Tv na magazeti ya chadema katika ukombozi wa kweli wa taifa letu....!

MAMA B

Member
Nov 1, 2010
29
0
Naomba wasom wetu ndani ya chama wafikilie kuweka tv ya chadema ambayo inaweza ikawa inamilikiwa na chama moja kwa moja au watu binafsi kuficha identity......tunapata shida sisi wadau na hasa inapotokea issue ambayo ni sensitive........tv zilizopo hatuna imani nazo na habari wanazotoa kama ilivyo kwa tume yetu......mkiweza muongeze magazeti na nna uhakika mtapata faida itakayowasaidia kwenye kuendesha chama kuliko kukaa na kusubiri ruzuku za hao wajinga.......tuangalia vyanzo vya mapato katika kuimarisha chama pia......na soko lipo linawasubili.......tunaangalia itv,tbc,na star tv kwa vile hatuna option wakuu.......
:angry:
 
ni wazo zuri, wadau lifanyiwe kazi, hivi project kama ya tv station, inaweza kugharimu kiasi gani hadi ikamilike?
 
Katika hali kipindi hiki ambacho chama kinahitaji kupambana kufa na kupona kuleta mabadiliko, kuwa na TV, RADIO, na MAGEZETI KADHAA ni sio muhimu tu, ila ni lazima. Viongozi wetu nawashauri mjitahidi ikiwezekana vitu hivi viwe tayari kabla ya uchaguzi ujao. Hawawezi kuzuia, ni haki ya watanzania kufanya biashara. Tenawachangiaji tupo, katika kipindi hiki cha mwamko huu, ukiitisha harambee kwa ajili ya mradi huo utashangaa mwitikio utakavyokuwa mkubwa.

Vilevile ni muhimu kutokutegemea ruzuku ya serikali. Wapigania uhuru (ukombozi) daima hujitolea kwa mali zao na hata uhai wao. Miradi hii itakiimarisha chama kisiwe tegemezi.
 
Wazo zuri sana na nakushukuru kwa kuwa umeniwahi,baada ya kusoma taarifa kwenye mwanahalisi kuwa kuna mpango wa kuhakikisha mwanahalisi,mwananchi na Tanzania daima hazisomwi kwenye radio na tv zinazoonekana nchi nzima(star&itv) nilipata wasiwasi kuwa watu wengi watakosa vichwa vya habari na uchambuzi kwa ufipi.CHADEMA NA WANACHAMA WAKE WAPENDA MAENDELEO NI WAKATI WA KUWA NA TV NA RADIO,Ili habari za uhakika ziwafikie wote.Wanachama ikiwezekana tuchangie.
 
Chadema ianzishe MEDIA FUND(wakereketwa wachangishane-TV station ya kukava nchi nzima as Turnkey project kwa sasa ni dola 1.5 million-kwa mkoa mmoja ni Dola 150,000) waombe leseni TCRA,mbona Redio Uhuru ipo Hewani ikitangaza toka Lumbumba street,karibu na msikiti wa manyema.Hilo linawezekana unaonaje?
 
Back
Top Bottom