TV Chaneli za Kulipia

Rover

Member
Apr 8, 2009
10
0
Wadau,

Wa Tanzania wengi tunaumia sana na hizi TV za kulipia,Mwanzo kulikua na TV Burudani ofisi zake ziliku Maarifa House Mtaa wa Ohio, Wametokomea na hela za watu wametuachia ving'amuzi vyao.

Ikaja GTV wao walikua pale Namanga watanzania wengi walinunua Ving'amuzi na Ma-dish nao wametokomea.

Sasa hivi kuna Easy TV na Startimes Digital TV. Sasa je tutaliwa tena? kwa kisingizio cha World Cup south Africa?

Serekali kupitia wizara husika haina jinsi ya kuzuia hili.

Nawasilisha.
 
:becky::becky::becky::becky: Unaulizia kata kisimani!

Subirini tu :target:

Huko mikoani watu wanauziwa ving'amuzi wanaaambiwa mitambo itawashwa kabla tu ya world cup!

Bongo hii bana!

marehemu mama mdogo alishawahi kuniambia Bongo ni sehemu unayoweza ukachota maji baharini ukayaweka kwenye chupa na ukawauzia watu! Nilicheka nikidhani utani lakini nilivyokua nathibitisha maneno yake!
 
Tumerogwa na aliyeturoga kakufa na alikua yatima patamu hapo hakuna reversal :yuck:
 
mimi ni muhanga wa gtv, kwakweli umenena kweli wanatumia kombe la dunia kama chambo baada ya hapo huoni mtu
 
GTV wakumanina sana, walilamba subscriptions zangu za mwaka wakatoweka na wala hatutangaziwa wamefilisika tukadai vijisenti vyetu.. au mtu akifilisika bongo msajili hatangazi kuwa wadeni wake wajitokeze... je kuna utaratibu wa kuwaprotect wananchi na hizi pre-paid services ambazo huletwa ki majini majini?
 
Anayewapa leseni ni nani? Kosa linaanzia hapo kwani wanatakiwa wathibitishe uwezo wa kumaintain biashara ili wasifilisike. Kama hawana hela ya kutosha wasipewe leseni kwani wataishia kutuliza wananchi haswa wale wa vijijini. Serikali wanahitaji kuliangalia hili swala upya na walifanyie kazi.
 
kwani si ndiyo hayo hayo ya shirika la reli na wahindi lesen mbele yakivurugika kuvunja mkataba shida.
 
Kwani kama wasipopata wateja si watafunga tu ofisi? Na sisi tumezidi kupenda dezo jamani achaneni nao!!!!!!! hakuna cha usajili wala nini wote hamnazo tu!!!!!
 
Usitegemee serikali kuingilia kati, wakati Startimes Digital TV ni mradi wake

Startimes Digital Tv ni Richmond nyingine. Watu wameuziwa mbuzi kwenye gunia. Remote za decorder zake nyingi ni mbovu (as usual substandard Chinese technology and ingenuity). Halafu hiyo TBC2 haimo kwa hiyo world cup ndio sorry. Kama una DSTv yako endelea nayo uone World Cup matches bana.
 
Ndugu zangu nchi yetu haiprotect walaji hata kidogo. Ni viini macho tu. Si mnaona Ewura na bei zake za kikomo? Ni w....zi mtupu. Kama umeingia humo katika TV za kulipia ujue ni wewe mwenyewe. Hakuna mtu wa kukutetea unapoliwa. La muhimu tuangalie historia tusiendelee kudanganyika na hawa jamaa wanaochance. Mimi naona DSTV ndo walao wapo sokoni kudumu japo bei zao usiseme. Lakini starehe GHARAMA.:angry:
 
Wanyonge mlie tu!!!! Wakulima na wale choka mbaya kazi kwenu. Utaweza kununua kaDecoder ka Startimes kwa 79,000/= weye au kaantena kasiposhika unauziwa nyingine kwa 20,000 ile ya nje? weye nakuuliza muuza kashata mpenda michezo utaweza???? Kalagabaho na Ubwezi wako ihihihihihihhiiiiiii..... Bongo tambarareeeeeeee :pound:
 
Back
Top Bottom