TV Program Alert: "Maonyesho Sekta ya Fedha" Watanzania Hawakopi Kwanye Mabenki!.

bank sio rafiki wa masiki hata kidogo!

Kuna mifumuko ya mabenki ya kinyonya zaidi ya 100 tanzania.ni dalili hii industry inawalipa sana kwa style hizo.sera za mikopo ya mabenki na masharti sio rafiki wa wajasiriamali wadogowadogo ambao ndio chimbuko kubwa la povert eradication and econonomic development ya nchi changa kama tanzania.hasa kwakua tanzania haina wigo mpana wa kumeza ajira za product zote za wanavyuo wanao hitimu (universities/training college/veta) ni wazi kujiaajiri is inevitable ili kujikomboa.hata asili ya mediam anad large scale enterprises ni ujasiriamali mdogo(small enterprises) ila serikali hii ya sisiemu haina nia ya dhati kurekebisha mifumo ya fedha ili kuziwezesha banki kutengeneza sera bora za mikopo kw wajasiriamali wadogo.imagine dhamana wanazozitaka mabenki ni nyumba zenye title, je ni % ya nyumba za tanzania hazijapimwa? Udogo wa mishara kiduchu ya watz wengi hamuwezeshi mtanzania kupata mikopo ya kujenga nyumba za kisasa
word mkuu
 
UP DATE 5

Program 6: Leo 13/10/2012
Kituo: TBC-1
Duration: 30 minutes
Broadcast Time: Saa 11:30 Jioni.
Contents:
TASAF
 
UP DATE 6

Program 7: Leo 13/10/2012
Kituo: TBC-1
Duration: 30 minutes
Broadcast Time: Saa 1:30 Usiku.
Contents:
MKURABITA.
 
Kwa nini ifike mahali watanzania tuambiwe kuwa ni watu wa ajabu sana kwa sababu tunajenga nyumba na kununua magari bila kukopa? Kwani maisha bila kukopa hayawezekani kabisa? Yaani mtanzania bila kukopa hawezi kufanya jambo lolote la maendeleo? Mimi sikubaliani na huu mtazamo hata kidogo. Kuna mbinu/kazi nyingi watu wanatumia kujiingizia kipato halali na hatimaye kujenga nyumba na hata kununua magari. Sio lazima wakope.

Kuna usemi kwamba "fedha siyo msingi wa maendeleo". Bali kazi ndio msingi wa maendeleo. Hii inashiria kwamba katika nchi yenye rasilimali nyingi kama tanzania, kufanya kazi kwa kutumia juhudi na maarifa ndio jambo la kwanza kabisa na fedha ni matokeo ya kufanya kazi kwa juhudi na maarifa. Kwa maana hiyo basi Mtaji mkubwa wa binadamu au mtanzania yeyote sio hela bali ni akili/maarifa na juhudi zake na jinsi anavyovitumia katika kupamabana na maisha na kujiongezea kipato/fedha halali ikiwa ni pamoja na kuweka akiba au kutumia vizuri kile kidogo anachopata kila siku.

Kuna watu wanafanya kazi za mikono au kazi za kawaida tu lakini wakipata hela wanakuwa na malengo mazuri na wanatumia hela yao kwenye mambo yenye manufaa kama kujenga nyumba na hatimaye wanafikia malengo yao. Hii ina maana hata kama ukikopa kama huna mipango mizuri, huna nidhamu ktk kutumia hela, mkopo hautakuletea maendeleo hata siku moja.

Ni kweli mikopo inachangia kuleta maendeleo kwa baadhi ya watu lakini kwa watanzania walio wengi mikopo imekuwa msiba mkubwa, na chanzo cha umasikini wa kutupwa. Kuna baadhi ya watu wanakopa kwenye mabenk lakini kwa bahati mbaya wanashindwa kulipa mikopo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kukosa maarifa jinsi ya kutumia mkopo kwa faida. Kinachowapata ni kunyang'anywa nyumba, viwanja au kitu chochote cha thamani walichokuwa nacho na kuwaacha katika hali mbaya kuliko hali ya awali.

Lakini pia lazima tujue kuwa malengo ya mabenki yote duniani si kukopesha hela, kusaidia watu au kunufaisha watu, bali lengo la benk ni kufanya biashara yaani kuzalisha faida kutoka kwa wateja wao ndio maana hakuna benki itakukopesha elfu 50 halafu ulipe elfu 50. Badala yake utakopa elf 50 utalipa elf 80 na kuendelea.

Ushauri wangu.
Pamoja na kuandaa kipindi kizuri kwenye Luninga kuonyesha shughuli mbalimbali za mabenk hapa tanzania na suala zima la kukopa na mikopo na kuhamasiha watu wakakope, ni vema mkalitupia macho suala la; Kwanza, kuwaelisha watanzania jinsi ya kujituma kufanya kazi yoyote iliyo halali kwa juhudi na maarifa. Pili, kuwaeliesha jinsi ya kutumia vizuri vipato vyao walivyo navyo. tatu, waelimishwe jinsi ya kujiwekea malengo na namna ya kuyafikia malengo. Nne, muwaelimishe jinsi ya kutumia mkopo vizuri ili kufanikisha kile kinachowapelekea kwenda benki kukopa. Bila hivyo naona kama mtakuwa mtangaza tu biashara ya mabenk, ili watu waende kukopa halafu waishie kupata hasara huku benki zikiendelea kuneemeka kwa riba kubwa na kupora nyumba nk kwa watz wanaoshindwa kulipa madeni

ni mtazamo wangu tu
 
Yeah Mkuu umenena ukweli mtupu
Mabenki mengi yenye riba yapo kibiashara zaidi na lengo si kusaidia bali nikufilisi Watz wenye nyumba na aset zao
Ndio maana Watanzania swala la kukopa kwenye Mabenki hatuna habari na tunaogopa kama ukoma.
 
Back
Top Bottom