Tuzo za MTV na Channel O

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082
<!--ThumbEnd-->
Hivi wadau kwa nini kila siku tunaona wa nigeria, south africa na mwaka huu ndugu zetu wa kenya wanachukua hizi tuzo za muziki ( MTV, Channel O) zaidi. Yaani kila mwaka wanawekwa wao tu, angalia nominees wa mwaka huu wamejazana kibao ktk vipengele vyote. Au ndo hawa MTV na Channel O wanajikosha kwa vile hizo nchi zina pesa (naamini sasa msemo wa Profesa Jay fedha inaongea).

Ni kama vile hakuna wasanii wakubwa nchi nyingine na wanaotesa vizuri tu ndani ya bara la Afrika, wengine wanasema sababu ni lugha ya kiingereza, hao wasanii wanaoshinda tuzo hizo kila mwaka wanatwanga lugha ya kiingereza, yaani badala kutoa tuzo kwa wasanii wanaotema lugha zao na wenye vipaji zaidi ya hao ili kuwapa moyo, wanaendelea kukandamiza vipaji vyao.

Mimi nilidhani hizi tuzo zitabadilika baada ya mwaka wa kwanza lakini ninachoona sasa ni tofauti, mimi nafikiri hizi tuzo zisiitwe "Africa Music Awards" bali "Nigeria & SA Awards". Yaani hata sijui kama hawa watu wa mtv na channel o wanajali nchi nyingine zaidi ya Nigeria na SA. Nakwambia Afrika kuna wanamuziki wakali sana lakini hizi tuzo kubwa wamelalia sana fedha zaidi ya kipaji.

Ushauri wangu watoe tuzo ili kukuza vipaji vya wasanii wa nchi tofauti na sio kwa baadhi ya nchi tu. (Msibane Habari Hii!)

http://www.globalpublisherstz.com/
 
Back
Top Bottom