Tuzungumzie kidogo swala la mipaka ya TANGANYIKA NA ZANZIBAR

MARCKO

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
2,258
274
Kutokana na rasimu ya Katiba Mpya, tutakua na serikali 3 . Sasa tusaidiane kidogo kifikra
"""""""""""""
NINACHOFAHAMU:
"""""""""""""
Ukisema NCHI, nilazima kuwepo na Watu, serikali na Ardhi (Yenye mipaka)
sasa kuhusu Tanzania bara na Tanzania Zanzibar itakuaje??????????
++think in capital letters++
 
Suala lako linaonyesha wewe ni mtu wa aina gani kwanza naweza kusema kuwa huijui Historia ya Tanzania kabla haijaitwa jina hili la Tanzania.

Kwa ufupi sana kabisa nitajaribu kukusaidia kama utaweza kuelewa historia ya nchi yako ya Tanzania. Ni kuwa jina hili la Tanzania limeanzisha mara tu baada ya Muungano wa nchi mbili huru. Nchi ya kwanza katika hizo mbili ni Zanzibar na nchi ya pili ilikuwa ni nchi ya Tanganyika. Nchi hizi zote kabla ya huo Muungano zilikuwa na mipaka yake na inajuilikana kimataifa.

Sasa endelea kufanya utafiti kuhusu mada yako.
 
Mipaka itarudi kama ilivokua kabla ya muungano ambapo ZNZ ilikua huru na Tanganyika ilikuwepo
 
Kutokana na rasimu ya Katiba Mpya, tutakua na serikali 3 . Sasa tusaidiane kidogo kifikra
"""""""""""""
NINACHOFAHAMU:
"""""""""""""
Ukisema NCHI, nilazima kuwepo na Watu, serikali na Ardhi (Yenye mipaka)
sasa kuhusu Tanzania bara na Tanzania Zanzibar itakuaje??????????
++think in capital letters++
Kama hujui jibu la hili swali la chekechea, huku JF umekuja kufanya nini?
 
Mpaka upo sehemu ya katikati ya Dar na Unguja. Panaitwa Chumbe. Kwa iliyesafiri toka Dar kwenda Unguja eneo hilo lina mawimbi makubwa sana. Lakini mipaka ya TZ na ZNZ itakuwa chini ya utawala wa serikali ya muungano kwani litakuwa ni suala la ulinzi na usalama ambalo lipo kwenye jamhuri ya muungano!.
 
Aksante mkuu!
Ila naomba uzungumzie kidogo juu ya mkataba wa Harmaton na Helligoland. Maana kuna makubaliano yaliowekwa na Umoja wa mataifa kuhusu Mipaka (lakini kumbuka wakati ule mtu akisema umoja__Uingereza ilikuaa na sauti kubwa mno, hivyo mkataba mingi iliipendelea hasa baada ya vita vya pili vya dunia)
Sasa sikumbuki ni mkataba upi uliozungumzia Sultan kumiliki 10miles kutoka "coastline", na sijui Wazanziba watakua tayari kufuata upi.
AKSANTE
 
Je, gavana wa mwisho wa Tanganyika alipokuwa anasaini kuondoka; na anaruhusu na kuona bendera ya Union Jac ikishushwa , aliishusha bendera hiyo nje ya mipaka ya Tanganyika?

Kama bendera hiyo aliishushia uwanja wa Uhuru (uwanja wa Taifa zamani) je eneo hilo lilikuwa nje ya Tanganyika?

Na je, magavana wa Uingereza waliotawala Tanganyika, waliitawala Tanganyika wakiwa
ikulu iliyokuwa nje ya Tanganyika? Je, walipoaga na kuuiacha Tanganyika huru, ikulu waliyomwachia Mwl. Nyerere (Waziri mkuu wa kwanza wa Tanganyika-1961-62) ilikuwa ndani au nje ya Tanganyika?

HAYO MASWALI UJIJIBU MWENYEWE
 
Yeah. Mjadala mzuri na kijana atayapata majibu humu humu. A point of correction. Naomba mnapojadili zile nchi mbili zilizotengeneza muungano wa Tanzania, muwe mnaitaja Tanganyika. Na sasa inayotakiwa kurejeshwa kwa mujibu wa rasimu hii ya Katiba ni Serikali ya Tanganyika. Msiwe mnasema Tanzania Bara kwakuwa hakuna na hakujawahi kuwa na nchi hapa ulimwenguni iliyoitwa/inayoitwa Tanzania Bara. Hii ni kuwachanganya hata watoto wetu ambao wanaweza wasiijue vema historia ya nchi yao pale wengine watakapodhani kuwa Tanzania ilitokana na muungano wa nchi za Tanzania Bara na Zanzibar. Ndio maana wengine walishawahi kusikika wakisema kuwa nchi ya Tanzania ni muungano wa nchi mbili za Zimbabwe na Pemba. Unaona sasa! Itajeni Tanganyika. Kwani ilikukoseeni nini hata kuanza kuibatiza majina yasiyo yake? Inaitwa JAMHURI YA TANGANYIKA, ndiyo haswaaaa inayopaswa kurejea.
 
Mpaka upo sehemu ya katikati ya Dar na Unguja. Panaitwa Chumbe. Kwa iliyesafiri toka Dar kwenda Unguja eneo hilo lina mawimbi makubwa sana. Lakini mipaka ya TZ na ZNZ itakuwa chini ya utawala wa serikali ya muungano kwani litakuwa ni suala la ulinzi na usalama ambalo lipo kwenye jamhuri ya muungano!.
We ndo kabisaa unapotosha.
Chumbe ni kisiwa kilicho karibu kabisa na Unguja, sio katikati kama unavyodai.
 
Kutokana na rasimu ya Katiba Mpya, tutakua na serikali 3 . Sasa tusaidiane kidogo kifikra
"""""""""""""
NINACHOFAHAMU:
"""""""""""""
Ukisema NCHI, nilazima kuwepo na Watu, serikali na Ardhi (Yenye mipaka)
sasa kuhusu Tanzania bara na Tanzania Zanzibar itakuaje??????????
++think in capital letters++

Kwani RAMANI ya ZAMANI ilikuwaje?? UKO SAWA KWELI? VISIWA sio NCHI? OH MAN... Tuna KARNE KIBAO za sisi KUENDELEA...
 
Back
Top Bottom