Tuzo za Nobel za Amani na Fasihi ni tuzo za propoganda za kimagharibi zaidi

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,558
46,096
Wakati tukiendelea kusherekea Tuzo ya Nobel ya Fasihi aliyepewa Abdularazak Gurnah na kubishana kama ni Mtanzania, Mzanzibari au Muingereza, jamii ya wasomaji vitabu ilapaswa iwe na mjadala vigezo gani hutumika kumpa mwandishi hiyo tuzo na kazi gani za Gurnah ambazo ni maarufu au zimewahi kusomwa angalau na watu wachache wa Watanzania wa Africa Mashariki.

Ukweli ni kwamba jina la Gurnah ni jina geni miongoni mwa Watanzania wengi hata wenye elimu ya juu ya fasihi au lugha. Watanzania wengi hata waliofika kidato cha nne tu wanamfahamu Ngugi wa Thiong'o na Chinua Achebe, wapo pia wanaomfahamu Alan Paton mwandishi maarufu kwa Africa kusini na nchi zinazoizunguka. Pamoja na kazi zao nzuri na umaarufu mkubwa ndani ya bara zima la Africa na nje manguli hawa wa Fasihi hawajawahi kupewa Tuzo ya Nobel mpaka sasa.

Kinachowaponza manguli hawa ni kazi zao za uandishi kuonyesha udhalimu mkubwa uliofanywa na wakoloni wazungu kwa fasihi ya hali ya juu pamoja na tawala zilizofuata za hovyo zinavyoifanya Africa kuendelea kuwa na maisha ya hovyo, kazi zao zinawafungua Waafrika kuona matatizo halisi ya bara lao kwa fasihi ya kuvutia.Wenye tuzo hawajapendezwa na hawapendezwi na uandishi wa harakati za aina hizo.

Kwenye tuzo ya Amani ya Nobel nayo ina vituko vingi. Baadhi ya waliopewa hiyo Tuzo katika mazingira ya ajabu ni Pamoja na Barack Obama na Abiy Ahmed waziri mkuu wa sasa wa Ethiopia. Hawa wawili wamepewa tuzo wakiwa madarakani hata kabla ya kumaliza muda wao, Obama aliendelea na vita akiwa na tuzo mikononi, Abiy anaendelea na vita dhidi ya Tigray mpaka sasa.

Tuzo hizo mbili kwa kiasi kikubwa ni vyombo vya kushawishi aina za mfumo wa maisha na mitizamo ya kimagharibi na uwasilishwaji wake kwa dunia katika njia ambayo watu wa Ulaya wanaona inafaa zaidi. Zinakosa weledi kuakisi mafanikio ya fasihi na jitihada za amani katika sehemu kubwa ya dunia tofauti na Magharibi, Tusizishangilie sana.
 
Hata UMOJA WA MATAIFA(UN) ulianzishwa kwa mtizamo wa nchi za MAGHARIBI ....ila pamoja na yote...nasi tunafaidika.......


Afrika ikitaka kuzianzisha tuzo aina ya hizo sidhani kama ITASHINDIKANA.....

Tusisahau tuzo hizo za NOBEL wanapewa mpaka wanasayansi waliotuletea mapinduzi ya kimaisha duniani japo pamoja na makubwa aliyoyafanya NIKOLA TESLA hakupata kutunukiwa tuzo hizo.... 🤣🤣🤣

#SiempreJMT
 
Abdularazak Gurnah na kubishana kama ni Mtanzania, Mzanzibari au Muingereza
Hili mbona liko wazi.

Ni mwingereza, mzaliwa wa zanzibar, ( kwa mujibu wa sheria tulizonazo kwa sasa)

Hivyo, Sio mtanzania,

Na Hapa ndipo hoja za wadau zinakuwa na mashiko zaidi

1633683348320.png



 
Back
Top Bottom