swagazetu
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 4,250
- 1,467
Nilitegemea Mchezaji bora wa Afrika mbwana Samatta angepongezwa kitaifa kumbe anapongezwa kichama! Je heshima aliyoleta ni kwa Watanzania kama Taifa au Ccm? Nauliza kwa sababu kwanza namuona akiwa amelembwa na kupambwa vitambaa vya chama cha mapinduzi hata pale walipoandaa hafla ya kumpongeza.
Hivi ndivyo mpira wetu Tanzania usivyoweza kusonga mbele kwa sababu ccm wanafanya siasa kwa kila jambo wanafikiri na kutaka kila kitu kiwe na unasaba na chama chao! Vitu vingine havifungamani na siasa vinahitaji uzalendo bila kujali itikadi.
Wapo wadau ambao wangetoa mchango kuendeleza soka bongo lakini kutokana na siasa za Ccm. Wanashindwa.
Samatta kafanikiwa kwa juhudi zake binafsi 90% na zingine wazazi wake na makocha lakn leo tunaona amefanywa bango la kutangazia maslahi ya ccm.
Ningetegemea ktk hatua za kumpongeza abebe bendera ya Taifa badala ya ile ya Chama maana ndiyo ishara ya uwakilishi wake sasa leo anabebeshwa bango la ccm kana kwamba ni wakati wa kampeni.
Ccm jifunzeni busara hata kidogo lakini kama Samatta ameshinda kwa goli la mkono hoja yangu itupilieni mbali maana ccm ni mabingwa wa goli la mkono hivyo itakuwa haki yao wao kama meza ya ufundi ya Samatta.