Tuzo ya DOWANS kwa TANESCO ni utapeli kama Richmond ilivyokuwa; Hakukuwa na hukumu ICC!

Imenibidi nilete changamoto hii kwa jukwaa la jamii forum ili ifanyiwe kazi haraka iwezekanavyo maana sisi kama watanzania tunaweza tukawa tumeingizwa mkenge uleule kama yalivyotokea mambo ya Richmund kwamba kampuni iligundulika feki kwa kujifanya mambo yao yamefanyika USA na kwingineko ulaya huku wakijua watanzania wana tatizo kubwa la kutafuta habari muhimu (kwa maana ya kutokutafiti mambo....yaani kutotaka kutafuta ukweli wa mambo haswa yale yafanyikayo nje ya mipaka ya Tz).

Ili limekuwa tatizo hata kwa professionals wetu wa ndani (sijui ni kwanini kuna uvivu wa kujua issues haswa za nje zenye uhusiano na nchi yetu??....maana huku ndiko tunakoingizwa mikenge mikubwa....angalieni issue za rada...richmond na dowans na hata madini yetu yanavyouzwa nje...na hata ufisadi kwenye mabalozi yetu...huku ndiko tunakopigwa ipasavyo....maana hatufuatilii mambo yakishatoka nje ya TZ. Nimeanza hivyo nikitaka kuleta issue hii ya sakata la malipo ya hii tozo ya ICC kwa dowans.

Nimefanya utafiti na kugundua yafuatayo kuhusu mchakato mzima wa jinsi dowans wanavyodai walipewa hii tozo...(tusijirizishe sana na documents zilizotumwa tz..kwani matapeli hawajulikani kwa documents). Hili linaweza likawa ni mkenge wa kufa mtu tumeingizwa kama nchi bila kujua(kwani mara ngapi hawa hawa professionals wetu wameingia mikenge???).Nianze kufafanua kama ifuatavyo alafu niwaachie mtafakari na mchukue hatua.....kila mtu kwa nafasi yake....
  • Kwa kuanza tu nianze kwa huyu bwana anayeitwa...Gerald Aksen. Huyu ameripotiwa kwenye magazeti kama ndie jaji aliyetoa eti hukumu katika kesi ya ICC International court of arbitration...yaani kesi imefanyika chini yake kama mwenyekiti. Katika profile yake huyu bwana ni retired prof.wa sheria katika law firm ya Thelen LLP-USA. Profile yake ni pana na amefanya kazi nyingi mojawapo ikiwa arbitration. Hajaandikwa kuwa aliwahi kuajiriwa na ICC ila kwasasa anafanya kazi kama self employed mediator and ADR Neutral. Katika hukumu ya ICC kwa Tanesco haijuklikani huyu bwana alitumikaje kwa ICC. Pata attachment yenye profile yake jumla hapa chini.
  • Katika ICC dispute resolutions...kazi ya ADR Neutral ni kama ifuatayo: kutumia busara,utaalamu na common sense katika dispute kati ya parties (pande husika).Pia kuonyesha imani kwa pande zote husika na kusaidia pande zote husika kufikia muafaka kwa manufaa ya pande zote mbili. Pia yeye ADR neutral kazi yake kubwa si jaji bali ni facilitator(mwezeshaji)kwa pande zote mbili kufikia muafaka.Yeye pia ndie anayeweza hata kuchagua ni lugha gani itumike katika shauri ili tu pawepo na muafaka na maelewano kwa manufaa ya pande zote mbili. Sasa kama hizi ndizo kazi za ADR Neutral wa ICC katika kutatua disputes...na kama huyu bwana alitumika na kwa experience yake ilivyo kubwa kwa maswala ya arbitration.....haiwezekani kabisa Tanesco washindwe kesi ile......haiwezekani hata kidogo.Sasa tujiulize nini kimefanyika?????.Nimeambatanisha document hapa yenye mchanganuo wa kazi za ICC ADR Neutral.Huyu bwana hawezi kuwa ametumiwa na ICC bila ya kuwa ADR Neutral na kama ametumiwa kama ADR Neutral na ICC basi haiwezekani Tanesco washindwe shauri lile.
  • Kama Gerald Aksen wanasema ametumika kama jaji wa ICC International court of arbitration.....pia haiwezekani kwani yeye si jaji na pia si mwanasheria tena kwani ameshastaafu.Profile yake inasema hajawahi kuwa jaji wa ICC court of arbitration.Soma attachment.
  • Sheria za ICC zinasema ADR Neutral anachaguliwa kwa makubaliano ya pande mbili husika au ICC wenyewe kwa kukubaliana na pande husika. Swali: je Tanesco walishiriki vipi kumchagua Gerald Aksen kama alitumika kama ADR Neutral?
  • ICC Dispute Board Centre inafanya kazi separate from the ICC International Court of Arbitration, the ICC International Centre for Expertise na pia ICC ADR Secretariat.Kama Tanesco hawakuridhika na maamuzi yaliyotolewa juu ya tuzo bado wangeweza kupeleka malalamiko kwenye ICC Dispute Board Centre au ICC ADR secretariat kama hawakuridhishwa na utendaji wa ADR Neutral. Swali: je Tanesco walifanya hivyo?????kwa mujibu wa ICC...tozo hutolewa baada ya makubaliano muafaka ya pande zote mbili.
Types of ICC ADR techniques:

· Under the ICC ADR Rules, parties may freely choose the settlement technique they consider most appropriate to their situation.Je hili tozo lilikuwa appropriate kwa Tanesco kama mdau mmojawapo?????

· 1) Mediation: The Neutral may meet each of the parties separately to help them find common ground for resolving the dispute amicably. Je common grounds zilifikiwa na pande zote mbili???

· 2)Neutral evaluation: The parties seek the Neutral's non-binding opinion on such matters as:

· An issue of fact:-Did the maintenance teams do what was expected of them?

· A technical issue. Were the girders supplied in accordance with stress specifications? or did the generators produce emergence power to the country???(Tanzania)

· An issue of law. Did the floods that held up delivery of essential spare parts constitute force majeure?

· Then the panel either seeks a solution acceptable to all the parties or expresses an opinion on the positions of each side.
  • Ukifatilia hizi techniques za ICC dispute resolution kwa vyovyote vile kama zingefuatwa kweli kweli kwa hakika Tanesco wasingeshindwa kesi. Nimeambatanisha hapa attachment yenye haya yote please read!!!!!!.Pia nimeambatanisha sheria....rules document ya ICC dispute resolution hapa.Someni muamue kama watanzania hatuingizwi technical mkenge hapa....na hawa wanasheria wetu haya mambo hawasomi?????hawa kina mwanasheria mkuu wanafanya nini jamani??????
  • Kwa kumalizia tu nimtaje mshiriki mwingine katika shauri hili alikuwa huyu bwana Switilin Munyantwali.Huyu ni Mganda mwanasheria anayefanyia kazi marekani na alitumika nadhani kwa dowans. Yeye profile yake (attached) inaonyesha ni executive director wa African law institute in USA na pia ana majukumu chungu mzima....na ukiangalia huwezi amini alipata wapi muda wa kukaa kwenye shauri na kuwashinda Tanesco kwa hoja.Hawa jamaa wote wako nje ya nchi wakati Dowans walifanya kazi Tz.......na tatizo lilkuwepo tz, sasa vipi hawa jamaa washinde kesi???inaonyesha mapungufu makubwa yalikuwepo kwa upande wa Tanesco (walifanya kwa makusudi kabisa ili washindwe kesi...)kwani hakuna kigezo ambacho kingewazuia kushinda...
  • Mjamaa mwingine aliyeshirikishwa na dowans kama inavyosemwa ni huyu.....Jonathan Parker....huyu bwana nimeshindwa kujua ni Jonathan yupi haswa maana wako wengi (unapo search). Nimejikuta nikifikiri kuwa ni labda mcheza cricket...maana yupo pia mcheza cricket mwenye hili jin...naomba mumtafute profile....now that you get the tip and food for thouth as Great thinkers....
Mwisho kabisa naungana na wote kupinga hii hela kupewa hawa matapeli......na nina uhakika hii hela ni utapeli.....kama kawaida unaofanywa na mitandao ya wajanja nje ikiwashirikisha wanasiasa wa maji tak tulio nao tz........nawasilisha.....find all the attachments please....


NYONGEZA:

The ICC ADR Rules offer a framework for the amicable settlement of commercial disputes with the assistance of a neutral. They were launched in 2001 to replace the 1988 Rules of Conciliation. Under the ICC ADR Rules, parties may freely choose the settlement technique they consider most appropriate to their situation. This may be mediation, whereby a neutral helps the parties to settle their differences through negotiation; a mini-trial, in which a panel comprising a neutral and a manager from each party proposes a solution or gives an opinion; or a neutral evaluation of a point of law or fact. Common to all these techniques is the fact that the decision reached by or in collaboration with the neutral is not binding upon the parties. The success of the chosen technique will depend largely on the qualities of the neutral. He or she may be designated directly by the parties or appointed by ICC. In the latter case, the parties may specify certain requirements as to the qualifications or attributes the neutral should possess. Lastly, the parties are not limited to a single technique, but may find it useful to apply a combination of settlement techniques.


Maswali ya kujiuliza:

· Uamuzi wa usuluishi kati ya pande mbili husika si binding kati ya pande husika (yaani hauzifunganishi pande husika….yaani waweza kubadilishwa kama kulikuwa na tatizo kwenye mkataba…si lazima uwe wa mwisho).Je hii imekuwaje kwa Tanesco kubebeshwa tozo kirahisi???hapa kuna walakini.Huu ni mchezo mchafu….hii kitu ni feki jamani.

· Mafanikio ya usuluhishi hutegemea ubora wa Neutral aliyetumika.Huyu bwana Gerald Aksen alitumikaje kwenye hii issue…maana inasemwa tu kuwa ndiye jaji….wakati sheria za ICC zinasema hamna jaji kwenye haya maswala bali facilitator (mwezeshaji).

· Kanuni za ICC zinasema huyu Neutral huteuliwa na ICC au pande husika.Je Tanesco walihusishwaje kwenye uteuzi wa huyu bwana Gerald Aksen?

· Pande husika zinatakiwa zitumie njia tofauti za usuluhishi na si moja tu ili kufikia muafaka, mfano, mediation, mini trial, etc (hii ni kw mujibu wa kanuni za ICC---someni).Je njia hizi tofauti zilitumika mpaka ukatoka uamuzi uliotoka????

· Maswali ni mengi na mkisoma kwa makini mtagundua hii tozo si kweli na inaweza kuwa imepikwa kijanja kama ilivyowahi kutokea kuwa Richmond ilikuwa kampuni feki…….tufatilie….hapa kuna uwezekano kuwa Tanesco wamebebeshwa hukumu kihuni na kijanja……..haya mambo yanweza yasiwe na connection hata kule ICC kwenye Dispute secretariat or ADB ICC boards (ninaamini hivi)…you will tell me….time will tell……
Kwanza kabisa, Samahani sana kwa kuiquote hii taarifa, kwa kweli ni ndefu
sana kuiquote. Pili ahsante sana mleta hoja kwa kuonyesha uzalendo wako kwa vitendo, hapa ndo unaonesha umuhimu wa kuelimika. Tatu nashauri habari hii ungeiweka pia kwenye magazeti mbalimbali kama maoni au habari maalum maana si wengi wanaofika huku.

Hili suala ni limegubikwa na wingu kubwa, Mafisadi wameshaisoma tabia ya watanzania walio wengi na sasa hivi wameamua kuuweka huu utapeli kwenye maandishi kwa vile wanajua kuwa ukitaka kumficha kitu "mtu mweusi" kiweke kwenye maandishi/vitabu, vile wanajua sisi ni wavivu kusoma na kufuatilia mambo yaliyokwenye format ya maandishi. Hata idadi ya viewers/contributors kwenye hii mada/thread inadhihirisha hilo, kwani wengi wameogopa urefu wa hii mada. If that is the case we need to use other means to make this fact reach majority of Tanzanians, either through mijadala ya kitaifa au other ways of communication ili umma ujue kinachoendelea, pia wape wanaharakati mbalimbali hii fact ili wabuild case from there. Serikali inaita Hukumu ya ICC, Pinda na wanasheria wetu uchwara incl. Mwanasheria mkuu wanaona nchi inastahili kulipa hizo 111bil na wanataka malipo ya harakishwe bila hoja ya msingi kufanya hivyo.

Hapa watanzania tusimame na kupinga hii wanayoiita hukumu hadi some doubts ziwe cleared. Nashangaa serikali kuwa na ari kubwa ya utayari na uharaka wa kulipa huu wizi wakati serikali inadaiwa na walimu, wazee wa east africa na wengine kibao na hawataki kuwalipa, kama pesa zipo nje nje hivyo si walipe walimu wa watu wanaowafundisha wanetu kwenye mazingira duni jamani?????Ni lini tutaachana na haya maudhi yanayoletwa na hili liserikali la wezi????
 
Hapa watanzania tusimame na kupinga hii wanayoiita hukumu hadi some doubts ziwe cleared. Nashangaa serikali kuwa na ari kubwa ya utayari na uharaka wa kulipa huu wizi wakati serikali inadaiwa na walimu, wazee wa east africa na wengine kibao na hawataki kuwalipa, kama pesa zipo nje nje hivyo si walipe walimu wa watu wanaowafundisha wanetu kwenye mazingira duni jamani?????Ni lini tutaachana na haya maudhi yanayoletwa na hili liserikali la wezi????

Tupo Pamoja Mkuu!!!!!
 
Tupo Pamoja Mkuu!!!!!
Kiongozi utendaji wa serikali yetu unaudhi sana, ss vijana tusipokuwa wakali na makini, hatutapata cha kuwaachia wajukuu wetu, hiki kikundi cha wezi wa mali za taifa kinadhani maisha yanaishia kwao na familia zao.
 
ANGALIZO - huyo mtajwa wa pili, Swithin Munyantwali anafanya kazi na shirika la sheria lenye affiliation Marekani lakini yeye yuko Kampala kama Mkurugenzi Mkuu. Ukisoma profile yake utaona jinsi ilivyoshiba, na kuna mahala inasema hivi karibuni alikuwa "international arbitrator" kwenye shauri moja hapa Afrika Mashariki baina ya mwekezaji na serikali.
Je, yawezekana shauri hili ndiyo hilo la Dowans?
 
Samahani wakuu,
Kesi ya TANESCO na DOWANS ni kesi inayotambulika kimataifa na ndani ya nchi.
TANESCO walikataa settlement, waziri mkuu akasitisha malipo kwa DOWANS.
Huu ni mfano mzuri wa siasa kuingilia technocrats. Ni aibu kubwa sana kwa TANESCO,Bunge na Serikali.
We don't have a case here, let it go.
 
Naomba Tanesco waharakishe kuwalipa hawa jamaa. Mwanzoni deni lilikuwa 94bl, sasa limefika 111bl. Tunazidi kuchelewesha malipo.

Maji yakishamwagika hayazoleki.

TANESCO wafanye haraka kwa sababu umeona dili linataka kuota mbawa eeh? Piga uwa hiyo pesa mtaendelea kuisoma magazetini tu. JK kama alikopa atajiju na RA wake.
 
Samahani wakuu,
Kesi ya TANESCO na DOWANS ni kesi inayotambulika kimataifa na ndani ya nchi.
TANESCO walikataa settlement, waziri mkuu akasitisha malipo kwa DOWANS.
Huu ni mfano mzuri wa siasa kuingilia technocrats. Ni aibu kubwa sana kwa TANESCO,Bunge na Serikali.
We don't have a case here, let it go.

Tofauti ni kuwa argument yako haina basis, hakuna references ni maneno tu ya mdomo. Mwenzako katupa references ili tuangalie ukweli ulivyo. So your argument will make sense if you support it with some references.

Do you mind going out and do your assignment?
 
Tofauti ni kuwa argument yako haina basis, hakuna references ni maneno tu ya mdomo. Mwenzako katupa references ili tuangalie ukweli ulivyo. So your argument will make sense if you support it with some references.

Do you mind going out and do your assignment?
Kasome hukumu,
Hapo kuna reference yoyote unayoiona?.... apart from trying to make "ICC" look fake?
ICC is arecognizable institution, na huwa haitenguliwi na mahakama yoyote. Msilazimishe vitu just because our ignorant politicians think so.
Hivi kuna mtu na akili yake anaweza kusema ICC na wale majaj ni fake?
Ka zaidi naomba msome hukumu nyingine iliyotolewa na "United Kingdom High Court, july 27,2011" au nayo hamuiamini?
 
serikali ya ccm haina mzalendo yote majizi tu wala hayana lolote. Lakini muda wao mfupi sana watamalizia maisha yao jela hasa hasa hawa maraisi wawili na watu wao wa karibu.
 
Wala serikali yangu niijuayo haitajishughulisha na hoja hii yenye mashiko. Nijuacho tutakuja kuelezwa baadaaae kuwa DOWANS walishalipwa!
 
Labda na hii hapa itasaidia!!!!!

Gerald Aksen
Contact Information
805 Third Avenue, 10th Floor
New York NY 10022
Phone: (212) 752-1000
Fax: (212) 355-4608
Email: gerald.aksen@yahoo.com

Profession
Attorney, Arbitrator, ADR Neutral
Current Employer
Self-employed

Work History
Full time arbitrator, mediator and ADR neutral, 2003 to present; Partner, Thelen Reid & Priest LLP (and predecessor firm Reid & Priest LLP), 1981-2002; General Counsel, American Arbitration Association/attorney and assistant to the President, American Arbitration Association, 1961-1980; Private Practice,1958-60.

Experience
Many years of experience as counsel and arbitrator in domestic and foreign arbitrations in 18 different countries. Also, 30 years as adjunct professor of law at New York University School of Law, teaching courses on domestic and international arbitration.
Extensive experience as an arbitrator and mediator. Arbitrator in over 200 cases ranging in value from $1 million to $1 billion. Serves as an arbitrator and mediator with the American Arbitration Association, National Futures Association, International Chamber of Commerce, London Court of International Arbitration, Japan Commercial Arbitration Association, Arbitration Institute of the Stockholm Chamber of Commerce and under UNCITRAL, ARIAS, BERMUDA FORM and other ad hoc rules, as well as with the United States District Court for the Eastern District of New York Early Neutral Evaluation Program.

Training
Participant in training by the American Arbitration Association, International Chamber of Commerce, CPR Institute for Dispute Resolution, the Eastern District of New York and the National Futures Association.

Licenses
Admitted to the Bar: New York, 1959; Federal, 1961; U.S. Supreme Court, 1964; U.S. Circuit Courts of Appeals for the Second, Fifth, Ninth, Eleventh and DC Circuits; U.S. District Courts for the Eastern and Southern Districts of New York.

Awards
2005 recipient of the prestigious D’Alemberte/Raven Award from the Section of Dispute Resolution of the American Bar Association.
Associations
Former President, College of Commercial Arbitrators; vice-chairman of the ICC International Court of Arbitration; Association of the Bar of the City of New York, Member, Committee on International Commercial Dispute Resolution, 2000-; (Chairman, Arbitration Committee, 1970-72; Chairman, Ad Hoc Committee on Alternative Dispute Resolution, 1993-94); American Bar Association (Member, House of Delegates, 1985-88); Chairman, Section of International Law and Practice, 1982-83).

Education
CCNY (BA-1951); Columbia University (MA-1952); New York University School of Law (LLB-1958).

Publications
Author of numerous publications primarily relating to arbitration issues.

Miscellaneous
Citizenship: United States of America
Locale : New York, NY

Inform @: College of Commercial Arbitrators
 
Prof. TIBA anamfahamu Swithin Munyantwali?

Swithin Munyantwali is a U.S. qualified lawyer admitted to practise before the Supreme Court of Pennsylvania. He is also the Executive Director and Co-Founder of the International Law Institute African Centre for Legal Excellence (ILI-ACLE). He is an advisor and Board member to international entities such as UNCTAD, the Centre for Strategic and International Studies, and the ABA-UNDP Advisory Board Centre in Washington, DC. He has also served as an advisor to major US entities on strategic investments in Africa. He was appointed by the UN Habitat to a special committee to advise on special investment initiatives by UN Habitat.

Na huyu hapa je?

Charles Rwechungura is the Managing Partner and founder of CRB Attorneys in Dar es salaam. He is a seasoned consultant in the fields of mining, corporate, banking and financial law. He regularly advises mining exploration and extraction companies on corporate and commercial issues and has conducted multiple large-scale due diligence exercises for foreign investors looking to invest in the Tanzanian mining sector. In addition to his expertise in the mining sector, he is often appointed to act as an arbitrator on complex commercial disputes.

Hawa ni members wa Advisory Board of Africa International Legal Awareness
 
Ama kweli mtaji mkubwa wa magamba ni ujinga wa mtanzania, but thanks to a few patriots who saw need to reveal the truth behind these culprits. Mkuu tuko pamoja!
 
Wengi mnatoa arguments based on paper work iliyoletwa TZ kama hukumu ili isajiliwe mahakama kuu kwa ajili ya malipo. Nizidi kusema tu huu ni ule ule muendelezo wa niliyosema mwanzo kuwa watanzania tufike mahali tuwe tunafanya follow up ya vitu.....yaani kwa vile wamekuja wajanja na makaratasi yenye kuonyesha hukumu basi yachukuliwe na kulipwa mara moja!!!!! eti kwa kuwa kuna &nbsp;vipengele venye kuonyesha madhara ya kutolipa!!!hii mikenge watanzania tutazidi kuingizwa kwa kuwa hatuhoji......kwa vile eti issue imepitia ICC (as they say!!)then lazima ilipwe!!!!hatutaki hata kujua mchakato mzima uliopitiwa ili kuja na hii so called hukumu ya ICC ulifanyikaje!!hata kama Tanesco kuna vipengele muhimu kwenye hoja yao vilikiukwa na wao kushindwa basi walipe tu!!!! Niseme tu kuwa kama kweli &nbsp;sheria za mashauri ya disputes kwenye ICC zilifuatwa, kwa maana ya pande zote husika(haswa Tanesco)kusikilizwa ipasavyo tangu walipoingia mkataba na richmond (ambao ni batili), na jinsi dowans walivyorithi mkataba batili toka richmond,mkataba ambao eti ndio umewafunga kwenye shauri, kweli kabisa..ICC Neutral kama alifanya kazi yake kwa maadili,haiwezekani Tanesco washindwe kwenye shauri. Kuna mambo ya muhimu hapa ya kuzingatia....<br><br><ul><li>Sheria za ICC ADR disputes zinasema mikataba inayoingiwa na parties haitakiwi kuwa binding(yaani haitakiwi kuzifunga pande husika),vinginevyo duniani watu wasingefanya biashara kimataifa maana mara nyingi mikataba huvunjwa kwasababu mbalimbali na pande husika hufikia makubaliano (kupitia huko huko ICC)kwa manufaa ya pande zote husika. Kwa maana kama miakataba ingekuwa yote ni binding basi biashara nyingi kimataifa zingekuwa zinakufa.(kwa maana ya mmoja kumfilisi mwingine pale anapovunja mkataba)......hii ipo hata kwenye provisions za ICC. Kwa maana hii mkataba wa richmond tayari ulikuwa na makosa ...kiufundi jambo ambalo lingeangaliwa na IDR Neutral lingewapa faida Tanesco kwenye maamuzi yaliyofikiwa mwishoni mwa shauri.......hii kitu haikuangaliwa.</li><li><br></li><li><br></li><li>Mkataba kati ya Tanesco na richmond (ambao ndio ulitumika kutoa maamuzi) tayari ulishajulikana kuwa batili kwa ujumla wake kwa vile richmond tayari ilikuwa imegundulika kuwa ni kampuni feki.............sasa ni shauri gani lingeweza kufikiwa kwa kupitia mkataba feki??????niseme tu...kama kweli ICC ADR Neutral aliyetumika alikuwa makini (kama hakuwa na maslahi yoyote na uamuzi) basi hapa pangetosha kusimamisha shauri immediately......kwa maana sheria za ICC zinasema kama Neutral ameona kuwa kuna tatizo kwenye makubaliano asi anaweza kusimamisha shauri lisiendelee,,,,,,,,someni hizi provisions ndugu zangu.........kwa maana hii hapa Tanesco angeshinda....</li></ul><br><br><ul><li>Kuna njia tofauti za kufikia shauri na kuna board za ICC na ICC dispute secretariat ambako Tanesco (kama kweli walikuwa na uchungu na malipo)basi wangeweza kulalamika kabla ya kubebeshwa eti hukumu.........sasa tuwaulize Tanesco, je walifanya nini kule ICC baada ya kubebeshwa inayoitwa huku???au wamekaa TZ wakaletewa makaratasi na kina Kingamkono kuwa hii ndi hukumu?????niseme tu kuwa hata wanasheria wetu watanzania kuna ambao wameonyesha kukosa sana uzalendo kwenye maswala yanayohusu....maslahi ya nchi.....tuna mifano mingi.....hivyo tusishangae wale rex attorneys kushindwa.......tumeona wanasheria wakiwaachia wale jamaa wapakistani walioiba wanyama KIA....wakaondoka zao Tz (sijui kama wamerudi?),.......tumeona nchi ikiingizwa mikenge kibao(kwa kupita wanasheria wetu)kwenye issue za mikataba ya madini......tena wengine wana majina makubwa tu.....hivyo tusije kufikiri kuwa wale Rex walijaribu mpaka mwisho wa uwezo wao kuwasaidia Tanesco(mi siwaamni chembe hawa jamaa).....na kwanini Tanesco bado wanaendelea nao hawa Rex???????</li><li><br></li><li>Mwisho: Nimeona hapa kwa gazeti la mwananchi kuwa D.Ringo Tenga katokea kusema ndie alisaini mkataba wa richmond na Tanesco, na pia yule mwanasheria wa Tanesco (sitaki hata kumjua jina)....sasa....wewe mtanzania unasaini mkataba(hata kama ni kazi yako)na unaona kuna vipengele ambavyo vitaidhuru nchi, kweli una saini tu!!!!!!!hivi &nbsp;sasa naona hata nafsi zao zinawauma hawa so called Tz lawyers....wanapoona nchi nzima wanalia dowans wasilipwe.....its so bad yaanii.........kweli naamini msemo kuwa adui wa mtanzania ni mtanzania mwenyewe....hili tunaliona kila kukicha nchi hii..................labda hapa nichambue baadhi ya hoja za Dr.Ringo Tenga....chini:</li></ul><br><em><strong>Dk. Tenga alisema hajaisoma hukumu ya Jaji Mushi kuhusu tuzo ya Dowans, lakini kama kuna kipengele ambacho Tanesco inaona kimekiukwa katika hukumu hiyo, wanaweza kukata rufaa Mahakama ya Rufani.<br><br>Alisema sheria ya usuluhishi nchini sura ya 15, inaeleza wazi kuwa unaweza kukata rufaa kupitiwa upya hukumu kama msuluhishi aliyesikiliza kesi hiyo kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi, alisikiliza upande mmoja, hakuweka kumbukumbu sawasawa maelezo ya ushahidi au msuluhishi alikuwa na mgongano wa kimaslahi katika kesi hiyo.<br><br>Hata hivyo, Dk Tenga aliishauri Serikali kuwa wakati wa kuingia mikataba mikubwa kimataifa, lazima ifuate weledi wa watalaam.<br><br><br></strong></em><ul><li>Labda tu ieleweke kuwa....kama tanesco watakata rufaa mahakama kuu kwa kupitia makaratasi waliyotumiwa kama hukumu ya ICC basi tusitegemee washinde kwani watabaki kukazia kipengele cha kuwa mambo yakiamuliwa ICC basi hayatenguliwi na mahakama za ndani za nchi....</li></ul><br><br><ul><li>Angalizo: mkazo au rufaa....ipelekwe.. kwenye origin ya hukumu..yaani kule ICC....kwamba je sheria zilifuatwa?????Neutral alikubalika pande zote husika????Neutral hakuwa na maslahi binafsi????tanesco walihusishwa kwenye hatua zote za usuluhishi?????hoja za msingi za tanesco zilisikilizwa na Neutral????????kwa maana hii.......rufaa isikatwe mahakama ya rufaa bali ipelekwe ICC ADR Boards au ICC Dispute Resolution Secretariat.....wale watapitia tena hoja kwa hoja na pia tanesco wakazie ubatili wa mkataba waliorithi richmond.....ni &nbsp;kwa njia hii pekee Tanesco wataweza shinda.......na mwisho kabisa kama Tanesco watarudi ICC......wasiwatumie tena Rex........wanatakiwa wabadili wanasheria watumie watu makini wenye uchungu na nchi hii kama kina Dr.Sengodo Mvungi........Shivji etc.......hawa hawawezi kununuliwa.......ni wazalendo.............</li></ul><br><br>
 
Pumba tupu. Endeleeni kuididimiza nchi kwa utafiti wenu uchwara. Unatafiti kwenye internet? Unanchekesha!
 
Pumba tupu. Endeleeni kuididimiza nchi kwa utafiti wenu uchwara. Unatafiti kwenye internet? Unanchekesha!

Unajua wewe kwa hakika mtu yeyote anayefuatilia michango yako huwa anabaki na conclusion kuwa inawezekana intellectual capacity yako ni well below average. Huwa unakurupuka na kulipuka bila hata kuelewa msingi wa hoja ni nini. Sasa unaposema haya mambo ni pumba kwa vile utafiti umefanywa kwenye internet, je unaweza kueleza wapi mtu afanye utafiti iwapo anataka kufahamu ICC na ufanyaji wake wa kazi? Tupatie basi hizo sehemu mbadala ambazo wewe huwa unakwenda kufanya utafiti (kama hata uwezo wa kutafiti jambo unao).
 
Unajua wewe kwa hakika mtu yeyote anayefuatilia michango yako huwa anabaki na conclusion kuwa inawezekana intellectual capacity yako ni well below average. Huwa unakurupuka na kulipuka bila hata kuelewa msingi wa hoja ni nini. Sasa unaposema haya mambo ni pumba kwa vile utafiti umefanywa kwenye internet, je unaweza kueleza wapi mtu afanye utafiti iwapo anataka kufahamu ICC na ufanyaji wake wa kazi? Tupatie basi hizo sehemu mbadala ambazo wewe huwa unakwenda kufanya utafiti (kama hata uwezo wa kutafiti jambo unao).
Hii kesi ilishapelekwa UK high Court,na Tanzania high court.. both in favor of Dowans. Tuachane na wanasiasa wetu mbumbumbu (CCM,CDM,CUF ), It's irritating!! let it goo!!
 
Nimependa ufuatiliaji huu, nawaomba muendelee kutujuza maana si wote tuwezao kufanya hivyo.
 
Back
Top Bottom