TV fake na original nazitofautishaje?

Sexer

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
8,215
7,906
wakuu, nahitaji kununua tv LG smart 43' naomba mniokoe kabla sijala hasara make nategemea itanitoboa mkwanja mrefu. je nitumie maujanja gani nisibambikwe tv fake?
 
Fake utaona rainfred masako anatangaza habari mubashara.....mwambie muuzaji ajupe warrant na risiti mkuu
 
brand pekee ninayoikubali kwa sasa ni lg na sony kwa kutoa tv original, cha msingi mkuu jua specifications za tv unayoihitaji. kweli hadi sasa bei za tv hasa hizi flat bado zipo juu sana kwa hiyo umakini mkubwa sana unahitajika ikiwa ni pamoja na kuwa na mtaalam wakati ukifanya manunuzi vinginevyo utapigwa tu
 
Kila brand mi navojua kuna fake yake.Kitu cha msingi kanunue kwa authorized dealer na pia uende maybe na mtu mwenye experience na mambo haya..
 
Kitu Kingine Bei Unaweza Uka Google na Kupata Bei halisi ya Bithaa

Unaweza Kukuta TV ina Inch 43 kwa Hiyo Brand unakuta Bei yake ina range $450-$500 halafu Tanzania Mtu anakwambia anaiuza Sh.750,000/= shtuka!
 
img12[1].gif
 
ngumu sana kukuta tv fake ila kuchukua tahadhari ni muhimu, hakikisha unanunua duka linaloeleweka na unapata warranty ili likitokea la kutokea uwarudishie, hizi ni baadhi ya tip ya tv ya lg ya inch 43 ipoje.

1. itakuwa na operating system ya web os ambayo inaonekana kama hivi,

webos-tv-feature-640x417.jpg

unless kampuni nyingine itumie android na launcher hio huwezi kuta tv ya kichina inatumia web os, hio ni ya lg tu.

2. remote yake ni kama mouse inayoelea, unaipoisogeza mbele na nyuma, kulia na kushoto ndio kile kimshale kwenye tv kinavyosogea

3. inatumia kioo cha led au oled, sifa ya hivi vioo ni kwamba vinaonyesha rangi nyeusi ambayo ni nyeusi, tofauti na lcd au vioo vibovu vya kichina ambavyo nyeusi inakuwa kama kijivu,

OLED-vs-LED-TV-Contrast.png

4. ni vyema kama una smartphone ya kisasa ukaenda nayo, smart tv ya LG itakuwa na Intel widi au Miracast ambazo unaweza ukaangalia vitu vya simu yako kwenye tv kupitia wifi.
 
Ufafanuzi wako kwa kweli huwa unaeleweka vizuri mno ubarikiwe sana mkuu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom