Twafa na faini za barabarani zilizo kali kama moto wa tanuru..

mbongowakweli

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
841
671
Madereva wenzangu, faini tunazokumbana nazo kwa kipindi, nafikiri haijawahi tokea kwa miaka mingi mno.
Kweli makosa yanatendeka, rushwa hawataki, HAKUNA KUBISHA WALA KU CONTEST MAKOSA YAKO, AIDHA MAHAKAMANI WALA KWA TRAFIKI HUSIKA.
PIA HAKUNA KULIPA KIDOGO KIDOGO (INSTALLMENT), YAANI NI MZIGO WOTE, PAA..!
Je tunaelekea wapi?! Ghafla imekuwa chanzo kizuri sana cha mapato Serikalini, ghafla haya mafaini yamegeuka visasi kwa ma-Trafiki na madereva, ghafla umekuwa mradi kabambe sana, hasa baada ya ma-Trafiki kutuleta mjini kwa haraka na kuturudisha hivyo hivyo!
Dola imedhamiria kila kitengo husika lazima kizalishe pesa!
Labda ni mawazo yangu tu..Mnasemaje wenzangu?!
 
Binafsi nimeamua kutokwenda na gari kazini nimelipaki na sasa nina amani tele kwani kila siku ugomvi na trafic siwezi na hela yangu naamuaga nile nyama choma(mishikaki) na ndizi choma jioni au kuku wa kuchoma jioni kiulaiiiiiiiiiiini.
Uamuzi makini sana huu especially kama uko mikoani/karibu na ofisi lkn ukikuta unakaa huko vigwaza/mwanagati afu ofisi iko mjini kati aisee ni changamoto.
 
Tatizo hakuna anayekubali enda mahakamani

Makosa kama kuvuka pundamilia
Kufunga mkanda
Overtaking

Haya ni makosa ambayo ushahidi wake mgumu sana labda akurekodi video

Makosa ya wazi ni speed japo unaweza wabishia kama hawajaonesha kibao ulichovuka

Uchakavu wa gari
 
Ukweli mahakamani haki inaweza ikapatikana ingawa wengi wanahofia gharama ya muda watakaopoteza ukipiga hesabu ni bora utoe mlungula au uandikiwe karatasi elfu 30 kuliko kukomaa kwenda mahakamani ambapo huenda ukatumia gharama zaidi na ukapoteza muda.

Mapato yanayokusanywa kutokana na faini za barabarani na matrafiki mengi ni DHULUMA.

YANA MWISHO HAYA NA MWISHO UMEKARIBIA.
 
Madereva wenzangu, faini tunazokumbana nazo kwa kipindi, nafikiri haijawahi tokea kwa miaka mingi mno.
Kweli makosa yanatendeka, rushwa hawataki, HAKUNA KUBISHA WALA KU CONTEST MAKOSA YAKO, AIDHA MAHAKAMANI WALA KWA TRAFIKI HUSIKA.
PIA HAKUNA KULIPA KIDOGO KIDOGO (INSTALLMENT), YAANI NI MZIGO WOTE, PAA..!
Je tunaelekea wapi?! Ghafla imekuwa chanzo kizuri sana cha mapato Serikalini, ghafla haya mafaini yamegeuka visasi kwa ma-Trafiki na madereva, ghafla umekuwa mradi kabambe sana, hasa baada ya ma-Trafiki kutuleta mjini kwa haraka na kuturudisha hivyo hivyo!
Dola imedhamiria kila kitengo husika lazima kizalishe pesa!
Labda ni mawazo yangu tu..Mnasemaje wenzangu?!
Kijana fuata sheria za barabarani ama la Paki chombo chako uepuka faini za barabarani
 
Tatizo hakuna anayekubali enda mahakamani

Makosa kama kuvuka pundamilia
Kufunga mkanda
Overtaking

Haya ni makosa ambayo ushahidi wake mgumu sana labda akurekodi video

Makosa ya wazi ni speed japo unaweza wabishia kama hawajaonesha kibao ulichovuka

Uchakavu wa gari
Tatizo ni mahakama zenyewe mkuu, unaeza enda huko ukapoteza muda , labda kama mahakama zianzishe kitengo cha kesi za barabarani,
 
Umefanya jambo la maana....Ila kwangu madaladala bado changamoto

Msongamano mkubwa wa abiria ... hatari ya kuambukizana magonjwa
Migomo ya madereva na wamiliki wa daladala ... kutokuwepo uhakika wa kufika kazini kwa wakati
Inapotokea kuna foleni kubwa njiani ... ni ngumu kutafuta njia mbadala/kukosa flexibility
 
Hawa watu aisee ni kuwa nao makini tu kwa kila hatua wandugu. Kuacha kuendesha nayo ni changamoto pia kwa baadh ya watu hawawezi public transport. Ila ukiwa makini huwezi kupata fine na kuwapa hela kiurahisi rahisi.

Kwenye Zebra simama, kwenye taa ya njano simama basi. Nafkiri kwa mjini makosa mengi ni Zebra na Taa ya njano.

Vitu kama speed labda ukiwa mkoani, lakini pia kwenye 50km/h nenda 50 tu utafika kuliko kusimamishwa ukapoteza muda na pesa.

Mwisho wa siku binadamu hatujakamilika lazma utakosea tu hata kwa bahati mbaya, ila hata mwenyewe utaona kabisa kuwa leo nimeteleza bahati mbaya lakini sio daily tu uwe unawapa pesa.

Lazma uumie aisee.
 
traffic wa vigwaza wanaomba rushwa kwa nguvu ukikataa wanakulima fine ,yani mtu anasimamisha lori akija anafungua mlango anatega mkono,na si chini ya elfu tano anayoitaka,ni kama walishafanya kamuradi vile,nimekuwa nikipta hapo mara kwa mara zamani nilisikiaga tu zamani ila sasa nimejionea,yani ukitaka mema toa tu elfu tano yao uondoke la sivyo gari yako itaondoka na fine ya ajabu.wanapata hela sana we jiulize kila lori inatoa elfu tano inayotoka dar kwenda mikoani ndo utaratibu wao huo inaumiza sana ila basi tu.
 
Back
Top Bottom