijenga viwanda vya kuzalisha bidhaa soko letu litakuwa la nje ya nchi?
Wizara ya elimu ilitoa tamko kuwa wanafunzi wote nchini wasome masomo ya sayansi kwa ulazima, bila kujali hawa wanafunzi watafundishwa sayansi ya viwanda au sayansi hii ya kawaida. Pia wizara haikutilia maanani kama nchini kuna uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi.
Kwanini TECHNICAL SCHOOLS zisijengwe upya ndio ziwe za kutoa wakufunzi wa viwanda. kwa kweli hatukijipanga kwa mambo mengine umeme wenyewe wa kusuasua huu umeme tulionao sasa na tukiongezea na huu wa mradi ulizinduliwa wiki za karibuni, ni kweli utaweza tosheleza mahitaji ya viwanda vikubwa?
Hii sera ina mapungufu makubwa, na haipaswi kuwa sera ya awamu mmoja inapaswa kuwa endelevu hata kwa awamu zijazo kama itafanywa kama sera ya KILIMO KWANZA basi hii viwanda vitakuja kufa kama vya hapo awali.