Mwanamayu
JF-Expert Member
- May 7, 2010
- 11,338
- 6,463
Demokrasia maana yake ni maamuzi yanayogusa maslahi mapana kabisa ya nchi kufanywa na wananchi wenyewe walio wengi bila kujali hali zao isipokuwa watoto na wagonjwa wa akili na wa kufikiri, ingawaje katiba haisemi juu ya wagonjwa wa kufikiri lakini wapo. Kazi ya serikali ya kidemokrasia ni kutekeleza maamuzi ya wananchi bila kutoa ushauri au kuingilia mchakato wa maamuzi au bila kuwachagulia mambo ambayo wao hawayahitaji.
Kuna kesi nyingi zimekuwa zikifunguliwa mahakamani za uchaguzi na chaguzi kurudiwa nyingine kutokana na dosari jinsi uchaguzi ulivyoendeshwa. Hiki ni kiashiria kimojawapo cha kuingilia baadhi ya maamuzi ya wananchi kwa mujibu wa katiba na sheria. Tume ya Taifa ya Uchaguzi ndio inasimamia na kuratibu uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani (ibara za 74 (6) (b) - (d), lakini ipo juu ya sheria na wala haishitakiwi juu ya kazi yake yeyote ile au kuhojiwa na mahakama yeyote ile wakati ushindi wa baadhi ya kesi za uchaguzi ni ushahidi wa nguvu na dhahiri kabisa kuwa kinga hiyo ni batili (angalia ibara ya 74 (12) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania)!!!
Wito kwa wananchi na wabunge kwa ujumla, hili tundu linahitaji kiraka ili sehemu za siri za mwili zisitiriwe.
Kuna kesi nyingi zimekuwa zikifunguliwa mahakamani za uchaguzi na chaguzi kurudiwa nyingine kutokana na dosari jinsi uchaguzi ulivyoendeshwa. Hiki ni kiashiria kimojawapo cha kuingilia baadhi ya maamuzi ya wananchi kwa mujibu wa katiba na sheria. Tume ya Taifa ya Uchaguzi ndio inasimamia na kuratibu uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani (ibara za 74 (6) (b) - (d), lakini ipo juu ya sheria na wala haishitakiwi juu ya kazi yake yeyote ile au kuhojiwa na mahakama yeyote ile wakati ushindi wa baadhi ya kesi za uchaguzi ni ushahidi wa nguvu na dhahiri kabisa kuwa kinga hiyo ni batili (angalia ibara ya 74 (12) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania)!!!
74 (12) No court shall have the power to inquire into anything done by the Electoral Commission in the discharge of its functions in accordance with the provisions of this Constitution.
Zaidi ya hilo, kitendo cha mahakama kusikiliza kesi za uchaguzi zinazohusihana na kukiukwa kwa taratibu za uchaguzi ni sawa na kuhoji utendaji wa Tume hii ya Taifa ya uchaguzi, jambo ambalo linakinzana na ''umungu'' wa Tume hii ya Uchaguzi, na baadhi ya maamuzi yake, kama nilivyosema hapo juu, ni ushahidi tosha kuwa utendaji wake na watendaji wake wanapaswa kuhojiwa mahakamani na kuchukuliwa hatua endapo watapatikana na makosa. Wito kwa wananchi na wabunge kwa ujumla, hili tundu linahitaji kiraka ili sehemu za siri za mwili zisitiriwe.