Twaweza na Wadau wa AZAKI wakutana na Wahariri wa Vyombo vya Habari kueneza uelewa wa Marekebisho ya Sheria 8 yaliyopelekwa Bungeni kwa dharura

Sauti za Wananchi

Senior Member
Sep 2, 2014
113
138
Ikiwa ni siku kadhaa tangu Asasi za Kiraia nchini kama sehemu ya wadau katika kuchangia mabadiliko ya sera na sheria mbalimbali kupokea mapendekezo ya marekebisho ya sheria nane tofauti (mapendekezo hayo yalifikishwa kwa Kamati ya Bunge ya katiba na Sheria kwa hati ya dharura), Twaweza wakishirikiana na wadau wengine wa AZAKI, walifanya mkutano na Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini ili kuwajengea uelewa kama wadau wenye nguvu ya kusaidia kupaza sauti dhidi ya suala hili lenye chembechembe za udhalimu.

Sheria hizo ni pamoja na Sheria ya Makampuni, Sheria ya Asasi za Kiraia, Sheria ya Takwimu, Sheria ya Vyama vya Kijamii, Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza pamoja na Sheria ya Wakala wa Usafirishaji Majini. Mabadiliko haya yanapendekezwa kufanywa kwa haraka kutumia taratibu ambazo kwa kawaida hufuatwa pale panapokuwa na jambo la dharura.

Kwa ujumla, mabadiliko yanayopendekezwa katika sheria hizo yanalenga kudhibiti utendaji kazi wa asasi za kiraia hivyo kuathiri namna wananchi wanavyoweza kufurahia haki yao ya kujumuika na kueleza maoni yao kwa uhuru, haki ya kushiriki katika maamuzi yanayowaathiri na kuwawajibisha viongozi wao.


Kujua msimamo wa AZAKI soma hapa >> https://www.jamiiforums.com/threads...bisho-ya-sheria-mbalimbali-juni-2019.1598471/

Katika mkutano huu uliofanyika hoteli ya Best Western Coral Beach jijini Dar es Salaam leo, mambo yaliyojadiliwa awali kabisa ni mikakati iliyoafikiwa na AZAKI kama njia za kuhakikisha mabadiliko haya yanapata mchango stahiki wa wadau.

1. Kuyatoa marekebisho haya kwenye hati ya dharura.

Moja ya dhana zilizojitokeza kwenye mkutano huu ni kwamba Serikali inataka kufanya mabadiliko ya Sheria ya Takwimu haraka iwezekanavyo kutokana na kutofautiana na wafadhili/washirika wa maendeleo ambao wametishia kusitisha misaada hivyo wamepenyeza mabadiliko ya Sheria zote nane ili kupitisha vifungu kandamizi.

Je, inawezekana Sheria zote 8 zikawa zinahitajika kuanza kufanya kazi kwa dharura?

2. Kuhakikisha marekebisho haya yanafahamika kwa umma ambao ndio unaathirika nayo.

Marekebisho haya yanamgusa kila mtu na si AZAKI pekee kwani yanagusa makampuni yaliyoajiri watu na yanayosaidia watu kwa namna mbalimbali, Asasi za Kiraia zinazosaidia jamii, vikundi vya kijamii kama vikundi vya kidini, makanisa n.k.

Hapa ndipo hasa jukumu la Wahariri linapokuja katika kuhakikisha wanatumia kalamu zao kufikisha ujumbe kwa umma, kuwahoji Wabunge ambao wako kwenye upande wa kupitisha Sheria n.k.

Mabadiliko ya Sheria yaliyojadiliwa kwa kina ni ya Sheria ya Makampuni, Sheria ya Asasi za Kiraia, Sheria ya Vikundi vya Kijamii na Ile ya Takwimu ambayo imefanyiwa marekebisho lakini bado hayakidhi haja kwa wadau wa utafiti na takwimu nchini.

Katika kuizungumzia Sheria ya Takwimu, Mkurugenzi wa Twaweza ambao wamekuwa wahanga wa Sheria hii iliyopitishwa mwishoni mwa mwaka 2018, ameeleza kuwa Serikali imelegeza uzi katika baadhi ya vifungu lakini bado kuna masharti yasiyo na lazima ikiwemo NBS kupewa jukumu la kusimamia taarifa zote za kitakwimu wakati awali walikuwa wakiwajibika kwa Takwimu rasmi pekee.

Pia kifungu namba 56 ambacho kinafafanua kifungu 24B kilichokuwa kinaeleza kuwa huruhusiwi kuchapisha taarifa za takwimu bila kibali cha NBS kimelegezwa ingawa kwa ubaguzi kinyume na Ibara ya 13 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani Taasisi kama World Bank, IMF n.k bila kuzitaja Asasi za Kiraia(CSOs) za nchini Tanzania.

Akizungumza kwa msisitizo, mmoja wa wawakilishi kutoka Twaweza ameelezea mchakato wa Utengenezaji Sheria na jinsi unavyokiukwa mara kwa mara kwa kutumia mwamvuli wa "Hati ya Dharura"

Utengenezaji wa Sheria unapaswa kuwa na ujumuishaji wa kutosha(inclusive enough) na wa majadiliano hadi kufika muafaka jambo ambalo upande wa Serikali haujalizingatia kwa kuwapa wadau chini ya masaa 48 kujadili mabadiliko.

Pia dharura haijaonekana kuwepo. Masuala ya usajili wa makampuni si masuala ya dharura, muda ungetolewa wa kutosha kujadili.
 
Back
Top Bottom