Tuzo za Grammy zasogezwa hadi mwezi Machi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,861
Tuzo za Grammy za mwaka 2021 hazitafanyika tena mwezi huu huko Los Angeles Crlifornia na badala yake zitatangazwa mwezi Machi kwa sababu ya kuongezeka kwa visa vya virusi vya corona na vifo.

Waandaji wa tuzo hizo waliwaambia waandishi wa habari siku ya Jumanne kuwa onyesho la kila mwaka litasogezwa mbele kutoka tarehe yake ya awali ya Januari 31 hadi tarehe isiyojulikana mnamo mwezi Machi.

Tuzo hizo za Grammy zitafanyika Los Angeles katika Kituo cha Staples, Kaunti ya Los Angeles, ambako ndio kitovu cha ugonjwa huko California, ambako umezidi vifo 10,000 na imekuwa na asilimia 40 ya vifo . Beyonce ndiye anayeongoza katika tuzo hizo mwaka huu akiwa na uteuzi katika vitengo tisa.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom