TV Ya JF Na Mwanasiasa Wetu Wa Kisasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TV Ya JF Na Mwanasiasa Wetu Wa Kisasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by X-PASTER, May 18, 2010.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  May 18, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Baada ya mageuzi ya hapa na pale, tovuti maarufu ijulikanayo kama JamiiForums, iliamua kuanzisha Television ya luninga, na kwa bahati nasibu kabisa nimebahatika kuwa mmoja wa watangazaji waandamizi wa television ya luninga wa mwanzo mwanzo kabisa kabla mafisadi hawaja fisadisha.

  XP: Kipindi cha leo ni cha tamthilia ijulikano kwa jina la Mwanasiasa wetu wa kisasa.

  Ndugu watazamaji, hii ni Television ya Luninga kutoka Jamiiforums ikiwajia moja kwa moja kutoka hewani... Leo tunawaletea tamthilia iitwayo "Mwanasiasa wetu wa kisasa". Katika Tamthilia hii tutaona jinsi Matata alivyopewa mtihani na wazazi wake na jinsi alivyoufanya. Karibuni sana (Tabasamu kuuuubwa si la kifisadi).

  Nyumbani kwa Baba Matata:
  Baba Matata na Mama Matata wanaonekana. Baba Matata anapanga vitu kadhaa mezani, huku Mama Matata akiwa anamuangalia.

  BABA MATATA: Leo nataka kujua kijana wetu Matata atakuwa nani akishaondoka hapa nyumbani. Vitu vyote hivi naviweka hapa ili avikute, halafu nitagundua atakuwa nani kutokana na kitu atakachochagua. Akichukua hizi pesa, basi atafanya kazi benki. Akichukua hii Biblia atakuwa mtu wa dini, kama sio mchungaji basi mhubiri tu. Akibeba hili boksi la nanihii atakuwa mtu wa wanawake, au muasherati hapo itabidi tumshughulikie mapema. Hii chupa ya pombe itatujulisha kwamba atakuwa bambata, yaani mlevi.

  MAMA MATATA: Weka basi na huu mkufu wangu.

  BABA MATATA: Hiyo ndiyo itatuonyesha nini?

  MAMA MATATA: Atakuwa kibaka, kwa hiyo tutamshughulikia kabla.

  BABA MATATA: Aisee mama Matata leo una akili!! Hebu weka hapo huo mkufu. Halafu nitaongeza na ile silaha yangu, pengine atakuwa mtu wa masilaha, labda polisi au askari.

  MAMA MATATA: Khe ! Je akiwa jambazi?

  BABA MATATA:
  Wewe mbona unamfikiria mabaya tu. Mara kibaka, mara jambazi!

  MAMA MATATA:
  Basi tuseme mwanamgambo.

  BABA MATATA:
  mfyuuu! Hebu tuondoke asije akatukuta hapa. Tukakae kwenye kale kadirisha kakutolea chakula tumuone akija atachagua nini.

  Baada ya muda, Matata anaingia, uku akipiga mruzi. Anafika mezani, anashangaa kidogo!

  MATATA:
  Siku zote wananiwekea chakula hapa, leo wameniwekea hivi vitu vyote. Nashukuru sana.
  (Anapitisha macho kuviangalia) Kufu la nguvu, mvinyo, boksi la soksi Duh! Ama kweli hawa wazee sasa wamekuwa. Nanga, neno la Bwana God Ila pesa wamepunja kidogo. Hata hivyo, si haba. Nakomba tu kiulaiiini. (Anaanza kuchukua vitu kuingiza chumbani kwake)

  MAMA MATATA:
  (Ananong'ona) He! Sasa mbona anabeba vitu vingi, tutajuaje?

  BABA MATATA:
  (ananong'ona) Ngoja tuone... kachukua pesa, pombe..eeeh.. na boksi la Cond... nanihii, na silaha. Mama yangu eeeh! Atakuwa mwanajeshi. Wanajeshi ndio wenye WWW! Sio world wide web ya internet ni Wine, Women na War.

  MAMA MATATA: Tutafaidi! Ndio vitu gani hivyo?

  BABA MATATA: Utafaidi? Nilikuona umeanza kupata akili, kumbe ni za sekunde tu. Wine ni pombe, women ni wanawake, na war ni vita. Hiyo ndiyo www ya jeshini.

  MAMA MATATA: Yobwa! Tuufwile nyaambala! Mbona kachukua na tule tupesa, hatakuwa benki?

  BABA MATATA:
  Sasa vitani ataenda bila kulipwa? Na wanawake na mvinyo atapata bila pesa?

  Mara Matata anatokea tena. Anachukua vingine vyote vilivyobaki mezani. Baba Matata anashika kichwa. Mama Matata amebaki kushangaa.

  MAMA MATATA:
  Jamani, sasa Matata wangu ndio atakuwa nani? Au atakuwa vyote?

  BABA MATATA: Lahaulaaaa!! Mke wangu, mwanao atakuwa mwanasiasa wa kisasa. Hao ndio wamechanganya vyoote alivyochukua Matata. Dalili ya ufisadi mke wangu... Yalaaah twafwaaa!

  -- MWISHO --

  XP: Ndugu watazamaji wa Televisheni yetu ya JF, kutoka jamiiforums, natumaini mmeburudika vya kutosha na tamthilia yetu. Tamthilia hii inaakisi moja kwa moja hali tuliyonayo katika jamii yetu.

  Hao ndio mfano wa viongozi wetu wa kisiasa. Hakuna wanacho kijuwa zaidi ya kujirundikia mali na kupenda kujitangazia kuwa wana vijisenti tu. Hali uku walalahoi ndio wenye kumenyeka kufanyakazi kutwa kucha, lakini ukapa ni kwa mlala hoi tu, kama vile Tanzania sio kwao.

  Maisha ya Mafisadi ni kama wapo peponi wangali duniani maana kwa upande wa viboksi vya nanihii ndio usiseme. Tunaona makasino yanavyokuwa mengi, karibu yatafikia idadi ya shule, Bei ya kwenda kasino sio ya kwenda kwenye mabaa ya mabambata ya kilalahoi. Mashindano ya wendauchi ndiyo hayo kila siku yanahudhuriwa na wanasiasa, kuangalia mabinti wa watu wakipita jukwaani na vichupi.

  Ukija kwenye dini, mafundi ni wao. Wao ni mashehe, wao ni mapadre, wao ndio maustadh, wao ndio maparoko. Na hawataki mwingine mwenye dini kuikosoa siasa, ila wenye dini wakisifu siasa zao utawaona wanatangwazwa kwenye redio na magazeti. "Shehe fulani kasema, Padiri fulani kanena" Kuna wale mashehe na mapadre wasiovuma, lakini kipindi cha kampeni kikifika wanakuwemo.

  Hivi ndivyo mwanasiasa wa kisasa alivyo. Ana vyoote alivyokomba Matata (pesa, pombe, neno la Mungu, silaha na maboksi ya nanihii). Na kinachotishia zaidi ni kwamba akina Matata bado wanazaliwa.

  Leo tutaishia hapa. Mimi ni mtayarishaji wako, XP, wa Televiheni ya JF kutoka jamiiforums. Tukutane tena katika kipindi kingine.

  Bye for now.
  (Tabasamu kuuuubwaaa na meno nje nje kama kaahidiwa Ubunge).
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mkuu X-Paster, kwanza hongera kwa ubunifu nambari moja ambao sijawahi kuuona tokea nijiunge na jukwaa hili, hongera sana ila kama utaniruhusu nipate niuchukuwe mchezo huu kuwafundisha vijana wa shule moja kule nyumbani kwa dhumuni la kutoa elimu ya uraia tu si biashara. Ulichokionyesha hapo ni ukweli na ukweli mtupu
   
 3. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #3
  May 19, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ruksa mkuu, bila kuomba unaruhusiwa.
   
 4. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #4
  May 19, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Ndo maana kila kukicha ooh jimbo langu... jimbo langu....
  Jimbo lako liko chumbani kwako buladi f@**%"l
  Kwa ulafi huo watakumbuka kuna wakinamama wanalala mzungu wa nne hospitalini!!
   
 5. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #5
  May 19, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,976
  Likes Received: 23,659
  Trophy Points: 280
  Hii thread imedeserve kupata Senksi yangu!
  Good stuff!
   
 6. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #6
  May 19, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Daa,stori tamu lakini usitusingizie wanasiasa..Tabia hizi zinakugusa karibu kila mahali,ukienda makanisani hali ndio hiyo,ukirudi kwenye asasi za kiserikali na mzisizo za kiserikali hali ndio hiyo,kwenye mabenk the same story.mashuleni halia kadhalika...ukweli ni kwamba wanasiasa ndio wanaoonekana zaidi thats why tunaona wao ndi wanadhambi sana..
   
 7. P

  PUNJE JF-Expert Member

  #7
  May 19, 2010
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 334
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  ...................Imetulia hiyo. ASANTE SANA
   
 8. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #8
  May 19, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  mkuu hongera kwa ubunifu wa aina yake hii bigup mkuu inabidi ss tuitengenezee video tuirushe hewani iwe tv live
   
 9. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #9
  Sep 9, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Tupo pamoja wakuu, ila Na hata JF wapo wamejaa tele...!
  Ndio hao tunao waona wakivurumisha matusi, wasio na hoja, waliojaa na kejeli...!
   
 10. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #10
  Sep 9, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Mkubwa imetulia hiyo.
   
 11. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #11
  Sep 9, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kichwa hicho hapa jamvini. Hongera sana mkuu!!!

   
 12. sidimettb

  sidimettb Member

  #12
  Sep 9, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ubunifu mzuri ,hasa kwa kuongeza vionjo.Ila ingekuwa vizuri ku aknowledge kidogo ,maana huu mfanao alishwahi kuutumia hata mkapa kwenye moja ya speech zake akiwaasa wanasiasa wenzake, can't remeber well,lakini ni kama wakati flani akihutubia bunge.

  Nimeamua kudokeza hivi maana nimeona kuna mtu jana ka copy na ku paste habari toka mwanahalisi inayosema-Ngeleja na Jairo hawatakiwi wizarani(Bila kutaja source).
   
 13. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #13
  Sep 9, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,289
  Likes Received: 22,054
  Trophy Points: 280
  Jubhaaaa, tufwile nnyambala
   
Loading...