TvT hebu angalia hii pliz

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Huenda mkiangalia wenyewe mtaweza kuona cha kufanya kwenye hii logo yenu mpya...

TvT1.jpg

TvT2.jpg

Ni mawazo yangu kama mzalendo kuwa logo hii na hata ile ya zamani ni pana sana kama kuna uwezekano fanyeni kuzipunguza zitapendeza zaidi ya sasa.

Invisible
 
Kama 'allergy' na mtandao imeisha then wataona hili wazo lako mkuu, otherwise weka kwenye bahasha utume kwa njia ya posta.
 
Asante Invisible,

Tatizo la serikali siku zote wanashindwa kutangaza tender na kushindanisha watu ili kupata Logo Nzuri,Na ndio matokeo ya Vazi la ajabu la kitaifa.hii itakuwa na harufu ya Rushwa Tu.

Siku Zote Logo inafanya Picha ya Television ivutie.Angalia logo ya ESPN,CNN,BBC na zingine ambazo ziko juu,ina mvuto flani na inasisimua..

sidhani kama wataweza kubadilisha sabau hata Mhe. Rais Leo asubuhi alishaizindua TBC.

ila kwa ushuri wa Bure naomba waibadilishe,na wakitaka niwasaidie mawazo nipo tayari.Steve D upo?
 
Shirika La Habari Ndio Limezinduliwa Hivyo

Unajua Kama Mtoto Anapozaliwa Huanza Kutambaa Na Kisha Kutembea

Nyinyi Ndio Wananchi Na Ndio Wadau Wa Habari

Tunapopata Maoni Kama Haya Tunashukuru Sana

Ahsanteni Ndugu Watanzania Kwa Uzalendo Wenu
 
siku hizi uko tbc swahib??????
 
Mimi nawapongeza sana Mkurugenzi na Wafanyakazi wa TBC. Mwanzo mzuri... na Kwa kweli changes kwenye taasisi ya Serikali sio jambo rahisi hata kidogo... kuna watu wengi wanapenda kufanya kazi kwa mazoea.

Kwa vyovyote vile inahitaji moyo... Logo itabadilishwa kidogo with time... that is not a big deal... ila ninauhakika logo sio mbaya hata kidogo.

Waweza ushindanishe watu... mwishoni pia, uchukue logo mbaya...mifano tunayo logo ya TTCL kabla ya MSI ilikuwa mbaya sana. nitawakumbusha logo zilizobadilishwa karibuni angalieni ya TCRA imezinduliwa miaka si mingi na sasa inamabadiliko madogo...

Hongera TBC... taarifa za habari ni nzuri kuliko za famous TV... in Bongo

Mh. Tido au Wafanyakazi wako kama wanatembelea huku... Tafadhali sana tunawaomba muwe na Website yenu. Pia nawashauri muwe na uhusiano wa Karibu sana na TSN.. wachapishaji wa Daily News, Habari Leo, Sunday News etc...

Infact I don't why haya mashirika mawili hayapo pamoja, especially kipindi hiki ambacho consolidation is the way of life....

Pale guardian, habari zingine zinazouzwa kwenye alasiri, ndiyo inayoenda guardin, nipashe, etc... meaning they enjoy being in the same media house.

Ila ile TBC wasingefanya kwenye italic!!!
 
Thanx Invisible,
Kumbukumbu zangu zinanionyesha hii logo inataka kufanana kidogo na ile iliyokuwa ikitumiwa zamani na KBC Kenya! hasa ukiangalia kwenye yale maigizo ya Vitimbi utaiona!
Does it mean hatuko creative enough au ndo tayari Kenya ndo tunawatumia kama benchmark?
 
Huyu Tido awali alipotoka RTD alienda KBC ama BBC Nairobi nandhani ana-legacy za KBC na ndiyo maana unaona kitu TBC kinafanana. Mimi nitachora nembo ya TBC na kuiweka hapa mkiona inafaa basi tuwape wabadili. Si lazima kutumia nembo kubwa kama bango la matangazo barabarani.
 
Hiyo logo ya mdau hapo juu ni ya kiubunifu zaidi kuliko hilo la TBC iliyofufuka.Mimi nadhani walitaka kuiga ya KBC wakaishia na kitu ambacho hakiko katika standard.Kingine inawezekana hata settings za hao ma IT wao.
 
Bubu hako kako me nadhani kanafaa tena by far ulikilinganisha na hilo la kwao issue ni kuwa watakachukua/watakakubali hao TVC (TV ya ya ccm). Ninawaita hivi kwani most of the times wanaboa sana mwanzo mpaka mwisho ni mambo ya CCM tu mpaka basi hata kama ndio chama twawala lakini huwa inazidi s'times.
 
hiyo logo mbona inafanana na ya kbc ya kenya? watanzania shida yetu kubwa ni moja......creativity zeroo!!! Mhando na Mungi angalau wameleta a breath of fresh air tvt, inaangalika siku hizi. zamani utafikiri inaangaliwa na wanakijiji cha ujamaa tu!!
somebody fix em a new logo please
 
Hapo vipi wana JF nadhani katafaa haka naomba mchango yenu.

Inapendeza kuona kuwa watanzania walau tuko makini pale tunapoona mapungufu na kujaribu kutoa mapendekezo kama alivyofanya ndugu Bubu 'Msemavizuri' na nadhani kama kuna mdau ambaye walau ana mawasiliano na wenzetu hawa awafahamishe mapema juu ya hili na kuwa hatuwezi tukakubali sisi kama watanzania kuona chetu kinakuwa kibaya!

Tunalipenda taifa letu na tunapenda kuona kila chetu kinakuwa mfano wa kuigwa na wenzetu na si aibu hizi za kunukuu vya wenzetu ambavyo hata hivyo ni almost wameachana navyo. Binafsi nilipoiangalia hiyo logo nilihisi haikuwa na ubunifu kabisa. Wajaribu kufanya marekebisho muhimu mapema na kuweza kukubaliana na hali halisi kuwa logo kubwa kiwango cha kufunika maandishi na ambayo ni wazi ni kopi ya KBC ni kituko kwa kizazi cha sasa. Hatuko tayari kuburuzwa katika mambo ambayo watanzania tuna uhakika tunaweza kufanya BURE. Kama vipi tunaweza kutoa ombi kwa watanzania popote walipo kutoa mapendekezo ya logo ya TBC na ikapendeza sana kuliko hii ambayo binafsi naona ni moja ya vitu vinavyoondoa ladha ya kuangalia TBC.

Ni mawazo yangu tu
 
jamani sasa hivi nasisi basi tubadilike na twende na wakati mdau hapo kwa logo hiyo bora mara 100 kuliko ya baba tido utafikiri bado ndio wageni kwenye haya maswala!
tunachotakiwa kutoa mashindano tu kwenyekutengeneza logo mbona world cup na olympic wanafanya ivo...
mdau endelea kucheza na sanaa
 
Inapendeza kuona kuwa watanzania walau tuko makini pale tunapoona mapungufu na kujaribu kutoa mapendekezo kama alivyofanya ndugu Bubu 'Msemavizuri' na nadhani kama kuna mdau ambaye walau ana mawasiliano na wenzetu hawa awafahamishe mapema juu ya hili na kuwa hatuwezi tukakubali sisi kama watanzania kuona chetu kinakuwa kibaya!

Tunalipenda taifa letu na tunapenda kuona kila chetu kinakuwa mfano wa kuigwa na wenzetu na si aibu hizi za kunukuu vya wenzetu ambavyo hata hivyo ni almost wameachana navyo. Binafsi nilipoiangalia hiyo logo nilihisi haikuwa na ubunifu kabisa. Wajaribu kufanya marekebisho muhimu mapema na kuweza kukubaliana na hali halisi kuwa logo kubwa kiwango cha kufunika maandishi na ambayo ni wazi ni kopi ya KBC ni kituko kwa kizazi cha sasa. Hatuko tayari kuburuzwa katika mambo ambayo watanzania tuna uhakika tunaweza kufanya BURE. Kama vipi tunaweza kutoa ombi kwa watanzania popote walipo kutoa mapendekezo ya logo ya TBC na ikapendeza sana kuliko hii ambayo binafsi naona ni moja ya vitu vinavyoondoa ladha ya kuangalia TBC.

Ni mawazo yangu tu
Yey Mawazo Mazuri..ila inabidi bubu aiweke Vizuri Mistari ya Bendera na aadjust Resolution.otherwise inabid Invisible uwatumie TBC
 
Hapo vipi wana JF nadhani katafaa haka naomba mchango yenu.

View attachment 1333

Serious people always have simple logo! umejitahidi lakini...binafsi napenda logo zisizokuwa na nakishi...

mfano... logo ya CNN, logo ya CISCO, Sun Microsystem, HP, Dell, SAP etc..

Kwa hivyo TBC ningenda Iwe as simple as it can be... infact bila background yoyote... maneno yabebe rangi zote mnazotaka kuweka... lakini mupunguze nakshi...

Kwa sasa nawashauri kwamba logo waliyonayo waitumie kwenye mabango yao na makarasi yao headed paper!

Logo kwenye TV yao waondoe ile background...
 
Logo kwenye TV yao waondoe ile background...
Hahahaha! At last umekubali mkuu. Logo hiyo haijakaa vema kabisa. Tatizo nikituma mails kwao zinasema "mailbox" yao imejaa. Sijui huwa wana limit ya mails kuingia? Ingependeza sana wakajua watanzania tuna maoni gani.

These changes have to take effect immediately!
 
Walau wameipunguza ukubw a na sasa inavutia! Interesting

mmm.jpg

nnn.jpg

BTW: Kwa sasa TBC1 ina mvuto na inatia moyo. Nice move Mhando!

Machache yanayohitaji mabadiliko tutakuambieni taratibu na tungependa kuona ufanisi daima. Kila la kheri katika ujenzi wa taifa

Invisible
 
Kuna mabadiliko makubwa na mazuri.... kama wakiendelea hivi then TBC itakua bomba sana in the near future.
Kuhusu hii logo, wengeifanya ile background ikiwa transparent kidogo, isiwe solid.
 
Back
Top Bottom