Twaomba utupe vichaa, wale watakaotufaa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Twaomba utupe vichaa, wale watakaotufaa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Nov 16, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Nov 16, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  (Makala, dua, nakala, wazo, njozi, au kauli hizi za usiku zaweza kutumiwa na gazeti lolote au chombo chochote na kusambazwa kwa namna yoyote ile kwa mtu yeyote yule bila ya kubadili jina la Mtunzi au kufuta barua pepe mwisho wa makala hii).  Na. M. M. Mwanakijiji

  Kama Mbinguni yupo Mungu anayesikiliza sala na dua za wanadamu basi ningemtolea sala na dua hii. Na kama huwa anazijibu basi ningemwomba hili atupatie. Kiongozi kichaa anayeongoza kundi la viongozi wengine vichaa ambao watatufaa. Ni viongozi ambao ni timamu wakiongoza matimamu wenzao ndio waliotufikisha hapa tulipo leo hii. Kama walio timamu wameweza kufanya haya yote na haturidhiki je vichaa wanaweza kufanya vibaya zaidi? Jibu langu ni “hapana”.

  Ee Mungu wewe ndiye uliyeumba vitu vyote tunavyoviona na tusivyoviona. Ndiye peke yako Mtawala usiye na mshirika wala mbia. Ni pekee ambaye ndiye asili ya mema yote na asili ya kila kitu kilichochema. Uovu kwako wapingana na asili yako ya wema. Uovu wote hautoki kwako. Twaomba utupatie na sisi kiongozi kichaa anayeongoza vichaa ambao watatufaa!

  Tangu enzi na enzi na tangu historia ya historia umewapa wanadamu mahali katika sayari hii kupaita pakwao. Mahali ambapo kwa haki yote ya asili ni mahali pekee ambapo kwa haki ni nyumbani kwao na ni hapo wanapata usalama wa kweli wa maisha, mali, na hatima yao; Mahali ambapo wao si wageni wa yeyote bali wao hukarimu wageni na kuwapa nafasi kati yao. Katika hilo jamii za watu duniani zikakusanywa katika familia, koo, makabila na hata mataifa mbalimbali.

  Ewe Mungu, watu hawa uliowakusanya katika sehemu mbalimbali wanatofautiana kwa rangi, lugha, na tamaduni zao. Ni katika tofauti zao hizi bustani yako ya wanadamu yapendeza na kupendezeshwa na uzuri kama ule wa bustani ya paradiso ambapo mimea, ndege, wanyama, samaki, wadudu na kila kilichona uhai kilipata usalama wake. Ni katika uzuri huo wanadamu wakajijengea katika sehemu hizo maisha yao.

  Na katika kujikusanya kwao kama jamii wakaweka viongozi kati yao. Viongozi ambao waliwaona wanawafaa katika kutimiza mahitaji yao kama jamii. Mahitaji ya kugawanya haki, kusimamia ulinzi na usalama, na kuhakikisha kuwa watu wao wanaishi huru kutoka katika tishio lolote lile dhidi yao au maslahi yao kama jamii. Hivyo, jamii za kiweka wafalme, machifu, mafumu, watemi, wafalme, malkia, n.k

  Na jamii hizo zilipoelewa zaidi utawala wa demokrasia yaani mamlaka ya watu kwa watawala wao zikaanza kuchagua viongozi kati yao kwa kufuata sheria walizojiwekea wenyewe. Na pale watawala wao walipojinyanyua kinyume chao wananchi hao waliasi; sehemu nyingine walijiletea mapinduzi kama kule Ufaransa na Marekani, na sehemu waliwatimua watawala wao kutoka katika majumba yao ya kifahari. Na wakati mwingine walipewa vichaa!

  Na hata sehemu nyingine ee Mola, wanadamu wengine walijinyanyua juu ya watu wasio wenzao, wakijiweka kama watawala juu yao na kuwageuza wengine watumwa na makoloni yao. Na kwa miaka na vizazi waliendelea kuwatumikisha na kuvunja vunja hisia ya utu na tunu ya uanadamu wao; wakipandikiza hofu na woga, wakikoleza machungu na huzuni huku wakipalilia uduni na kutojiamini katika vizazi vya watu hao wazima na watoto wao wanyonyao. Na mpaka pale walipotokea wale vichaa kati yao; wale waliowafaa!

  Ndipo ukawapa mashujaa kati yao; na sisi kati yetu twawakumbuka Ee Mola tunawakumbuka kina Kinjekitile wa Ngwale, Mangi Meli Kiusa Bin Rindi Makindara, Chifu Mkwavinyika Munyigumba Mwamuyinga Mkwawa, wale watawala wa wakati huo waliwaona vichaa wa watu! Ndiyo! Tunawakumbuka kina Mtemi Mirambo, Mpambalyoto, Nduna Songea Mbano na mashujaa wenzake walionyongwa wakikataa kusalimu amri kwa watawala wao; walikuwa vichaa kati ya watu wao! Ee mola twaomba uwainue mashujaa kama hao kati yetu tena.

  Tunaomba utupe viongozi vichaa ambao hawatakimbia huku na huku kuwabembeleza wawekezaji wanyonyaji ili waje kutunyonya urithi wetu na ule wa watoto wetu! Tunaomba utupe viongovi vichaa ambao hawataremburiana macho na mafisadi tena wala kufanya nayo vikao wala kuwaundia kamati au tume ya kuwachunguza bali watasababisha sheria kufuata mkondo wake kokote itakakoelekea.

  Twakuomba uinue viongovi vichaa kati yetu kwani hawa timamu wametushinda!

  Kwani tumechagua watu timamu mara kadhaa na hali yetu imezidi kuwa mbaya. Leo hii katika taifa lililo na ardhi yenye rutuba, likizungukwa na maziwa makubwa ya Afrika, likikingwa na Bahari ya Hindi iliyojaa samaki bwelele na ikiwa na mifugo ya kila aina, wanyama wa mwitu na ndege wa kula na kutazama watu wake wanaishi kwa hofu ya njaa; ati tuna viongozi timamu!

  Leo hii katika nchi ambayo watu wanaishi katika utajiri wa kila namna ati tuna watu wanaishi kwa kuomba omba na kutegemea hisani. Kwamba katika taifa lenye kila aina ya raslimali ati leo tunashindwa kuzitumia na badala yake tunaagiza hata kandambili kutoka nje; samani kutoka ng’ambo na kwa aibu hata vitunguu na nyanya zetu hatuzioni zina ulingano wowote na zile za kigeni; viongozi wetu timamu ee Bwana wameendeleza hisia ya uduni na kujiona kwetu kulikofanywa na wageni!

  Wanavaa tai na suti za kupendeza; wanaendesha magari ya kuvutia huku wakitembea kwa kunesanesa utadhani ndio wamiliki wa nchi na mbingu; Ee bwana wanajiona wao ndio timamu. Wamekomba hela zetu toka Benki Kuu, huku wakilindana wameanzisha makampuni hewa ambayo majina yake yanaimbika kama nyimbo za kutambikia; Hawa walio timamu ee Bwana, wanatutaka tuwatukuze, kwa kuwapongeza kwa kutujengea kiwanja cha mpira, kwa “kutupa uhuru” ambao kwa kweli ni tunu yako wewe Mwenyewe uliyo juu na si zawadi yao kwetu. Hawa walio timamu wanaendelea kututawala wakituringishia mema, wakitutega kwa ahadi zao na wakiwaonea watu wetu na kuwafanya duni mbele zao kwa kutukuza usomi na utajiri wao; Ee Bwana twakuomba utupe vichaa!

  Hata kama hutatupa wewe mwenyewe kwa sababu nawe umeona kukata kwetu tamaa; basi wasababishe wainuke wenyewe kati yetu;

  Vichaa watakaoupinga ufisadi si kwa kutuhumu wengine ufisadi bali kwa kuwafikisha mahakamani wale mafisadi wanaowajua; usitupe kama Sofia Simba! – twakuomba utusikie!

  Vichaa watakaojiuzulu mara moja wakijua wanakabiliwa na tuhuma nzito zenye kuhusu uwezo wao wa kuongoza na maslahi yao binafsi; usitupe kama Andrew Chenge – twakuomba utusikie!

  Vichaa watakaosimama na kukiri makosa yao bila kutafuta kisingizio na kudai kuonewa na kudhalilishwa sana; usitupe kama Edward Lowassa – Twakuomba utusikie

  Vichaa ambao hawatakubali kutengeneza Mikataba mibovu huku wakijidai ni wasomi na wakijua wanauza urithi wetu kama njugu; usitupe tena kama kina Nazir Karamagi – twakuomba utusikie

  Vichaa ambao hawasimama juu yetu na kutaka sheria ziwapendelee wao, huku wakijichagulia tuhuma, majaji na adhabu wazitakazo wao bila kujali sheria zetu; usitupe kama Rostam Aziz – Twakuomba utusikie!

  Vichaa ambao wakiwa madarakani hawatatumia madaraka yao kujipatia habari ambazo watazitumia kuchota utajiri wetu na kuugawia familia zao na marafiki zao; usitupe tena kama Benjamin Mkapa – twakuomba utusikie

  Vichaa ambao hawatakaa kimya wakiona uovu ukitendeka kwa sababu wakiuekemea na wao wataitwa mafisadi; usitupe kama baadhi ya wabunge wetu – twakuomba utusikie!

  Vichaa ambao hawatavumilia viongozi wazembe kwenye safu zao hata kwa siku moja au viongozi ambao utendaji wao ni duni; usitupe tena kama fulani – twakuomba utusikie!

  Umetupa matimamu kwa muda mrefu na leo twaishi kama vichaa; twaomba utupe vichaa ili hatimaye na sisi tuishi kama timamu!

  Niandikie: mwanakijiji@mwanakijiji.com
   

  Attached Files:

 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Nov 16, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Mungu Mwenyezi hana hiana atakujibu tu sala yako_Our own Stalin is in making, and probably not very far from our vicinity...ila akitokea tusimkimbie maana atatunyoosha bila huruma.
   
 3. Wayne

  Wayne JF-Expert Member

  #3
  Nov 16, 2009
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 663
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mhubiri: Utujalie hayo baba, kwa njia ya Yesu kristo, mpatanishi wetu na mwombezi wetu.

  Waumini:Amen
   
 4. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #4
  Nov 16, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Sala nzuri na yenye kuamsha hisia za mabadilkoo kutoka kwa muumba wetu.

  Ila Maombi ya mwishoni hukutaja wahusika ili hali wanajulikanaaaaa...Kwa nn?????
   
 5. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #5
  Nov 16, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  nadhani tuko pamoja katika hili. cheki Maandiko na mabandiko havitoshi Mziwanda [​IMG] 13th November 2009, 11:05 AM
  Katika kuleta mabadiliko ya kidola kuna njia tatu, kwanza ya kikatiba, pili kuingia msituni, tatu kupindua uongozi uliopo. Hakuna njia ambayo si halali hapo. Uhalali na si uhalali inategemea na upande unaohusika kwenye harakati. Kwa tz kalam imetumika sana na hakuna badiliko. Katiba imechakalia kwenye kibeti chake. Watawala wamekuwa sugu kwa kwa kauli na maandishi ya watawaliwa. Hawahisi tena, kwa maana hiyo wanahitaji namna ya kuifanya milango yao mitano ya faham kuhisi. Mifano iko mingi Afrika ila njia zao wengine ni za kishenzi. Madagascar ni mfano mzuri. Bermuda ni mfano mzuri. Hatuhitaji njia ya msituni, tunahitaji mapinduzi. Yaweza kuwa ni traditional coup au mapinduzi ya fikra. Yote yanahusika. Adui anapoingia kwenye himaya yako unamkabili kwanza ndipo unaangalia aliwezaje kuingia. Adui si lazima awe mtu. Wadudu, fikra, mazoea, woga, n.k vinahusika. Ni wakati wa mapinduzi ama tuache kuchonga domo zetu. Tunaharibu rasilimali bure; karatasi, wino, fikra, muda, n.k. Nadhani ujumbe huu ni delivered, not only sent.


  Bado sijafahamu kuweka link
   
 6. Mike-Austin

  Mike-Austin Member

  #6
  Nov 16, 2009
  Joined: Nov 20, 2008
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunaomba hayo kwa njia ya kristu Bwana wetu, Amen
   
 7. E

  Engineer JF-Expert Member

  #7
  Nov 16, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu usitupatie vichaa watakaokuwa wanachukua posho mbili mbili kama wanavyofanya wabunge na mawaziri wetu. Usitupatie vichaa watakao kuwa wanatumia magazeti yao kuchafua wengine kama anavyofanya Mengi na Rostam
   
 8. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #8
  Nov 16, 2009
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hivi mgombea wako atagombea kupitia chama gani vile! yes nasema Mwakalinga
   
 9. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #9
  Nov 16, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Ee Mungu na ukasikie kuomba kwetu. Amen
   
 10. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #10
  Nov 16, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  amina na uwalete hao vichaa watutawale, watuongoze kuelekea neema na mafanikia, awakamate kina rostam na lowasa plus manji
   
 11. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #11
  Nov 16, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Eeh Mwenyezi tunakuomba utuletee vichaa kama Jerry Rawalings wa miaka ya 1980 tuweze kusafisha uoza huu uliopo na kuanza upya. Twakuomba utusikie. Eeh Mwenyezi utuletee kichaa kama Idd Amin angalau afanye jambo moja tu nalo ni kuweka uchumi wetu katika mikono ya wazalendo. Twakuomba utusikie.
   
 12. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #12
  Nov 16, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  kwa DUA hizi , mimi naamini Mungu wetu sikiziwi hata kilio chetu kisisikiwe masikioni pake, na tuendelee kusali, na kuomba kwa nguvu zote
   
 13. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #13
  Nov 16, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,867
  Trophy Points: 280
  Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa!
   
 14. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #14
  Nov 16, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  na maarifa ni kuwatoa kafara wana CCM WOTE BILA HAYA WALA HURUMA, KISHA KUMKATA LOWASA, RA na Manji.
   
 15. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #15
  Nov 16, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Mch. Abihudi Misholi anasema mwaka huu usipite bila kutenda Muujiza
  Na dada Kabula anasema Mungu adhihirishe uwezo wake.

  Kuna January moja itakuja kuja ambapo tutapata uhuru wa kweli, inaweza ikawa January ya 2011 au 2016 au 2021 lakini kuna siku tutaamka wapya na tanzania mpya yenye nuru mpya.
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Nov 16, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  amin!
   
 17. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #17
  Nov 16, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Naona umeanza na "kama", neno linaloashiria kutokuwa na uhakika.

  Zaidi, nimefurahi kuona kwamba humtolei sala, ila unasema "ungemtolea" jambo linalotilia mkazo imani yako ndogo na huyu mungu.

  Ukweli ni kwamba mungu katengenezwa na mafisadi pamoja na maganga-ongo, ili wakati nyinyi mnaendelea kusali na kupiga dua, wao wawe wanaendelea kufisadi kilaini tu.

  Ni wakati wa kuacha sala na dua na kufanya kazi ya kweli kuelekea kumaliza dhahama hizi. Tumesali na kuomba dua tangu kabla ya mkoloni lakini hali yetu inazidi kuwa mbaya, mungu huyu wa kuchongwa na binadamu si mungu wetu.
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Nov 16, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  kama huyo Mungu hayupo basi vichaa wajitokeze wenyewe ili tusije tukambebesha lawama Mungu za bure...
   
 19. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #19
  Nov 16, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135

  Now you are talking.
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  Nov 16, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Na sense watu kukata tamaa kwa kiasi flani. Kubadilisha fikra za Miafrika si lelemama.
   
Loading...