TV Ya JF: Safari za kwenda Marekani za Rais | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TV Ya JF: Safari za kwenda Marekani za Rais

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by X-PASTER, Jun 11, 2010.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Jun 11, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Safari za kwenda Marekani za Rais.

  XP: Watazamaji wa Television ya luninga, leo tena tunawaletea mahojiano yasio rasmi ya viongozi wetu vijana, yaliofanyika Ikulu nyeupe kule kwa bwana washilingi ya mtoni wenyewe wanaiita eti Washington. Mheshimiwa alidai hivi majuzi kuwa hana mpango na kura za wafanyakazi, kumbe ana kitu anacho kitegemea... kikamera chetu cha mchina kwa siri kilifanikiwa kunasa mazungumzo yalio rasmi lakini si rasmi baina ya mahendisamu hawa wawili. Mtatusamehe waungwana kwani picha kidogo ina sheki sheki...!

  Basi ndugu raisi Kikwe alikuwa akiteta na mwenyeji wake kama ifuatavyo.


  OBAM: Karibu Mshikaji, habari za huko?

  KIKWE: Ahasante mshikaji, mambo vipi? (Tabasamu kuuubwa na meno nje)

  OBAM: Poa, mshikaji. Vipi mambo? Hivi unaitwaje vile?

  KIKWE: Naitwa Kikwe au Jina la utani ni Vasco da Gama.... Rais wa bongo tambarare (uku akicheka cheka) si unajuwa ule mlima kili upo kwetu…!

  OBAM: Aisee! Mambo yanaendaje, Kikwe.

  KIKWE: Kama unavyojua tumo kwenye kuelekea uchaguzi.

  OBAM: Ah, mimi ndo nishaingia hivi, kwa hiyo kila kitu kitakuwa shwari. Lakini naona huna wasi wasi.

  KIKWE: Ah, wapi mshirika. Kuna jamaa hao sijui wanajiita Wapinzani. Wananitia mcheche kishenzi. Tena afadhali umeniuliza.

  OBAM: Sasa mimi nitakusaidiaje wakati ndio kwanza nami mambo ya Iraki na Afughanistan hayajaisha? Na Muiran si unamsikia naye anayo nyuki. Mimi nataka kuja uko kutalii, maana nilikuwa nasikia tu huku kuna mlima mrefu kuliko yote Afrika, halafu kuna wanyama kibao. Pia nilitaka na mimi niucheki tu ule mlima.

  KIKWE: Fanya lolote uwezalo, mshikaji. Unajua mimi nakumaindi sana. Si unajua Hayati Mzee Jully alivyokuwa hawamaind mayakii, anawaita mabepari. Sasa hivi hayupo ndio maana sioni noma kupanga majamboz na wewe, sio! Wewe mwenzangu uko freshi, tena rais wa dunia, si unaweza kunisaidia? (Tabasamu)

  OBAM: Ah, mimi niko freshi. Si unacheki hata madogi yangu yaliyocheki gari yako yalivyo?

  KIKWE: Oh, mshkaji una mijibwa balaa! Halafu unajua umenitoa nishai kwa walinzi wangu na raiya wangu wanao ishi uku, sasa yale ndo yalikuwa yanacheki nini.

  OBAM: Ah, unajua tena mshikaji, ulinzi ulinzi tu. Halafu si unajua mambo zangu, sasa maadui zangu wanaweza wakafanyiza kinoma noma, kwa hiyo yale madogi yakianza kuhakikisha usalama hayaelewi. Yanaingia tu kila mahali. Halafu mshikaji huku kwetu gari ya Rais huwezi kuijua upesi, iko sawa na ya meneja wa kiwanda. Kwa hiyo wale manjagu wangu hawakujua kama ile ndio gari ya lako.

  KIKWE
  : Sasa unapakaza mshikaji. Hebu tuongee maswala muhimu. Kabla kikao hakijaanza, utanisaidiaje?

  OBAM
  : Mimi ninachoweza kukusaidia ni ubabe tu, si unajuwa sisi makau boi. Zetu si unazijua? Mtu akijitia mbabe tunaingia tu tunabonda halafu tunaondoka. Akiwa sugu kama Saddam tunawaleta washirika wetu kibao tunasaidiana kum-bonda. Sasa wewe hao sijui ndio nani, hao unaowaogopa, wanahitaji ubabe au pesa?

  KIKWE: Pesa sio tatizo. Hao wao hawaangalii pesa. Unaweza kuwamwagia pesa na wakakuliza vile vile. Hao ubabe tu maana si unajuwa nina uchaguzi oktoba hii?

  OBAM: aah kumbeee... Sasa nipe ruhusa ya kuingiza vifaa vyangu.

  KIKWE: Vifaa gani mshikaji? Madogi au...!?

  OBAM: Ah, unazungumzia madogi!? Nipe ruhusa ya kuingiza zana zangu za angani. Mzee Jully ndio alikuwa mnoko sana, hakupenda mambo yetu, lakini wewe ukinipa ruhusa ya kuingia humu na ndege zangu hao jamaa zako wenyewe watafyata mikia. Sasa unasemaje? Nilete meli moja hapo ya Eakrafti karia (Aircraft carrier) USS Theodore Roosevelt hiyo oktoba, nataka bezi hapo si unajuwa wasomali tena?

  KIKWE: Yap, yap. Gonga basi! Hamna noma. Hiyo tu. Wala sina haja ya kuitisha kikao chochote. Mimi ndo Netanyahu wa huku. Leo hii hii tuandikishane. Tuweke mkataba wa anga huru, ili noma likiibuka uingie kiulaiini kunisevu.

  OBAM: Kwa nini tusipange siku nyingine.

  KIKWE: Hapana, linalowezekana leo lisingoje kesho.

  OBAM: Basi freshi, mimi nitasaini mkataba, halafu wakijidai wajuaji we unanitonya tu, naingia. Halafu uzuri wenyewe watu wako ni poa kishenzi, nasikia hawajui vita wala vagi, kwa hiyo mimi nitakusevu. Hata hivyo, mkataba huu utasaidia pia kudhibiti na wengine unaopakana nao, kama hapo Sudan na Somali wanapojidai wana siasa kali. Si unakumbuka tumewaweka kwenye listi yetu ya magaidi? Wakijidai tu natua kwako halafu nawabonda kishenzi kutokea kwako. Au vipi!

  KIKWE: Sasa tena, si unacheki, bonge la advanteji. Twende, naona namba saba anakuja, tuminye kwanza.

  OBAM: Sawa, mshikaji.

  M7: Vipi, naona mmekutana mahendisamu mnateta. Mnapanga jinsi ya kumaliza huu mgogoro wa wenzetu uko Darfuu?

  KIKWE na OBAM: Ndio!

  Kikamera chetu cha mchina kwa bahati ghafi i mean mbaya kikakata mawasiliano ya kwisha betirii...
   
 2. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  quite creative.....jitahidi ubadilishe hiyo kamera upate original....
   
 3. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Njoo nikuazime ya kwangu Mkuu; Asante kwa kuwasilisha
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Jun 12, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Jukwaa la siasa limegeuzwa kuwa la udaku?
   
Loading...