Tuzo ya ICC-Dowans/Tanesco ni feki? Angalizo muhimu kwa Watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuzo ya ICC-Dowans/Tanesco ni feki? Angalizo muhimu kwa Watanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nderingosha, Oct 13, 2011.

 1. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2011
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,528
  Likes Received: 1,313
  Trophy Points: 280
  Imenibidi nilete changamoto hii kwa jukwaa la jamii forum ili ifanyiwe kazi haraka iwezekanavyo maana sisi kama watanzania tunaweza tukawa tumeingizwa mkenge uleule kama yalivyotokea mambo ya Richmund kwamba kampuni iligundulika feki kwa kujifanya mambo yao yamefanyika USA na kwingineko ulaya huku wakijua watanzania wana tatizo kubwa la kutafuta habari muhimu (kwa maana ya kutokutafiti mambo....yaani kutotaka kutafuta ukweli wa mambo haswa yale yafanyikayo nje ya mipaka ya Tz).Ili limekuwa tatizo hata kwa professionals wetu wa ndani (sijui ni kwanini kuna uvivu wa kujua issues haswa za nje zenye uhusiano na nchi yetu??....maana huku ndiko tunakoingizwa mikenge mikubwa....angalieni issue za rada...richmond na dowans na hata madini yetu yanavyouzwa nje...na hata ufisadi kwenye mabalozi yetu...huku ndiko tunakopigwa ipasavyo....maana hatufuatilii mambo yakishatoka nje ya TZ. Nimeanza hivyo nikitaka kuleta issue hii ya sakata la malipo ya hii tozo ya ICC kwa dowans. Nimefanya utafiti na kugundua yafuatayo kuhusu mchakato mzima wa jinsi dowans wanavyodai walipewa hii tozo...(tusijirizishe sana na documents zilizotumwa tz..kwani matapeli hawajulikani kwa documents). Hili linaweza likawa ni mkenge wa kufa mtu tumeingizwa kama nchi bila kujua(kwani mara ngapi hawa hawa professionals wetu wameingia mikenge???).Nianze kufafanua kama ifuatavyo alafu niwaachie mtafakari na mchukue hatua.....kila mtu kwa nafasi yake....
  • Kwa kuanza tu nianze kwa huyu bwana anayeitwa...Gerald Aksen. Huyu ameripotiwa kwenye magazeti kama ndie jaji aliyetoa eti hukumu katika kesi ya ICC International court of arbitration...yaani kesi imefanyika chini yake kama mwenyekiti. Katika profile yake huyu bwana ni retired prof.wa sheria katika law firm ya Thelen LLP-USA. Profile yake ni pana na amefanya kazi nyingi mojawapo ikiwa arbitration.Hajaandikwa kuwa aliwahi kuajiriwa na ICC ila kwasasa anafanya kazi kama self employed mediator and ADR Neutral. Katika hukumu ya ICC kwa Tanesco haijuklikani huyu bwana alitumikaje kwa ICC. Pata attachment yenye profile yake jumla hapa chini.
  • Katika ICC dispute resolutions...kazi ya ADR Neutral ni kama ifuatayo: kutumia busara,utaalamu na common sense katika dispute kati ya parties (pande husika).Pia kuonyesha imani kwa pande zote husika na kusaidia pande zote husika kufikia muafaka kwa manufaa ya pande zote mbili. Pia yeye ADR neutral kazi yake kubwa si jaji bali ni facilitator(mwezeshaji)kwa pande zote mbili kufikia muafaka.Yeye pia ndie anayeweza hata kuchagua ni lugha gani itumike katika shauri ili tu pawepo na muafaka na maelewano kwa manufaa ya pande zote mbili. Sasa kama hizi ndizo kazi za ADR Neutral wa ICC katika kutatua disputes...na kama huyu bwana alitumika na kwa experience yake ilivyo kubwa kwa maswala ya arbitration.....haiwezekani kabisa Tanesco washindwe kesi ile......haiwezekani hata kidogo.Sasa tujiulize nini kimefanyika?????.Nimeambatanisha document hapa yenye mchanganuo wa kazi za ICC ADR Neutral.Huyu bwana hawezi kuwa ametumiwa na ICC bila ya kuwa ADR Neutral na kama ametumiwa kama ADR Neutral na ICC basi haiwezekani Tanesco washindwe shauri lile.
  • Kama Gerald Aksen wanasema ametumika kama jaji wa ICC International court of arbitration.....pia haiwezekani kwani yeye si jaji na pia si mwanasheria tena kwani ameshastaafu.Profile yake inasema hajawahi kuwa jaji wa ICC court of arbitration.Soma attachment.
  • Sheria za ICC zinasema ADR Neutral anachaguliwa kwa makubaliano ya pande mbili husika au ICC wenyewe kwa kukubaliana na pande husika.Swali: je Tanesco walishiriki vipi kumchagua Gerald Aksen kama alitumika kama ADR Neutral?
  • ICC Dispute Board Centre inafanya kazi separate from the ICC International Court of Arbitration, the ICC International Centre for Expertise na pia ICC ADR Secretariat.Kama Tanesco hawakuridhika na maamuzi yaliyotolewa juu ya tuzo bado wangeweza kupeleka malalamiko kwenye ICC Dispute Board Centre au ICC ADR secretariat kama hawakuridhishwa na utendaji wa ADR Neutral. Swali: je Tanesco walifanya hivyo?????kwa mujibu wa ICC...tozo hutolewa baada ya makubaliano muafaka ya pande zote mbili.
  • Types of ICC ADR techniques:
  • Under the ICC ADR Rules, parties may freely choose the settlement technique they consider most appropriate to their situation.Je hili tozo lilikuwa appropriate kwa Tanesco kama mdau mmojawapo?????
  • 1)Mediation: The Neutral may meet each of the parties separately to help them find common ground for resolving the dispute amicably. Je common grounds zilifikiwa na pande zote mbili???
  • 2)Neutral evaluation: The parties seek the Neutral's non-binding opinion on such matters as:
  • An issue of fact:-Did the maintenance teams do what was expected of them?
  • A technical issue. Were the girders supplied in accordance with stress specifications? or did the generators produce emergence power to the country???(Tanzania)
  • An issue of law. Did the floods that held up delivery of essential spare parts constitute force majeure?
  • Then the panel either seeks a solution acceptable to all the parties or expresses an opinion on the positions of each side.
  • Ukifatilia hizi techniques za ICC dispute resolution kwa vyovyote vile kama zingefuatwa kweli kweli kwa hakika Tanesco wasingeshindwa kesi. Nimeambatanisha hapa attachment yenye haya yote please read!!!!!!.Pia nimeambatanisha sheria....rules document ya ICC dispute resolution hapa.Someni muamue kama watanzania hatuingizwi technical mkenge hapa....na hawa wanasheria wetu haya mambo hawasomi?????hawa kina mwanasheria mkuu wanafanya nini jamani??????
  • Kwa kumalizia tu nimtaje mshiriki mwingine katika shauri hili alikuwa huyu bwana Switilin Munyantwali.Huyu ni Mganda mwanasheria anayefanyia kazi marekani na alitumika nadhani kwa dowans. Yeye profile yake (attached) inaonyesha ni executive director wa African law institute in USA na pia ana majukumu chungu mzima....na ukiangalia huwezi amini alipata wapi muda wa kukaa kwenye shauri na kuwashinda Tanesco kwa hoja.Hawa jamaa wote wako nje ya nchi wakati Dowans walifanya kazi Tz.......na tatizo lilkuwepo tz, sasa vipi hawa jamaa washinde kesi???inaonyesha mapungufu makubwa yalikuwepo kwa upande wa Tanesco (walifanya kwa makusudi kabisa ili washindwe kesi...)kwani hakuna kigezo ambacho kingewazuia kushinda...
  • Mjamaa mwingine aliyeshirikishwa na dowans kama inavyosemwa ni huyu.....Jonathan Parker....huyu bwana nimeshindwa kujua ni Jonathan yupi haswa maana wako wengi (unapo search). Nimejikuta nikifikiri kuwa ni labda mcheza cricket...maana yupo pia mcheza cricket mwenye hili jin...naomba mumtafute profile....now that you get the tip and food for thouth as Great thinkers....
  Mwisho kabisa naungana na wote kupinga hii hela kupewa hawa matapeli......na nina uhakika hii hela ni utapeli.....kama kawaida unaofanywa na mitandao ya wajanja nje ikiwashirikisha wanasiasa wa maji tak tulio nao tz........nawasilisha.....find all the attachments please....
   

  Attached Files:

 2. M

  Madcheda JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 416
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35

  Hv sasa ni saa 7 na nusu usiku, ngoja nikalale zangu mie!!!
   
 3. kidi kudi

  kidi kudi JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 60
  Ndugu yetu binafsi nikushukuru nikiamini lipo kundi kubwa la wanajamii waliomo humu wakiwa ni memba au wasomaji tu wa kawaida wasio membazi wa hii foramu wameukubali mchango wako wa kutupa mwangaza wa sie kama watanzania tutakao/tunao athirika na ulipwaji wa mamia ya mabilioni yetu. shukrani sana! nitoe tu mtizamo na mawazo yangu kuhusu hili jambo, binafsi nimesoma kwa makini na nimegundua ya kwamba si mimi peke yangu ambae kwa uwezo na upèo wangu mdogo wa kupata habari sahihi na pia kuzitafakari taarifa nizipatazo,ambae siungi mkono kwa asilimia zote zilizopo dunian ulipwaji wa hayo mabilioni! watanzania kwa muda mrefu tumekua tukinyimwa fursa ya kutimiziwa haki yetu ya kupata taarifa tena sahihi pindi tunapozihitaji.
  Nitoe maoni yangu tu kwamba,hakuna sababu ya kukataa kulipa,cha msingi waliohusika kufanya madudu wanajulikana..kuanzia mwanasheria mkuu,waziri,waziri mkuu,alieileta dowans na kupewa mamlaka kisheria kuiwakilisha,na hata kampuni ya uwakili ilowakilisha tanesco,walilipe hilo deni! kwishaaa!!
   
 4. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Shukrani sana
   
 5. w

  wikolo JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 801
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Asante sana ndugu yangu kwa kazi yako nzuri manake hili nalo ni la kuliangalia kwa upekee wake. Naamini kuna watu hapa jamvini watatusaidia tu kujua hili suala. Mwanakijiji nasubiri kuuona mchango wako manake siku zote huwa unaona pale ambapo mimi binafsi siwezi.
   
 6. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2011
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,528
  Likes Received: 1,313
  Trophy Points: 280
  NYONGEZA:

  The ICC ADR Rules offer a framework for the amicable settlement of commercial disputes with the assistance of a neutral. They were launched in 2001 to replace the 1988 Rules of Conciliation. Under the ICC ADR Rules, parties may freely choose the settlement technique they consider most appropriate to their situation. This may be mediation, whereby a neutral helps the parties to settle their differences through negotiation; a mini-trial, in which a panel comprising a neutral and a manager from each party proposes a solution or gives an opinion; or a neutral evaluation of a point of law or fact. Common to all these techniques is the fact that the decision reached by or in collaboration with the neutral is not binding upon the parties. The success of the chosen technique will depend largely on the qualities of the neutral. He or she may be designated directly by the parties or appointed by ICC. In the latter case, the parties may specify certain requirements as to the qualifications or attributes the neutral should possess. Lastly, the parties are not limited to a single technique, but may find it useful to apply a combination of settlement techniques.
  Maswali ya kujiuliza:
  • Uamuzi wa usuluishi kati ya pande mbili husika si binding kati ya pande husika (yaani hauzifunganishi pande husika….yaani waweza kubadilishwa kama kulikuwa na tatizo kwenye mkataba…si lazima uwe wa mwisho).Je hii imekuwaje kwa Tanesco kubebeshwa tozo kirahisi???hapa kuna walakini.Huu ni mchezo mchafu….hii kitu ni feki jamani.

  • Mafanikio ya usuluhishi hutegemea ubora wa Neutral aliyetumika.Huyu bwana Gerald Aksen alitumikaje kwenye hii issue…maana inasemwa tu kuwa ndiye jaji….wakati sheria za ICC zinasema hamna jaji kwenye haya maswala bali facilitator (mwezeshaji).

  • Kanuni za ICC zinasema huyu Neutral huteuliwa na ICC au pande husika.Je Tanesco walihusishwaje kwenye uteuzi wa huyu bwana Gerald Aksen?

  • Pande husika zinatakiwa zitumie njia tofauti za usuluhishi na si moja tu ili kufikia muafaka, mfano, mediation, mini trial, etc (hii ni kw mujibu wa kanuni za ICC---someni).Je njia hizi tofauti zilitumika mpaka ukatoka uamuzi uliotoka????

  • Maswali ni mengi na mkisoma kwa makini mtagundua hii tozo si kweli na inaweza kuwa imepikwa kijanja kama ilivyowahi kutokea kuwa Richmond ilikuwa kampuni feki…….tufatilie….hapa kuna uwezekano kuwa Tanesco wamebebeshwa hukumu kihuni na kijanja……..haya mambo yanweza yasiwe na connection hata kule ICC kwenye Dispute secretariat or ADB ICC boards (ninaamini hivi)…you will tell me….time will tell.
   
 7. M

  Mwadada Senior Member

  #7
  Oct 14, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 142
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Du! Shukrani ndugu. Indeed the whole saga has been enginered by an intelligent syndicate in collaboration with unfaithfull leaders of this land. I have been saying this and i still insist that it's only a matter of time that things will be open to all. It's making sense that our nation should not pay that money. If real we have to pay for any case let the govt make those who are responsible in bringing this shame with their selfish intent be accountable in paying the money by any means, unless the citizens will make the govt accountable. It's once claimed that government doesn't know who the dowans owners are, the president either so who are we paying? Do they know them now? Are they real serious?How can they enter into contract with someone you don't know! Ghosh! God still loves this country that is why he is revealing these scandals and dirty games to us. For those with authority they have to be more wise in their decisions now more than ever. P'se my dear countrymen and women let us stand firm on this and in all matters which are intending to jeopardise our country. There is no politics in this,it's about our nation. Your pain is my pain in this. May our country be blessed.
   
 8. y

  yaya JF-Expert Member

  #8
  Oct 14, 2011
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu, shukrani kwa kutujuza kuhusu huu utapeli wa wazi tunaotaka kufanyiwa wa TZ.
  Mwenyezi Mungu iokoe nchi hii kutoka midomoni mwa mafisadi wenye uchu mkubwa na utajiri mkuu tulionao kwa majaliwa yako. Amina.
   
 9. M

  Massenberg JF-Expert Member

  #9
  Oct 15, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 1,173
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  ANGALIZO
  Nakubaliana na maelezo yako kumhusu Gerald Aksen lakini huyu Swithin Munyantwali ukiangalia website ya shirika lao utakuta kwamba lina affiliation Marekani na yeye ndiye Mkurugenzi Mkuu na anafanyia kazi Kampala, Uganda. Katika profile yake kumeandikwa kuwa hivi karibuni alikuwa "international arbitrator" kwenye shauri moja Afrika Mashariki kati ya mwekezaji na serikali. Je, yawezekana shauri hili likawa ndilo la Dowans?
   
Loading...