Elections 2010 Tuziunge mkono posho za wabunge

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,159
4,443
Nimekuwa nikiona malalamiko mengi sana kuhusiana na posho za wabunge, mbona Tanzania kuna watumishi wengi tuu wa kawaida kabisa wanao pata wastani wa mishahara na posho zinazofika milioni12 na zaidi kwa mwezi, kwanini tunawaandama wabunge tuu? kwa ufahamu wangu wa kawaida kabisa shs12 kwa mwezi kwa mbunge ni pesa ya kawaida tuu. Mimi ni mjasiria mali wa kawaida kabisa na nina uwezo wa kutengeneza kiasi hicho cha pesa kila mwezi lakini sioni kama ninaweza kuishi maisha ya anasa. Plz M12 siyo pesa ya kumvalia njuga mbunge na kumkosesha raha.
 
Am not sure of what ure saing...............kumbuka watu wanaishi chini ya dola moja.Ndugu we waishi mjini, unaonekana unauwezo ila ndugu zetu wa vijijini wanahangaika....acha masihala ndugu yangu.
 
Unataka wale keki ya Taifa peke yao??
Kumbuka TZ ni miongoni ya nchi masikini duniani. Sasa mambo ya posho Sh. 12M kwa mwezi kwa wabunge, pesa za maendeleo zitatoka wapi??
 
Kuna haja kujua matumizi yao bse unapodish ela nyingi kwa hao watu maanake ni kuwa kuna watu wanaenda bungeni sio kutumikia wananchi bali kama project fulani ivi
 
Kuna haja kujua matumizi yao bse unapodish ela nyingi kwa hao watu maanake ni kuwa kuna watu wanaenda bungeni sio kutumikia wananchi bali kama project fulani ivi

Nakubaliana na wewe, kuna jamaa yangu alikuwa mbunge yeye alipoingia bungeni alifanya hesabu ya mapato akagundua atakuwa anapocket kila mwezi shs.7million kwa mwaka alipata shs( shs,7,000,000 x 12 =shs.84,000,000) kwa miaka 5 ni sawa na shs.420,000,000 alipata barua toka bunge ya kuthibitisha kipato hicho.Alichofanya alienda bank akaomba mkopo wa shs.280,000,000 payable in 5years na akapata akaenda kujenga hotel ya kisasa.Kwa hiyo hiyo ni project kabisa na concentration bungeni inakuwa ndogo kwani wengi wanakuwa wamefungua miradi mikubwa zaidi na hivyo wana-vest all human capital kwenye hiyo project badala ya kuwakilisha wananchi bungeni.
Piga panga posho ili concentration yao iwe bungeni
 
nimekuwa nikiona malalamiko mengi sana kuhusiana na posho za wabunge, mbona tanzania kuna watumishi wengi tuu wa kawaida kabisa wanao pata wastani wa mishahara na posho zinazofika milioni12 na zaidi kwa mwezi, kwanini tunawaandama wabunge tuu? Kwa ufahamu wangu wa kawaida kabisa shs12 kwa mwezi kwa mbunge ni pesa ya kawaida tuu. Mimi ni mjasiria mali wa kawaida kabisa na nina uwezo wa kutengeneza kiasi hicho cha pesa kila mwezi lakini sioni kama ninaweza kuishi maisha ya anasa. Plz m12 siyo pesa ya kumvalia njuga mbunge na kumkosesha raha.
umegombea nini?
Ulikopa pesa ya campaign, sasa unatakiwa urudishe ...
Ushaanza kuogopa na hizo zinapunguzwa hadi 3 m!
 
Back
Top Bottom