UZUSHI TWAWEZA yaahirisha uzinduzi wa matokeo ya utafiti mpya wa Sauti za Wananchi, leo Agosti 25, 2022

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Twaweza.png

Kufuatia kutangazwa kwa tukio la uzinduzi wa takwimu za shirika lisilo la kiserikali la TWAWEZA East Africa linalotarajiwa kufanyika leo tarehe 25 Agosti, 2022, kumekuwepo madai/uvumi kuwa tukio hilo limeahirishwa.

Taarifa hizo ambazo zimekuwa zikisambazwa katika makundi sogozi ya WhatsApp pamoja na mtandao wa Twitter, zimedai kuwa tukio hilo ambalo linatatajia kuwashirikisha wananchi matokeo ya utafiti uliyofanywa na TWAWEZA unaolenga kuutaarifu umma matokeo hayo yenye uwakilishi wa kitaifa kutoka Sauti za Wananchi - ambalo ni jukwaa la kupigia kura kwa njia ya simu ya mkononi - umeahirishwa, ingawa bila kutoa taarifa kuwa umesukumwa hadi siku/tarehe gani.

Hapa chini ni picha ambayo imetumika kusambaza uvumi huo.
 
Tunachokijua
Shirika hilo lisilo la kiserikali, kwa kupitia mtandao wa Twitter, limekanusha madai hayo.

Ujumbe wa mtumiaji mmoja wa Twitter, Lubasha Jr, ulisema: #SautiZaWananchi is back. Kesho report ya Utafiti kuhusu Mtazamo wa Wananchi kwenye hali ya Uchumi inatolewa rasmi. Usikose.

Hapa chini ni kielelezo cha picha aliyoshiriki mtumiaji huyo

screenshot_20220825-002252_firefox-jpg.2333953

Hata hivyo, mtumiaji mwingine wa mtandao huo maarufu alijibu ujumbe huo kwa kuambatanisha na picha inayoonesha maandishi ya rangi nyekundu katika tangazo ambalo awali lilitolewa kwa umma na TWAWEZA, yakisema: IMEAHIRISHWA.

screenshot_20220825-002557_firefox-jpg.2333955

Ujumbe huo ulijibiwa na TWAWEZA ukikanusha taarifa hiyo kwa kuweka maandishi makubwa - karibu sawa na yale ya wapotoshaji - kuwa "HAIJAAHIRISHWA".
screenshot_20220825-002804_firefox-jpg.2333958


Ukurasa huo wa Twitter ndiyo unaotumiwa na taasisi ya TWAWEZA kwa shughuli zake rasmi. Hata hivyo, vyanzo vyetu vya kuaminika vimethibitisha kuwa ni kweli kwamba tukio hilo halikuahirishwa na liliendelea kama lilivyopangwa na kutolewa taarifa yake rasmi katika kurasa za mitandao ya kijamii na vyombo vya habari.

Tukio hilo lililofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard Hotel (SeaView) pia linaweza kuonekana kupiti kiunganishi hiki.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom