TWAWEZA: Upatikanaji wa maji safi na salama vijijini haujaongezeka ndani ya miaka 10 iliyopita

Sauti za Wananchi

Senior Member
Sep 2, 2014
113
138
Twaweza leo wamezindua Ripoti ya utafiti wao inayoitwa "Safi na Salama"?

Ripoti hii inawasilisha takwimu juu ya upatikanaji wa maji, njia za kutibu maji na usafi wa mazingira kwa ujumla.

Takwimu hizi zinajibu maswali kama:

Je, jitihada na uwekezaji katika Mpango wa Maendeleo wa Sekta ya Maji na ule wa Matokeo Makubwa Sasa vimeleta tija katika kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama na usafi wa mazingira kwa wananchi?

Je, ni njia kuu zipi za kutibu maji zinazotumiwa na wananchi?

Je, ni wananchi wangapi walioshiriki kwenye kampeni ya jamii ya kufanya usafi iliyohamasishwa na Rais Magufuli?

Moja ya Matokeo ya utafiti huu yaliyojumuishwa kwenye ripoti ni hali ya upatikanaji wa maji safi na salama:

========

Ili kupata picha halisi ya mwenendo wa upatikanaji wa maji, hasa katika maeneo ya vijijini, tunalinganisha takwimu juu ya upatikanaji wa maji kutoka awamu kadhaa za utafiti wa Sauti za Wananchi na takwimu zilizokusanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kupitia tafiti zake za kaya, pamoja na takwimu zilizoripotiwa na Wizara ya Maji (MoW) na matokeo yaliyoripotiwa na Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).

Mwenendo wa takwimu zilizokusanywa na NBS pamoja na Sauti za Wananchi zinanonesha kwamba upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo ya vijijini haujabadilika tangu mwaka 2015. Kati ya tafiti kumi na nne, kumi na mbili kati ya hizo zilikadiria kwamba kati ya asilimia 41 na asilimia 48 ya kaya zinatumia vyanzo vilivyoboreshwa kwa ajili ya maji ya kunywa.

Hata hivyo, takwimu za Sauti za Wananchi zinaonesha kuwa upatikanaji umepungua kutoka asilimia 55 mwaka 2014 hadi asilimia 46 mwaka 2016.

Wizara ya Maji imeripoti kuongezeka kwa kiwango cha upatikanaji wa maji kati ya asilimia 50 na asilimia 60, na takwimu za Matokeo Makubwa Sasa pia zinaripoti ongezeko la kasi kutoka asilimia 40 mwaka 2013 hadi asilimia 67 mwaka 2015.

maji1.JPG


=====























 

Attachments

  • SzW-TZ-2017-Water-KIS-FINAL-web.pdf
    1 MB · Views: 43
Watoke hapa hii nchi tangu uhuru maji ni kasma almasi maji yanapatikana mjini tu na kwenyewe ni shida vijijini huko wanakunywa maji na mifugo yao
 
always tafiti za TWAWEZA zipo safe na perfect 100%

sipingi kitu
 
Clean water is human right but thousands have no access. Just imagine for the past 10 years since 2007 very little have done to help find long term solutions. Does this mean we care no more for our own people? Nimeona jamaa anaitwa chakabars kwa kutumia account yake Instagram managed to raise $1m in 24 hours kwaajili ya Somalia. As a country we give so much attention to politics and politicians and forget what really matters to us.
 
Yan TWAWEZA tangu avurunde na tafiti zao za kumbeba Magu hakuna mtu anayejali tena kazi zao, tangu asbh uzi huu umewekwa lkn watu wanapita tu kama hawaoni vile!
 
Kukosekana wachangiaji kwenye hii mada ni ushahidi mwingine wa alichokisema Rais jana.

Dar es Salaam kuwa na bomba ni jambo moja, changamoto ni hilo bomba kutoa maji. Ni kama dawasco wana ubia na hao wafanyabiashara wa maboza!
 
Ukiskia Kauli za Rais na kauli za Wananch unaweza dhani....ni pale Watoto katika familia wavyo gundua baba'mnoko' wanaye ishi nae sio baba yao mzazi.....
 
Back
Top Bottom