Sanctus Mtsimbe
R I P
- Jul 14, 2008
- 1,820
- 1,032
TPN kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali Tanzania inapenda kupata maoni ya namna gani ya kutoa TUZO maalumu kwa Mtanzania ambaye atakuwa ametoa mchango mkubwa katika jitihada za kuboresha maisha ya Mtanzania wa kawaida katika kipindi husika.
Hili ni moja ya madhumuni ya TPN.
Katika utafiti wetu wa awali kuna wadau ambao bila shaka wangependa kusaidia katika gharama za utayarishaji wa TUZO hiyo ambayo tunategemea itakuwa na thamani kubwa na inayoendana na mchango mtunzwaji ili kuwatia moyo wengine wafanye vizuri.
Maoni yatakayotolewa yanaweza kuwa katika maeneo yafuatayo:
Maoni yote yatahaririwa na kisha kuwa na mchanganuo wa wazi ambao utakubalika na Watanzania walio wengi.
Naomba kutoa hoja!

- Jina la TUZO
- Atakayeikabidhi TUZO kwa Mshindi
- Vigezo vya ushindani na vya kupata mshindi
- Wanakamati/Waamuzi/Wadau watakaopitia maombi na kumchagua mshindi
- Utaratibu wa kupata mshindi/ Je anaweza kunyang'anywa TUZO?
- Sherehe za kuikabidhi TUZO
- Tuzo itolewe kila baada ya muda gani? na maoni Mengineyo
Maoni yote yatahaririwa na kisha kuwa na mchanganuo wa wazi ambao utakubalika na Watanzania walio wengi.
Naomba kutoa hoja!