Tv stations zetu na kuripoti kwao matokeo ya mechi

tanga kwetu

JF-Expert Member
May 12, 2010
2,194
1,434
...huwa nafuatilia sana taarifa za habari za hapa bongo na vituo vya nje kama CNN, BBC na SANBC. Vituo vya nje vinapotangaza matokeo ya mechi fulani ya soka huwa lazima virushe clip za mabao. Mathalani kama mechi imeisha 3-2, lazima utaonyeshwa mabao yote matano yalivyopatikana. Lakini TV zetu za Bongo mara nyingi sana (almost 95%) hawaonyeshi mabao hata kama mechi ilikuwa na mabao kadhaa. Afadhali kama hawana record ya hiyo mechi lakini wanakuwa nayo na mbaya zaidi wanaonyesha vipande vya matukio mengine katika hiyo mechi kama vile chenga, kona na move za ajabuajabu. Inanikera sana! Naomba wabadilike katika hili
 
Unajua hawa jamaa hasa TBC naona ITV naona labda hawana ufundi ni maneno tu? Wanatakiwa watuonyeshe scenes ili mtazamaji apate kuappreciate. Naona hawajui matumizi ya Technology zaidi ni longolongo.
 
Huwa hawana muda wa kijifunza kwa wenzao kazi yao kubwa ni kujiona masupastaa na kupoteza muda kukaa vijiweni na kupiga mizinga ka vile hawana mwisho wa mwezi.
esp. radio moja! kuna yule mtaalam wa kunyoa kibwenzi huwa anaboa sana huku akijitamba mkongwe,ati jezi no 9
 
Umesema kweli nimekupata anaboa sana mno. Eti mechi imechezwa Uwanja wa Taifa lakini mpaka saa 2 taarifa hawana matokeo simu/hand set ni za nini sasa. Upuuzi mtupu!
 
kwa ujumla watanzania tumelala sana, tunapenda starehe ila kuumiza vichwa hatutaki kabisa. Ikitokea mgeni wa nchi za nje akamiliki vitu vyetu tunaanza kulalamika, ngoja wachina wachukue kila sekta maana wao hadi kupiga debe wamo.
 
Hilo linachangiwa sana na tatizo la kamera moja uwanjani...Lakini wakati mwingine ni la uchovu wa taaluma wa cameraman na mwandishi wake
 
Tatizo ni namna wanavyorusha au kurekodi matukio ya kimichezo. Kwa mfano,kwny soka iwe ITV au TBC1 unakuta wanatumia kamera 2 au 3 tu. Ivyo hata kiwango cha urushaji wa matukio kwny mechi husika unakuta duni. Angalau Star TV wanajitaidi kiasi fulani. Pia mafundi wa station za kibongo hawako creative,na wengi wao hawajasomea izo kazi zaidi ya kuzifanya kwa mazoea.
 
...kwa mfano mechi za Senior TUSKER Chalenge Cup 2010 mbona wanarusha vizuri hadi slow motion safi na inaonekana wana camera nyingi uwanjani na still kwenye taarifa ya habari wahaonyeshi clip za amgoli. Mfano Kilimanjaro Stars Vs Uganda jana, nilitegemea wangeonyesha hata vile Kaseja anaokoa Penati lakini ni blaa blaa tu!!!
 
Kuna haja akina Tido Mhando na Joyce Mhavile wazinduliwe wajue majukumu yao, mojawapo ni kuwapatia elimu ya kutosha hao akina Kitenge na wengine ili sisi watazamaji tufaidi matunda ya uhuru
 
replay ya matukio muhimu ni shida kuonekana, Mtangazaji hajui hata off-side anasema foul, ikitokea goli limefungwa wakati kamera imeelekea kwa washabiki basi hamtaliona tena hilo goli.
 
...kwa mfano mechi za Senior TUSKER Chalenge Cup 2010 mbona wanarusha vizuri hadi slow motion safi na inaonekana wana camera nyingi uwanjani na still kwenye taarifa ya habari wahaonyeshi clip za amgoli. Mfano Kilimanjaro Stars Vs Uganda jana, nilitegemea wangeonyesha hata vile Kaseja anaokoa Penati lakini ni blaa blaa tu!!!

TBC walionyesha, they are getting better; lakini ITV nafikiri wana matatizo makubwa huwezi kuona goli kwenye taarifa hata kama zilipigwa kumi
 
Tatizo ni namna wanavyorusha au kurekodi matukio ya kimichezo. Kwa mfano,kwny soka iwe ITV au TBC1 unakuta wanatumia kamera 2 au 3 tu. Ivyo hata kiwango cha urushaji wa matukio kwny mechi husika unakuta duni. Angalau Star TV wanajitaidi kiasi fulani. Pia mafundi wa station za kibongo hawako creative,na wengi wao hawajasomea izo kazi zaidi ya kuzifanya kwa mazoea.

Umelonga nakubali wanajifanya wanajua lakini hawana kitu. TV over 20 years bado camera moja maana yake nini?? jamani tuamke
 
...kwa mfano mechi za Senior TUSKER Chalenge Cup 2010 mbona wanarusha vizuri hadi slow motion safi na inaonekana wana camera nyingi uwanjani na still kwenye taarifa ya habari wahaonyeshi clip za amgoli. Mfano Kilimanjaro Stars Vs Uganda jana, nilitegemea wangeonyesha hata vile Kaseja anaokoa Penati lakini ni blaa blaa tu!!!

TBC hawana ubavu wa kuonesha game kwa utaalamu kama waliounesha CECAFA TUSKER CHALLENGE japo kiuhalisia ameonekana kuleta matumaini ya mbeleni....Walikuwa wakionesha kwa kushirikiana na wataalamu wa Super Sport ndo maana ukaona hata jana mara ya mwisho walikuwa wakijitahidi kutomuonesha mangazaji wa Super Sport aliekuwa akiripoti matukio ya ugawaji zawadi bila mafanikio..........Inabidi wabadilike kwa kuwaajiri wataalamu wenye uwezo(toka nje) ama kuwapeleka wafanyakazi wake wanaopiga na kuchanganya picha nje ya nchi(hata South Africa) wakajifunze namna ya kupiga na kuchanganya picha kwa ajili ya matangazo ya moja kwa moja ikiwa ni pamoja na hiyo REPLAY
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom