Tuzungumze upya kuhusu Utanganyika na utanzania (Bara) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuzungumze upya kuhusu Utanganyika na utanzania (Bara)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Raia Fulani, Jun 7, 2012.

 1. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Prof Shivji katika kipindi chake cha Katiba ITV kasema hakuna Dola ya Tanganyika. Ni mipaka tu ya wakoloni iliyoifanya hiyo Tanganyika ambayo ilidumu kwa miaka mitatu tu na ndipo ilipozaliwa Tanzania. Hata Mwalimu Nyerere aliwahi kukiri kuwa hajui jina 'Tanganyika' asili yake nini. Wengi tumezaliwa Tanzania. Tanganyika mnaitakia nini?
   
 2. A

  Albimany JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45

  Unaonekana kama una alegi na Tanganyika!.
   
 3. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  siwezi nikasema naitaka ama la maana kiukweli sikuwahi kuwa nayo hiyo Tanganyika. Ila hayo hapo juu si maneno yangu bali ni ya Shivji. Anauliza wabara wanaitaka Tanganyika ili iweje?
   
 4. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Katiba ya Jamhuri ya Muungano inasema katika ibara ya 2 kuwa Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar...

  Ibara ya 4 (2) inasema, Vyombo vyenye mamlaka ya utendaji vitakuwa ni serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar...

  Hapa hatuoni tena nafasi ya Tanzania Bara wala Tanganyika, bali ni kama ilivyoandikwa hapo juu. Iko wapi nafasi ya Tanzania Bara katika Muungano?
   
 5. Jembe Ulaya

  Jembe Ulaya JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2012
  Joined: Oct 27, 2008
  Messages: 456
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tanganyika ni jina lililobuniwa na mkoloni. Wana historia wanadai lina maana ya Nyika za Tanga. Lilikuwa jina lenye dharau juu ya ardhi yetu. Tulirithishwa na wakoloni kama tulivyorithishwa mipaka yetu. Tanzania ni jina tulilobuni sisi wenyewe baada ya uhuru. Kama kuna wanaotaka kujitoa kwenye Jamhuri ya Muungano wa Tanzania basi wajitoe na sisi tubaki na jina letu Jamhuri ya Tanzania.
   
 6. Chilli

  Chilli JF-Expert Member

  #6
  Jun 7, 2012
  Joined: Jul 17, 2011
  Messages: 1,638
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Ni bora kubaki na hilo jina 'la kikoloni' kuliko kuwa na jina lenye element zozote za Upemba. Tukibaki na jina lenye element za kipemba wanaweza kutuambukiza hata roho ya kibaguzi.
  Njia nzuri ya kumsahau mke mloachana ni pamoja na kuondoa kila kitu ambacho kinaweza mrudisha mawazoni mwako. Acheni wapemba waende na Zenji yao na sisi tubaki na Tanganyika yetu bana.
   
 7. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #7
  Jun 7, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Hapa ndio mahali nashindwa kuwaelewd wenzangu. Mimi ni Mtanzania na ni mzaliwa wa Tanganyika. Tusiwe wajinga wa kuikataa hata historia. Tar 9 dec, tunakumbuka uhuru wa Tanganyika, na sio Tanzania bara. Huo ndio ukweli. Tanganyika ilikuwepo na ilikuwa dola iliyokuwa inajitosheleza. Baada ya muungano ikaundwa Tanzania. Leo tukijifanya eti tumezaliwa tanzania na ku act as if Tanganyika haikuwepo ni upuuzi na ufinyu wa fikra. Tunatakiwa tujivunie nchi yetu!
   
 8. Mtoto wa nzi

  Mtoto wa nzi JF-Expert Member

  #8
  Jun 7, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 3,873
  Likes Received: 2,904
  Trophy Points: 280
  kipindi hili koloni lipo chini ya uangalizi wa uingereza baada ya vita ya kwanza ya dunia, ndipo jina tanganyika likazaliwa ...., ilikua ni "tanganyika protecorate" kwa kuchukua jina la lake tanganyika..., ndivyo navyofahamu kwa ufupi mwanzo wa jina tanganyika, kama tanganyika haikuwepo iliyopata uhuru mwaka desemba 9,1961 ilikua inaitwaje?
   
 9. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #9
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  mkuu kuna wadau hapo juu wanasema kuwa Tanganyika ni ukoloni. Wapo wanaosema Tanzania Bara ina element za visiwani. Ila pia katika katiba ya Jamhuri sioni popote TB ilipopewa mamlaka ya kiutendaji badala yake ni Jamhuri ya Muungano na Tanzania Zanzibar
   
 10. m

  mzaire JF-Expert Member

  #10
  Jun 7, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 11. Asnam

  Asnam JF-Expert Member

  #11
  Jun 7, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 4,268
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Idumu Tanganyika we unaesema hilo jina ni la ukoloni kwani nchi zingine majina yao wameyatoa wapi ni huo huo ukoloni isipokuwa kwa nchi ambazo hazikutawaliwa.Tanganyika iliungana na Zanzibar ndipo ikazaliwa Tanzania,rudi darasani kasome
   
 12. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #12
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Inabidi tujiulize mtu kama Prof Shivji anakwepa kuweka bayana Utanganyika na Muungano wakati anasema tukitaka mjadala wa Katiba mpya uwe huru na wa haki basi pasiwepo jambo lililofichika, je sisi wa miaka ya 70's tuzungumze nini kuhusu Muungano?
   
 13. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #13
  Jun 7, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  raia fulani,
  namalizia kucollect data zangu halafu ntaziweka hp jf nikujibu.
   
 14. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #14
  Jun 7, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  asnam,
  kama wachangiaji wengine wanasema tanganyika ni jina la kikoloni. je nigeria, kenya, uganda etc nani alitoa majina hayo?
   
 15. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #15
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Itakuwa jambo la heri mkuu maana utatufumbua wengi
   
 16. k

  kombo1 Member

  #16
  Jun 8, 2012
  Joined: May 27, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sisi kutoka visiwani hatujali mkibakiwa na jina la nchi yenu ikiitwa Tanzania au Tanganyika, kitu tunachokitaka mtuachie turudishe utaifa wetu huko umoja wa mataifa haraka iwezekanavyo na jina la nchi yetu halina matatizo ni Zanzibar. Tafadhali watanganyika na wakereketwa wa CCM tuachane kwa njia ya usalama na tuishi kama majirani wema
   
 17. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #17
  Jun 8, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  ukweli ni kwamba kwa gharama yoyote ile inaonekana Muungano hauwezi kuvunjika. Ukivunjika ni dhahiri Zanzibar nayo itavunjika. Wale ni wachache sana na wadhaifu kila pande. Mataifa ya Magharibi yatautumia udhaifu uliopo visiwani kuweka vituo vyao vya kimaslahi katika ukanda huo. Wakati huohuo mwarabu nae angependa kuona anajaribu kurejesha historia.

  Ishu sasa hapa ni jinsi gani ya kuridisha hadhi ya Bara maana katika katiba ya Muungano, Bara haipo. Zipo serikali mbili: ya Muungano na ya Zanzibar!
   
Loading...