TV za Tanzania Ingeni mfano wa BBC Swahili

Mchokozi

JF-Expert Member
Feb 9, 2012
215
29
Jana kuanzia saa tatu usiku kipindi cha BBC swahili kilianza rasmi kurushwa kupitia STAR TV kilichonifurahisha ni mpangilio mzuri wa habari pamoja na picha, ninachojiuliza kwa nini TV za Bongo zinashindwa kuwa na mpangilio kama wa BBC?? mfano kwa habari za Bongo utakuta habari haiendani na picha au pengine utakuta mtangazaji amemaliza kuelezea tukio lakini picha inayokuja inachelewa dakika kadhaaa...... Watangazaji na mafundi mitambo jifunzeni japo kwa kuangalia BBC swahili.
 
unawezaa kuweka clip ya hiyo habari ili sisi madongo kuinama
tuweze kufaidi uhondo pia?
 
Wacha waje waiue CCM. CCM walizoea kulazimisha media kutangaza wanachotaka, sasa hawa jamaa wataingia mpaka uvunguni kusasamua uozo na utamu. 2015 hapatoshi.
 
Back
Top Bottom