Hivi sasa karibu kila chombo cha habari yaani magazeti,radio,television,mitandao ya kijamii n.k inazungumzia malumbano ya kisiasa ama baina ya vyama au makundi ya urais 2015 n.k kila kukicha vichwa vya habari ni malumbano tu.jamani hebu tubadilike.turipoti mambo ya maendeleo,kuhamasisha wananchi kushiriki katika mambo mbalimbali yanayohusu mustakbali wao na ya watoto wao,kutoa tahadhari ili kuepukana na magonjwa hatari kama ukimwi,malaria,kutoharibu mazingira n.k. Kama mambo ya kushika dola basi tusuburi 2015.nchi inateketea.kwa kutambua hali hii ndiyo maana hata majirani zetu wanatumia mwanya huu kutaka kutuangamiza.mfano mgogoro wa mpaka na malawi.wao wamegundua kuwa nchi yetu ni malumbano na kukashifiana tu.naomba tubadilike.