Tuzungumze kuhusu Vyama vya Ushirika na Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania

Momburideo

New Member
Jul 4, 2021
4
1
Tuzungumze kuhusu ushirika na kinachoendelea juu ya mabadiliko ya Sheria ya vyama vya ushirika Na. 6 ya mwaka 2013. tuzungumze juu ya Time ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania.

Tuzungumze juu ya umuhimu wa Maafisa ushirika nchini, na je ni kwanini serikali haioni umuhimu wao?

Pia kwanini Tume ya Maendeleo ya Ushirika pia hawajawapa umuhimu Maafisa ushirika wa wilaya?

Pia nini kifanyike?
 
Fatma kifanyike Nini ili Ushirika uweze kurudi? Pia Kama umepata fursa ya kuipitia hiyo Sheria ya vyama vya Ushirika pamoja na muundo wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kipi kiboreshwe?
Lengo la sheria hii ni nini?Lengo la serikali ni kutaka kupata pesa kutoka kwenye hivi vyama. I wish kama lengo la serikali lingekuwa ni kuboresha ushirika obviously hata sheria ingelenga kuimarisha. Serikali yetu inapenda sana kuzima moto. Serikali yetu haina focus. Haijui inataka nini. Mimi ningeshauri, ili kuwa na sheria inayo-promote, ni vizuri tukaanza kutenganisha key segments katika ushirika. Ushirika ni mpana. Tuwe na maeneo kama manne hivi makubwa ya ushirika (aina) halafu kila moja tuitengenezee sheria yake. Huwezi kuwa na sheria moja inayowa-guide watoto wa miaka 0 hadi 18. Never. Ushirika ni mpana sana. Ila serikali ikienda na hilo lisheria kama lilivyo, watakwama tu. Narudia tena, lengo la sheria isiwe kukamua vyama pesa. Lengo liwe ni kuchochea financial deepening and inclusion kwa wananchi wake.
 
Unadhani vyama vya Ushirika vikigawanywa katika makundi na yakatungiwa Sheria yake Ushirika utasimama?Je pia Kuna haja ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika kuwepo au irudi Kuwa idara chini ya wizara ya kilimo?
 
Katika soko huria sioni hii kitu kama inaweza kufanya kazi.
Pia ushirika ni watu waliojiunga sio watu wakiolazimishwa kuwemo.
Ushirika uliopo si enclusive kwahiyo wakulima wanalazimishwa kuwemo.
Fikiria mkulima amelima kwa gharama zake halafu unampangia auze kwa mfumo gani. Je unajua wakati analima alipata wapi mtaji wa kulimia?

Hizi sheria hazijazingatia hali halisi ya mkulima, ushirika sio ujamaa, na kama ziundwa kipindi cha Ujamaa ambao umeshindwa kufanya kazi zifumuliwe upya zifanywe kuzingani hali ya mkulima mdogo pia.

Kila sehemu Ushirika haujapata kuungwa mkono na walio wengi si kwa sababu ni mbaya lakini ni kwa sababu unanyang'anya power ya mkulima juu ya mazao yake.
Mfano ikiwa mkulima amepata Pamba yake kidogo na anahitaji kupeleka mtoto wake shule kwa hela hiyo hana asses nayo kwa haraka, atalazimika asubiri mnunuzi au mnada kupitia ushirika ambaye hatampa pesa siku hiyo, atalazimika kufungua akaunti na kukatwa riba ya benki

Maafisa ushirika watoe elimu kwa wakulima ili wauelewe na kuupokea sasa hivi ni mfumo unaoshuka toka juu kuja chini kwa utekelezaji, wakulima ambao ndio wahusika hawajui kinachoendelea.

Soko ndio jambo nyeti. Ushirika wajiulize lengo la kuunganisha watu ni nini?
Je wanaibiwa na makampuni kwa kukosa uelewa wa masoko?
Je wanapata jukwaa ambalo wanaweza kukuza uwezo wa kuzalisha?
Yaani kwanini mkulima awe na ushirika?
Majibu wajibu yakiwa na manufaa chanya, sio chanya kwa serkali, la sivyo ushirika utabaki wa serkali sio wananchi
 
Unadhani vyama vya Ushirika vikigawanywa katika makundi na yakatungiwa Sheria yake Ushirika utasimama?Je pia Kuna haja ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika kuwepo au irudi Kuwa idara chini ya wizara ya kilimo?
Utaanza kusimama. Tume ni muhimu hasa ikienda zaidi mikoani na ikijikita kwa kila aina ya ushirika. Yaani iwe na window za kila aina ya ushirika. Ni makosa kuweka ushirika chini ya wizara ya kilimo kwa sababu ushirika ni zaidi ya kilimo. Ndiyo maana nilisema serikali huwa haijui inachotaka na haina focus. Inapenda kuzima moto.
 
Umetoa mawazo mazuri Sana kuhusu ushirika,pia unadhani Tume isipoweka Ofisi au kuhusisha upya muundo wake kwa kuwatambua Maafisa Ushirika wa wilaya (DCO/MCO/TCO) pamoja na kuwatambua Maafisa Ushirika waliopo chini yao unadhani usimamizi utakuwa timilifu?Je kuwepo kwa usimamizi ngazi ya Mkoa inatosha?
 
Umetoa mawazo mazuri Sana kuhusu ushirika,pia unadhani Tume isipoweka Ofisi au kuhusisha upya muundo wake kwa kuwatambua Maafisa Ushirika wa wilaya (DCO/MCO/TCO) pamoja na kuwatambua Maafisa Ushirika waliopo chini yao unadhani usimamizi utakuwa timilifu?Je kuwepo kwa usimamizi ngazi ya Mkoa inatosha?
Huitaji watu wengi kusimamia ushirika. Kumbuka hawa watakuwa wana-regulate na kuzipromote "hizi organizations". Unahitaji watu wanaoelewa maana ya ushirika lakini pia wanaofahamu biashara. Siyo wanaofahamu kilimo maana ushirika ni mpana kuliko tunavyodhani. These officers wanatakiwa kuishia mikoani tu na wawekewe malengo. Wawe promoters na siyo wakamuaji na wasumbufu. Lakini kubwa zaidi watekeleze sheria inayotofautisha aina za ushirika. Wawe integrated na ofisi ya RAS, DED, DAS, na afisa biashara, mipango wa mikoa na wilaya bila kusahau bank zao na TRA. Swala la kulea linahitaji players wote muhimu ndani na nje ya serikali. Kuajiri watu ambao hawana kazi ni misuse of resources. Shida ni kwamba, tunaajiri watu huko chini tukiwaita wanaushirika wakati tukiwa na lengo kichwani la wanakilimo!. Ushirika ni biashara. Scientific business approaches must guide it.
 
Umeweza kuzungumza mengi mazuri,Ila kiukweli bado Kuna umuhimu mkubwa wa Hawa Maafisa Ushirika,hususani katika kutoa elimu na kufanya usimamizi juu ya uendeshwaji kwenye hivi vyama vya Ushirika vilivyopo katika halmashauri zetu nchini, mwisho wa siku wakiondolewa kutapelekea vyama bingo kushindwa kupata huduma kwa uharaka
 
Umeweza kuzungumza mengi mazuri,Ila kiukweli bado Kuna umuhimu mkubwa wa Hawa Maafisa Ushirika,hususani katika kutoa elimu na kufanya usimamizi juu ya uendeshwaji kwenye hivi vyama vya Ushirika vilivyopo katika halmashauri zetu nchini, mwisho wa siku wakiondolewa kutapelekea vyama bingo kushindwa kupata huduma kwa uharaka
Ni kweli ila tukivifanya hivi vyama kuwa "enterprises" hutakuwa na haja ya maafisa wengi. This is because, "biashara" itajiendesha "kibiashara". Tume ibaki na regulatory and promotion roles tu. Shida ya ushirika TZ ni kudhani kuwa siyo biashara. Ushirika is business. Serikali ichochee ushirika ambao umekaa kibiashara. Siku njema.
 
Back
Top Bottom