Tuzo za waandishi wa habari Afrika: CNN | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuzo za waandishi wa habari Afrika: CNN

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Noti mpya tz, Jul 25, 2012.

 1. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  NImesikitika sana kuona hakuna hata mwandishi wa habari toka Tanzania alieingie katika list ya waandishi 30 bora Afrika huku wenzetu Kenya na Uganda wakig'ara, cha ajabu kabisa mwandishi bora wa habari za utalii akatoka Uganda na wakati Tanzania ndio ina vivutio kemu kemu vya utalii katika Afrika.

  Jana nilimsikia mmiliki wa CLOUDS MEDIA Joseph Kusaka ambae alikuwa mmoja wa waalikwa kwenye tamasha hilo lililofanyika nchini Zambia akisikitika na kuuliza nini kinawapata waandishi wa tanzania, au hawajui taratibu za shindano hilo ndo maana wanawasilisha kazi ambazo ziko sub standard?

  Lakini pia katika kupita pita humu jf jana nakutana na post kuwa kuna waandishi wa habari makanjanja ambao hata elimu hawana ametajwa Ramadhan Semtawa kuwa ana elimu ya darasa la saba huku akikitumikia chombo cha habari ambacho kinaheshimika sana nchini, Mwananchi.

  Lakini pia nimejaribu ku connect na jinsi uandishi wa habari ulivyo hivi sasa nchini, kwa wafuatiliaji wa vyombo vya habari wataniunga mkono kwa hili, Ukiangalia waandishi wetu walio wengi wameondoka kabisa katika maadili yao na kujikuta wakitumikia watu wengine na ushabiki wao wengine kwa kujua na wengine kwa kutojua, wengine kwa malipo na wengine bila malipo yoyote.

  Kiangalie chombo kama TBC, hawa wako wazi wanaitumikia serikali na chama chake, sasa wapo ambao wanatumikia vyama vya siasa kwa ushabiki wao, achana na vyombo vya habari vinavyomilikiwa na wahusika kama UHURU ambao hatutarajii kuandika habari ya kuikosoa ccm, achana na vyombo vinavyomilikiwa na madhehebu ya dini, angalia chombo vinavyomilikiwa na freemedia na kuna vyombo vinavyomilikiwa na watu binafsi ambavyo vingi vinafata matakwa na mapenzi ya waandishi husika, angalia vinavyomilikiwa na IPP, mwananchi, Habari corporation n.k.

  Hawa kama kuna mtu anataka kuwatumia kufikisha ujumbe au kampeni yake ni rahisi mno maana you don't need to go kwa mhariri wakati mwingi unaongea tu na mwandishi anakuwa anaandika habari zako tu, hii ni tofauti na vyombo vinavyomilikiwa na taasisi ambao inamlazimu mwandishi kufuata matakwa ya taasisi husika.

  Waandishi tanzania they are far thousands miles to wake up and walk to catch other journalists from other countries and mpaka hapo ngoja nisome gazeti la Shigongo ambalo najua ni mzaha mtupu kisha nikalale.
   
 2. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Waandishi wengi wa Tanzania hawana taaluma hiyo na hata wale wachache walikuwa na weledi wamejikita katika kutafuta pesa kwa kuvunja maadili na miiko ya uandishi wa habari.

  msitegemee kupata tunzo makini kama hizi kwani hizi ndani ya tunzo hizi pamoja na kuangalia weledi wa mwandishi lakin vile vile wanataka mtu ajikite kwa kufuata kanun na taratibu za kiuandishi na wengi wanaopata wanatakiwa wajikite kwenye uandishi wa kiuchunguzi jambo ambalo ni mtihani mkubwa sana kwa waandishi wa Tanzania.

   
 3. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Ni kweli, kule huwezi kupata tuzo kwa uandishi wa 'kulamba viatu' vya watawala pamoja na wengine. Sina uhakika sana kama hili linasababishwa na umasikini maana naona wengine wanazo resources na standards za maisha kuzidi hata hao waliopita. Taitizo zaidi naona ni kukosa upeo wa kuelewa mambo na kujitambua.

  Mfano, ile story ya 'an african tribe in India' pamoja na Wamasai wanaocheza cricket ambazo wametengeneza Wakenya ni mambo ambayo ukitafakari kidogo unagundua kuwa hapa tuna vitu vingi sana vya kuvutia/inspire dunia. Lakini wadau wanaangalia 'mkate wa kila siku'.

   
 4. Z

  Zimamoto JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 464
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  There are very few journalists in Tanzania, there are highly incompetent news reporters, who report in the interest of some individuals or groups of people. Nowdays there are many radio presenters who cannot speak standard Kiswahili, let alone English.
   
 5. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kwa hakika huyo mkenya alistahili kabisa kupewa Tuzo kwani alifanya investigation ya hali ya juu sana kufuatilia kwa kina sana maisha ya hao wakenya waliolowea India na kuishi huko lakin bado wakiwa wanafata mia na desturi za makabila yao ya kenya.

  Alifanya presentation yake nzuri sana na alistahiki kupata TUZO.

  Suala la kujiuliza je waTz mnaliweza hilo? au ndo story za uchochezi na majungu tu. Mtaishia kuwa wasindikizaji wa Tuzo kubwa kama hizo ambazo kwa kanda yenu zilifanyika mjini Lusaka Zambia.

   
 6. bongo-live

  bongo-live JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2016
  Joined: Jul 3, 2013
  Messages: 824
  Likes Received: 350
  Trophy Points: 80
  aiseeeee
   
 7. R

  Retina JF-Expert Member

  #7
  Mar 29, 2016
  Joined: Mar 6, 2015
  Messages: 660
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 80
  Waandishi wa habar wa Tz,wanafik wa kutupwa,katu haitatokea tena hiyo.
   
Loading...