Twaweza: Asilimia 98 hawaifahamu vizuri sheria ya makosa ya mtandao, 69% hawajawahi kuisikia

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,441
7,780
Habari kwenu,

Wadau wa habari ikiwemo Baraza la habari Tanzania, LHRC na taasisi ya Twaweza wamekutana na waandishi wa habari na kuipongeza Serikali kwa kupitisha Sheria ya Upatikanaji wa Taarifa(2016).

Hata hivyo wamesema kanuni za kuratibu utekelezaji wa Sheria hiyo hazijatungwa na pia haijatangazwa rasmi ktk gazeti la Serikali. Baraza la Habari(MCT) limedhamiria kutoa taarifa kila baada ya miezi 6 kuhusu mwenendo wa matumizi ya Sheria hii.

Sehemu ya taarifa yake imesema wananchi wanapoomba taarifa kutoka mamlaka za serikali za mitaa, kwenye nyakati 2 kati ya 3 hunyimwa taarifa hizo.

TWAWEZA.jpeg

Twaweza kwa upande wake imesema wananchi wachache wana uelewa wa sheria ambazo zinawahusu. Sheria ya makosa ya mtandao ilipitishwa Aprili 2015 na kuingia katika utendaji Septemba 2015. Asasi za kijamii na waandishi wa habari walionya sheria hiyo kuwa na nguvu ya kuzuia mawazo kinzani na kuchochea wadau wa vyombo vya habari na wananchi kujidhibiti wenyewe. Asilimia mbili pekee ya wananchi wanasema wanafahamu kwa kina sheria ya makosa ya mtandao japokuwa asilimia 31 wameisikia tu.

Pia Twaweza wamesema asilimia 78 wanakubali uhuru wa kupata taarifa utasaidia kupunguza rushwa na maovu ilhali asilimia 60 wanasema serikali izuie taarifa ambazo ni muhimu kwa usalama wa taifa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za binadamu, Dkt. Helen Kijo‐Bisimba alihitimisha kwa kusema, “Kila Mtanzania ana haki ya kupata taarifa za serikali. Serikali wazi na inayowajibika lazima iwahakikishie wananchi wake uhuru wa kupata taarifa.

Mwaka 2016 serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilipitisha Sheria ya Upatikanaji wa Taarifa lakini sheria hii imeacha mambo mengi yasiyo ya kawaida ambayo yanahatarisha haki ya kupata taarifa.

Kwa mantiki hii tunaiomba serikali kupitia na kuanisha mambo hayo kuhusu Sheria ya Kupata Taarifa kabla sheria hiyo haijaanza kutumika. Baadhi ya mambo hayo ni muda wa kusubiri kabla maombi ya taarifa kujibiwa, wananchi wa Tanzania pekee kuruhusiwa kupata taarifa, wigo mdogo wa taarifa zinazopaswa kutangazwa, utata katika kuzuia baadhi ya taarifa, ada kwa ajili ya kupata taarifa na mambo mengine mengi yanahitajika kupitiwa.”
 
Attachments

  • ATIDataPacket-KIS-FINAL.pdf
    955.2 KB · Views: 53
Hii sheria ina matobo mengi, jamaa wakiamua kuikazia wengi zaidi wataumia.
 
Twaweza katika uchwara wake.

Sheria , zinatakiwa kusomwa na wananchi na kueleweka na siyo serikali kusomea watu sheria.

Povu lisiwatoke wajameni.
 
Inawezekana katika hiyo asilimia 98 kuna asilimia 99.9 ambao hawajawahi hata kupata huduma ya mtandao wa intaneti:rolleyes:
 
Watanzania sisi watu wa ajabu sana: badala ya hao twaweza kuwaelimisha wananchi juu ya mambo hayo ya sheria wao wanakutana kupeana taarifa za majedwali ya asilimia. Mngeleta majedwali ya kuonyesha mmewafikia watu wangapi na kuwaelimisha hizo sheria ningewaelewa. Lakini hayo majedwali ya kugawania mafungu ni mwendelezo wa porojo zile zile tulizozizoea.
 
Kwanini watu wasipewe elimu, lakini pia bunge likapewa kazi ya kuandaa sheria hiyo badala ya kuwa na tabia za kutungia sheria vyumbani. Tanzania tumekosa heshima katika mihimili ya serikali. Huwezi jua thamani ya bunge, mahakama wala serikali.
 
Watanzania sisi watu wa ajabu sana: badala ya hao twaweza kuwaelimisha wananchi juu ya mambo hayo ya sheria wao wanakutana kupeana taarifa za majedwali ya asilimia. Mngeleta majedwali ya kuonyesha mmewafikia watu wangapi na kuwaelimisha hizo sheria ningewaelewa. Lakini hayo majedwali ya kugawania mafungu ni mwendelezo wa porojo zile zile tulizozizoea.

Hii imekaa sawa, elimu kwanza majedwali na %badae. Asante.
 
Hivi hawa jamaa hawawezi kufanya tafiti zenye tija kwa Taifa? Kila siku ni vitafiti vya ajabuajabu tu. Hii SACCOS inapaswa kuchunguzwa.
 
Watanzania sisi watu wa ajabu sana: badala ya hao twaweza kuwaelimisha wananchi juu ya mambo hayo ya sheria wao wanakutana kupeana taarifa za majedwali ya asilimia. Mngeleta majedwali ya kuonyesha mmewafikia watu wangapi na kuwaelimisha hizo sheria ningewaelewa. Lakini hayo majedwali ya kugawania mafungu ni mwendelezo wa porojo zile zile tulizozizoea.
Wao ni taasisi ya Utafiti na kazi yao inaishia hapo. Huwezi kufanya kila kitu hapa duniani, focus muhimu!
 
Wao ni taasisi ya Utafiti na kazi yao inaishia hapo. Huwezi kufanya kila kitu hapa duniani, focus muhimu!
Wanamwachia nani afanyie kazi hizo tafiti zao? Huo ni ugawanaji mafungu ya wafadhili usiokuwa na tija yoyote.
 
Wanamwachia nani afanyie kazi hizo tafiti zao? Huo ni ugawanaji mafungu ya wafadhili usiokuwa na tija yoyote.
Kazi itafanywa na wahusika either Serikali au taasisi binafsi. Wakijikita kufanya kazi za wenzao, ya utafiti itawashinda.

Halafu acha kuhesabu baraka za wengine maana naona hayo mafungu yanakuuma sana wakati huchangii hata senti na wala hawatumii jina lako kuomba.
 
Back
Top Bottom