Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,397
HATIMA ya hati ya kusafiria ya Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya Twaweza, Aidan Eyakuze, bado haijafahamika, baada ya Idara ya Uhamiaji kusisitiza kuwa itaendelea kuishikilia kwa muda usiojulikana.
Idara hiyo imesema kuwa ingawa bado wanaendelea kuishikilia hati hiyo, Mkurugenzi huyo anaweza kufuata masharti aliyopewa kama anataka kusafiri nje ya nchi kikazi.
“Tunaendelea kuishikilia hiyo hati, lakini kama anataka kusafiri yapo maelekezo ya ofisi ambayo tumempa ya nini anatakiwa kufanya, akitimiza anaweza kuruhusiwa kusafiri,” alisema Msemaji wa Idara hiyo, Ali Mtanda.
Mmoja wa maofisa wa Twaweza ambaye aliomba jina lake lisitajwe, aliliambia Nipashe hivi karibuni kuwa wamejitahidi kuifuatilia hati hiyo kwa muda mrefu, lakini wameshindwa kuipata na majibu ni kwamba uchunguzi unaendelea.
Alisema wamekuwa wakiandika barua mbalimbali wakiomba kupatiwa hati hiyo, lakini Idara hiyo imekuwa ikiwajibu kuwa inaendelea na uchunguzi ingawa hawasemi watakamilisha lini.
Ofisa huyo alisema Mkurugenzi huyo hajasafiri nje ya nchi tangu hati yake ishikiliwe Julai 24, mwaka huu hivyo amekuwa akikosa mikutano mbalimbali muhimu ya kimataifa na kikanda.
“Sisi tuna ofisi zingine Kenya na Uganda ambako alipaswa kwenda mara kwa mara kwaajili ya shughuli za kiofisi, lakini amekwama kutokana na hati hiyo kuendelea kushikiliwa na Uhamiaji,” alisema.
“Tunaomba mtusaidie kuwauliza Uhamiaji wanachotaka nini kwasababu miezi minne yote hawajachunguza na kupata taarifa wanazotaka au ni kumkomoa mtu jamani,” alisema ofisa huyo.
Alipozungumza na waandishi wa habari baada ya hati yake kushikiliwa Agosti, mwaka huu, Eyakuze alisema hakuelezwa sababu za kushikiliwa kwa hati hiyo ambayo alinyang’anywa Julai 24, mwaka huu.
Alisema alipokea wito kutoka Uhamiaji kwamba anatakiwa na baada ya kufika, aliambiwa aandike maelezo na siku ya pili alitakiwa kuwasilisha hati yake ya kusafiria.
Alisema Agosti Mosi, alizuiwa kusafiri kwa kutumia shahada ya dharura iliyotolewa kwa utaratibu uliopo ili aweze kushiriki mikutano ya kikazi kwenye ofisi ya Twaweza jijini Nairobi na Kampala, Uganda.
Chanzo: Nipashe