Tuzo za Grammy: Burna Boy na Wizkid washinda tuzo za Grammy

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
21,713
35,512
Wasanii maarufu wa Nigeria Burna Boy na Wizkid wameshinda tuzo za Grammy za mwaka huu wa 2021.

Burna Boy ameshinda tuzo ya kipengele cha kuwa na Albamu bora ya muziki wakati Wizkid ameshinda katika kuwa na video bora zaidi kwa wimbo wake aliomshirikisha Beyoncé unaoitwa Brown Skin Girl, kutoka Lion King: Albamu ya The Gift.

Binti yake Beyoncé Blue Ivy alikuwa mshindi katika wimbo huo huo.

Katika kipengele cha video bora, tuzo inatolewa kwa msanii, muongozaji wa video na muandaaji wa video pia.

Burna Boy, ambaye jina lake halisi ni Damini Ogulu, ambaye ameshiriki kwa mwaka wa pili ameshinda katika albamu yake ya Twice As Tall .

Tuzo ya Grammy ya 63 imefanyika mjini Los Angeles. Kwa kawaida huwa sherehe kubwa ya muziki huwa inafanyika kila mwaka lakini mwaka huu hali imekuwa tofauti kutokana na janga la corona.

Hakuna watazamaji, na watumbuizaji walikuwa wametengwa katika majukwaa matano, na wakiwa kwa umbali.

Burna Boy, mwenye miaka 29, amewashinda wengine wanne ikiwemo bendi ya Malian, Tinariwen.

Tuzo za Grammy zimeielezea albamu ya Twice As Tall kuwa muziki uliotengenezwa kwa kiwango cha juu cha kimataifa, ni fundisho kuwa pia kwa wegine na ndio maana imemfanya Burna Boy kuingia katika kiwango hicho cha kimataifa".

"Aliendelea kusema kuwa kuwa albam hiyo imechanganya miondoko mbalimbali kama midundo ya pop, Afrobeat, dancehall, reggae na miondoko mingine mingi," walieleza.

Albumu yake ilishirikisha wanamuziki wengi duniani wakiwemo Stormzy, Youssou Ndour, Naughty By Nature, na Chris Martin wa Coldplay, na vilevile Sean Combs akiwa muandaaji mkuu.

Video ambayo imemfanya Wizkid kushinda imeelezewa kuwa imezingatia mitindo na kusheherekea urembo wa mwanamke mweusi mahali popote duniani ".

Burna Boy amechaguliwa katika kipengele kilekile cha mwaka 2019 - kinachojulikana kama 'Best World Music Album' - lakini Angelique Kidjo aishinda katika tuzo za mwaka 2020.

Ingawa Kidjo aliamua kutoa ushindi wake kwa Burna Boy, alisema: "Burna Boy ni miongoni mwa wasanii wachanga ambao wanatoka Afrika ambao wanabadili mtazamo wa muziki wa Afrika."

Mwanamuziki huyu aliyezaliwa Nigeria, Burna Boy alizindua albamu yake ya kwanza ya LIFE, mwaka 2013.

Na baadae alizindua albamu ya Redemption mwaka 2015 na Outside mwaka 2018 ambayo ilijumuisha ngoma iliyovuma kimataifa

Lakini ilikuwa katika albamu yake ya mwaka 2019 ya African Giant ambapo Burna Boy alijulikana zaidi kimataifa na kupata tuzo yake ya kwanza ya Grammys.

Akiwa analinganishwa na mwanamuziki wa Nigeria Fela Ransome-Kuti na kupata umaarufu barani Afrika.

Wakati wa mgogoro wa ubaguzi Afrika Kusini mwaka 2019, alitishia kutoenda katika taifa hilo kama serikali ya nchi hiyo haitachukua hatua dhidi ya xenophobic.

Pia alijumuishwa katika maamndamano ya #EndSARS ya kupinga unyanyasaji wa polisi, alitoa wimbo wa wahanga ambao waliuawa katika maandamano hayo Oktoba 20,2020 katika geti la Lekki Toll Gate mjini Lagos.

Vilevile ameandika katika kurasa yake ya tweeter kuunga mkono waandamanaji wa Senegal ambao walijitokeza barabarani baada ya kiongozi wa upinzani Ousmane Sonkokukamatwa.

View attachment 1726081View attachment 1726082


BBC/SWAHILI
 
Wizkid hii ni pili ya kwanza alishinda kwenye nyimbo aliyo shirikishwa na Drake.

Hongera zake Burnaboy,kuna kipindi alitaka kuacha mziki kabisa,ila naona mama yake mzazi alimpigania na sasa hivi ana manage kazi zote za mwanae.

Hii album Burnaboy ukiisikiliza upande wa production na ukilinganisha na productions za kazi zetu ni mbingu na ardhi,wasanii wa bongo wame invest kwenye kufanya Collabo kuliko kuzalisha kazi zenye ubora upande wa productions.

Tanzania tuna maproducer wazuri ila system yetu haiwalindi maproducer upande wa maslahi na ndio maana maproducer wanaojua wameamua kutafuta shunguli nyingine na kuachana na mziki.
 
Mshindi ni Burna.......

He's very serious and he deserves. Wizkid anawekwa kwa appreciation tu, maana wimbo ni wa Beyonce.

Mwaka jana na mwaka huu Burna kafanya kazi kubwa sana na wasanii wengi wakubwa kina John Legend ( kwenye soundtrack ya Coming2America), Sia, Stormyz, Sam Smith, Ed Sheeran etc.

Wanaijeria wako juu sana sasa hivi: Fireboy, Davido n.k kuperfom kwenye Late night shows US ni kawaida.

Congrats.
 
Hapo kwenye ubora wa utayarishaji na tungo inabidi wasanii wetu na watayarishaji wao wajifunze kitu. Sound ya Naija iko na viwango vya juu sana ukikinganisha na sound yetu, acha washinde tu.
Sisi huku tuna Muziki wa Instagram. Ni hype tu.

Instagram ikizimwa tu, asilimia 85 ya wasanii na watu maarufu wanapotea.

Producers wanaendeshwa na wasanii.
 
Hapo kwenye ubora wa utayarishaji na tungo inabidi wasanii wetu na watayarishaji wao wajifunze kitu. Sound ya Naija iko na viwango vya juu sana ukikinganisha na sound yetu, acha washinde tu.
Af unakuta wasanii wanalalamika media kucheza ngoma za west na south zaidi..Production ya kibongo haina taste kabisa..ngoma chache sana zinazotoka ndo zinakuwa na viwango.
 
Mshindi ni Burna.......

He's very serious and he deserves. Wizkid anawekwa kwa appreciation tu, maana wimbo ni wa Beyonce.

Mwaka jana na mwaka huu Burna kafanya kazi kubwa sana na wasanii wengi wakubwa kina John Legend ( kwenye soundtrack ya Coming2America), Sia, Stormyz, Sam Smith, Ed Sheeran etc.

Wanaijeria wako juu sana sasa hivi: Fireboy, Davido n.k kuperfom kwenye Late night shows US ni kawaida.

Congrats.
Alianza Burna kuperform kwenye SNL ( Saturday Night Live) hapo ndo nikaanza kukubali kuwa tumepigwa gap kubwa tayari.

Tunahitaji kizazi kingine waje na muziki utakaokuwa na authority.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom