Tuzivunje pia kumbukumbu mbaya kwetu.

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
5,958
2,000
Kufuatia kifo Cha Floyd kwa sababu za kibaguzi, dunia inapambana kuondoa kumbukumbu mbaya kwa mwafrika dhidi ya wazungu na watu weupe.

Wakati wenzetu wakipambana kuvunja masanamu ya watu walioutweza uafrika huko nyuma sisi tunazitunza eti kuja kuwaonyesha wazungu ili watupe fedha. Mimi sijawahi kuona mzungu akisikitika, kutoa machozi na kujutia anapoonyeshwa masalia ya utumwa na ukoloni. Badala yake inazidi kuwakumbusha ubora wao dhidi ya watu wengine hasa waafrika.

Huu Ni muda ya kupoteza kabisa masalia yoye ya kumbukumbu mbaya dhidi ya mwafrika Kama vile minyororo ya watumwa, miti walimonyongewa waafrika, masoko ya watumwa, makubuli ya watu waliowatweza watu weusi, nk ili kuungana na vita ya ubaguzi wa mtu mweusi.
 

Blood of Jesus

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
1,284
2,000
Kujua kilichowapata mababu zetu sio kitu kibaya. Historia ni historia tu. iite mbaya ama nzuri haijalishi.
 

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
5,958
2,000
Kujua kilichowapata mababu zetu sio kitu kibaya. Historia ni historia tu. iite mbaya ama nzuri haijalishi.
Shida yetu Hatuzintunzi hizi kumbukumbu mbaya kwaajili ya kuwaonyesha watoto na vizazi by, bali tunazitunza ili kuwaonyeshe watoto na wajukuu wa wazungu haohao ili watupe hela. Badala yake wanaendelea kutudharau wakishaona babu zao walivyotufanyia. Maana mtoto wa Mamba ni Mamba pia wanaendeleza usupriorty kwetu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom