TVT, Star TV washinikizwa kutoonyesha Bunge

Asha Abdala

JF-Expert Member
Mar 21, 2007
1,130
44
Kutokana na uzito wa Hotuba ya Dr Slaa, msemaji wa kambi ya upinzani ofisi ya Waziri Mkuu inayotarajiwa kuwasilishwa saa 12 jioni leo; TVT na Star TV wameshinikizwa kuacha kuonyesha kikao cha Bunge. Inaelekea Slaa alipanga kuanika masuala yote ya EPA, Richmond, Kamati ya Bomani, Kiwira nk. Tufanye kampeni ya haraka ya kuwashikiza kuonyesha

Asha
 
Kutokana na uzito wa Hotuba ya Dr Slaa, msemaji wa kambi ya upinzani ofisi ya Waziri Mkuu inayotarajiwa kuwasilishwa saa 12 jioni leo; TVT na Star TV wameshinikizwa kuacha kuonyesha kikao cha Bunge. Inaelekea Slaa alipanga kuanika masuala yote ya EPA, Richmond, Kamati ya Bomani, Kiwira nk. Tufanye kampeni ya haraka ya kuwashikiza kuonyesha

Asha

SIRI KALI!!!!! Duh! Wawaonyeshe wale wa upande wa mafisadi tu wakisema uongo!!!!!
 
Ndio nikasema CCM na ZANU PF wanafanana kwa kila kitu sema wapo nchi mbili tofauti. Hawa CCM siku wakipambana na upinzani wa kutishia kutolewa madarakani tutawashuhudia wakitembea bila nguo barabarani.
 
yale yale kwa kwa Mugabe .Then mnaema oh tanzania tuna nafuu .Yaan hata ya kusema ukweli mnazima TV duh!!!
 
Of course ni aibu kwetu opposition kutokuwa na chombo cha habari chenye kutetea maslahi ya wananchi hata baada ya miaka 15 tangu huru wa vyama vingi uanze. Hivi vyombo vyote vya habari vya TV vinamilikiwa ama na sympathisers wa CCM au watu ambao hawana ubavu wa kusimama wima CCM wakikohoa. This is a wake up call!
 
Huu ni UDIKTETA ambao umekidhiri. U-DICTATORSHIP huwa na mwisho. Na mwisho umekaribia, hawa CCM hawajui kuwa hii ni Karne ya Sayansi na Teknolojia. Nadhani bila ya wao kujua mawasiliano ya Internet yatawaangusha.
 
Olesendeka ,anatumia kanuni kumzuia Slaa na anasema kuwa CCM hawaibi kura ,ukisoma kwenye hotuba yake utaona kuwa alisema ilidhihirika wazi kuwa wanaiba kura sasa Dr .SLAA anawaambia kuwa wasome kanuni za 63.4 kuwa anayesema kuwa kasema uongo basi yeye kakataa na kumuumbua kuwa hajui kanuni kwani kanuni zinasema kuwa aliyesema ndio athibitishe .
 
Ni nchi gani nyingine zinazotangaza live majadiliano ya bunge?Kwa maana tangu kikao kinapofungliwa hadi mwisho?

Nadhani ni nchi chache sana duniani na hili lina maana yake.Kama ndani ya nyumba kuna siri ya familia si vema kuanika kila kitu.

Naunga mkono Majadiliano yasiwe wazi ili kulinda hadhi ya nchi.Kama kuna jambo llinalohitajika kuwekwa wazi zipo Hansards.

Bunge halitakiwi kuwa so transparent kiasi hiki.
 
Zittpo anawataka wabunge wa CCM kukaa kimya na sasa wabunge wa CCM wanazua fujo na kupiga kelele mpaka zitto anashindwa kutoa hoja.

Fujo zipo bungeni sasa jamani
 
Funzo kwa wana JF .
Mmesha madhara ya ku pre empty issues .naomba from now we learn from this error .It is a huge mistake we have done na sasa watanzania wanakosa kumsikia Mzee akiunguruma .Shame on CCM lakini yana mwisho .waandishi wahoji kulikoni .Next time naomba wana JF wavumilie kuleta ngoma hadi mambo na matuko yaishe nasi tuna mwaga .They got terrifieed baada ya kuona ama kawaida JF we are far ahead of them na sasa wamefanikiwa kuzima TV zao .

Endelea kutuma habari zote mkuu
 
Of course ni aibu kwetu opposition kutokuwa na chombo cha habari chenye kutetea maslahi ya wananchi hata baada ya miaka 15 tangu huru wa vyama vingi uanze. Hivi vyombo vyote vya habari vya TV vinamilikiwa ama na sympathisers wa CCM au watu ambao hawana ubavu wa kusimama wima CCM wakikohoa. This is a wake up call!

Hili la kutokuwa na TV yenu mlipe kipaumbele ili katika miezi 12 ijayo muwe na channel yenu inayopatikana kila kona ya Tanzania kwa bei nafuu sana au bure.
 
unafikiri mtu akipitiwa na kusema kuingia msituni si wa kumlaumu kwa sababu kuna mambo yanatia hasira sana!Haya sasa kama hili tena
 
JAMANI HIVI HUYU TIDO NA AKINA SUSAN NDIO WANATUFANYIA USHINZI HUU WATZ TUMEACHA SHUGHULI KUWAHI KWENYE TV KUMBE HAMNA KITU JAMANI.WALAANIWE TUNAIMANI FMES UTATUHABARISHA TU NA WENGINE MLIO HOME.another ufisadi
 
Katika ulimwengu wa leo, huwezi kuficha habari ama kunyamazisha wana habari!

unajua CCM wanachokosa ni "washauri" wenye ufahamu! Mara zote washauri wao wamekuwa wakionyesha ufahamu mdogo kama ule wa kumuadabisha Zitto Kabwe kwa kudanganya Bunge, walifikiri itaishia pale, lakini matokeo yake walijuta (ktk historia ya Tanzania, haijapata kutokea Mawaziri kuzomewa hadharani!!)!

Karamagi kuficha mkataba wa Richmond! mnajua yaliyompata ...

Acha waendelee kujichimbia kaburi! Wanatwanga maji kwenye kinu, kwani kesho habari yote itakuwa kwenye magazeti!
 
Jamani kumbe hatuna viongozi wetu hawako kwa ajili ya kuwatetea wananchi hili tumelishuhudia sasa. nafikiri kila mtu atume ujumbe wa Dr. Slaa kwa watanzania wote wenye E-mail. Huu ni uhuni.
 
Tatizo ni kuwa ukijaribu kuficha kitu mara nyingi ndo wengi wanapata access
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom