TV Talk Show Ya "Changamoto za Mahusiano Na Ufumbuzi Wake" 22nd January 2014

Jul 14, 2008
1,820
1,031
Tunapenda kutoa mwaliko kwa wageni 30 tu watakaohudhuria katika kipindi kipya kitakachorushwa TBC1 siku ya Jumapili tarehe 26th January 2014 saa 3 hadi saa 4 usiku na kurudiwa siku ya Jumatano Tarehe 29th January 2014 saa 8 hadi saa 9 mchana. Wageni lazima wawe na uzoefu sana na mambo ya Mahusiano na wawe tayari kuleta changamoto katika kipindi au kusaidia kupata ufumbuzi wa tatizo.

Kipindi kitarekodiwa siku ya Jumatano saa 12 jioni hadi saa 2 usiku. Tafadhali thibitisha kuhudhuria kwako kupitia namba: +255 755 285 023

Mada itakayoongelewa na “Changamoto Katika Mahusiano na Ufumbuzi Wake". Wataalikwa Wataalamu mbalimbali na wazoefu wa mambo ya mahusiano kama wageni wawezeshaji.

Wale wote wenye michango ya msingi au maoni au ufumbuzi au maswali mnayopenda wahusika waulizwe pia mnaweza kuniandikia mapema.

TV Talk Show itajulikana kama "Wake Up & Change" au "Amka na Badilika" na ni kipindi kitakachorushwa kila wiki siku ya jumapili usiku na kurudiwa Jumatano.

1. Madhumuni ya Kipindi

a) Kubadilisha mitazamo ya watazamaji ili iwe mitazamo chanya zaidi kwa mambo mbalimbali pamoja na kuwahamasisha kubadili tabia na kuchukua hatua katika kukabiliana na matatizo.
b) Kutafuta na kutoa majibu kwa masuala muhimu yanayohitaji kupatiwa ufumbuzi au utatuzi wa matatizo na pia kujibu maswali yanayohusiana na mada husika kutoka kwa watazamaji waalikwa.
c) Kukifanya kipindi kama jukwaa la majadiliano katika mambo muhimu ya kijamii na kitaifa na kuhamasisha mabadiliko chanya.

2. Ubunifu wa Kipindi

Kipindi kimebuniwa ili kuleta majadiliano yatakayoleta hisia kwa wote watakaohusika katika mjadala na pia watazamaji. Jambo hili ni muhimu zaidi ili kuleta matokeo chanya kwa wote wanaoangalia kipindi. Kwa ujumla kipindi kimebuniwa kutatua matatizo mbalimbali ya watu binafsi, familia, jumuiya, jamii na taifa kwa ujumla huku kikitoa mikakati na mipango ya kutatua matatizo na kuwahamasisha watazamaji kubadilika. Studio itakoyorekodi vipindi hivyo pia imetengenezwa katika hali ya ubunifu na kupendezesha kipindi.


3. Mada Zitakazoongelewa

Kutakuwa na mada mbalimbali na mpya ambazo zitaongelewa kila wiki. Mada hizi zitategemea utafiti utakaofanywa na mamombi ya watazamaji ili mradi tu liwe ni tatizo ambalo linaigusa jamii au watu wengi. Mfano wa mada hizi ni pamoja na biashara; mahusiano; kazi na ajira; kilimo; Wanawake, rushwa; madawa ya kulevya nk.

4. Mpangilio wa Kipindi:

a) Kuwakilisha mada husika na kuitambulisha huku takwimu zikitolewa toka chanzo cha kuaminika.
b) Kulielezea tatizo husika katika uhalisia wake na kuwafanya watazamaji waone ukubwa wa tatizo
c) Kulijadili tatizo na kulichambua kwa kina huku maswali yakijibiwa
d) Kuwakilisha majibu na ufumbuzi wa tatizo
e) Kuhamasisha watazamaji wazinduke/waamke, kubadilika na kuchukua hatua ya kutatua tatizo kama lilivyo ainishwa.
f) Kipindi kitaendeshwa kwa mtindo wa majadiliano yenye hisia kali na hivyo kupeleka hisia kwa watazamaji pia.


5. Walengwa wa Kipindi:

a) Vijana
b) Wanafunzi
c) Wafanyabiashra
d) Wanandoa
e) Na wananchi wote kwa ujumla.


6. Urushaji wa Kipindi na Upatikanaji katika DVD

a) Kipindi kitakuwa kinarekodiwa na kurushwa katika Luninga siku ya Jumapili saa 3 hadi saa nne usiku kwa muda wa saa moja. TBC1 na kurudiwa Jumatano Mchana
b) Baadhi ya vipindi vitavyoonekano kama ni mafunzo muhimu na adimu kwa watu na jamii vitarekodiwa katika DVD na kusambazwa na kuuzwa kwa bei nafuu kwa walengwa.


Karibuni sana.
 
Back
Top Bottom