Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature currently requires accessing the site using the built-in Safari browser.
Shirika La Habari Ndio Limezinduliwa Hivyo
Unajua Kama Mtoto Anapozaliwa Huanza Kutambaa Na Kisha Kutembea
Nyinyi Ndio Wananchi Na Ndio Wadau Wa Habari
Tunapopata Maoni Kama Haya Tunashukuru Sana
Ahsanteni Ndugu Watanzania Kwa Uzalendo Wenu
Thanx Invisible,
Kumbukumbu zangu zinanionyesha hii logo inataka kufanana kidogo na ile iliyokuwa ikitumiwa zamani na KBC Kenya! hasa ukiangalia kwenye yale maigizo ya Vitimbi utaiona!
Does it mean hatuko creative enough au ndo tayari Kenya ndo tunawatumia kama benchmark?
Hapo vipi wana JF nadhani katafaa haka naomba mchango yenu.
Yey Mawazo Mazuri..ila inabidi bubu aiweke Vizuri Mistari ya Bendera na aadjust Resolution.otherwise inabid Invisible uwatumie TBCInapendeza kuona kuwa watanzania walau tuko makini pale tunapoona mapungufu na kujaribu kutoa mapendekezo kama alivyofanya ndugu Bubu 'Msemavizuri' na nadhani kama kuna mdau ambaye walau ana mawasiliano na wenzetu hawa awafahamishe mapema juu ya hili na kuwa hatuwezi tukakubali sisi kama watanzania kuona chetu kinakuwa kibaya!
Tunalipenda taifa letu na tunapenda kuona kila chetu kinakuwa mfano wa kuigwa na wenzetu na si aibu hizi za kunukuu vya wenzetu ambavyo hata hivyo ni almost wameachana navyo. Binafsi nilipoiangalia hiyo logo nilihisi haikuwa na ubunifu kabisa. Wajaribu kufanya marekebisho muhimu mapema na kuweza kukubaliana na hali halisi kuwa logo kubwa kiwango cha kufunika maandishi na ambayo ni wazi ni kopi ya KBC ni kituko kwa kizazi cha sasa. Hatuko tayari kuburuzwa katika mambo ambayo watanzania tuna uhakika tunaweza kufanya BURE. Kama vipi tunaweza kutoa ombi kwa watanzania popote walipo kutoa mapendekezo ya logo ya TBC na ikapendeza sana kuliko hii ambayo binafsi naona ni moja ya vitu vinavyoondoa ladha ya kuangalia TBC.
Ni mawazo yangu tu
Hahahaha! At last umekubali mkuu. Logo hiyo haijakaa vema kabisa. Tatizo nikituma mails kwao zinasema "mailbox" yao imejaa. Sijui huwa wana limit ya mails kuingia? Ingependeza sana wakajua watanzania tuna maoni gani.Logo kwenye TV yao waondoe ile background...