Tuweni makini wakati wa kuwapa watoto majina

sir mweli

JF-Expert Member
Feb 8, 2017
495
573
Hili limekuwa tatizo sasa, wazazi mnawapa watoto wenu mizigo bila kujua. Majina yana tabia ya ku-reflect tabia ya mhusika... Mfano mtu anaitwa mashaka, tabu, shida, mawazo,hatia,majuto.
Matokeo yake mtoto akiwa mbaya mnaanza kumlaumu kumbe shida ni nyie.

Mfano mtu anaitwa kilevi... Alafu unategemea awe na busara kweli.. Matokeo yake ndo haya mnakuja kuwapa watu shida buree.
Kuweni makini.

Updated:
Angalizo jingine : Msipende kuwapa watoto majina ya watu wengine eti kwa kuwaenzi, mfano mtu anampa mwanae jina la babu yake, bibi,mjomba,shangazi,mama au baba. Huwezi jua hao watu wana maagano gani humu duniani, ama wananadhiri gani walizokwisha ziweka au mikataba gani na wameekeana na nani. Matokeo yake unamrithisha mwanao majini, laana au hata vifungo bila hata kujua.
Ni ushauri tu... Hujalazimishwa kuukubali.
 
Mie mwanangu Wa kwanza nilitaka kumpa jina ",mapesa" yaani nilikuwa chuo nikapata field shirika lina hela lile jamani wanaofisi wakanipenda kila wiki ni night tu yaani singida babati mwanza kote huko napewa hela ya nguvu, Wa pili niliugua sana... Ila nilijifunza kusali kwa imani... Na kweli niliposali kwa imani nilifanikiwa kujifungua kawaida bila uchungu na ndani ya dakika 40.. Nikasema mungu yu nami tena ni mwaminifu mno mno...
 
Kuna utaratibu wa kisheria pale unapoona jina ulilopewa na wazazi wako waki wewe haujitambui ,na ukaona jina hilo limekuwa kero kwako, halikupendezi na linakuwa nuksi unaweza kujaza " DEED POOL " na ukasajili kwenye msajili wa hati. Hizo ni taratibu zipo watu wanafanya hivyo na wataendelea kufanya hivyo kwani jina sii mtu, ukilibadilisha bado utaendelea kuwa yuleyule ni sawa na kubadilisha nguo.
 
nasikia hata ile amri ya kuzuia viroba ilitokana na tabia ya watu kutumia jina la muheshimiwa vibaya hata mida ya kazi!
 
Mie mwanangu Wa kwanza nilitaka kumpa jina ",mapesa" yaani nilikuwa chuo nikapata field shirika lina hela lile jamani wanaofisi wakanipenda kila wiki ni night tu yaani singida babati mwanza kote huko napewa hela ya nguvu, Wa pili niliugua sana... Ila nilijifunza kusali kwa imani... Na kweli niliposali kwa imani nilifanikiwa kujifungua kawaida bila uchungu na ndani ya dakika 40.. Nikasema mungu yu nami tena ni mwaminifu mno mno...
Hata haueleweki!
 
Huu Uzi sitaweka comment kabisa, yaani umekaa kimtego sana!
Najuta hata kuufungua!
:rolleyes::rolleyes:
Woga wako tuu.... Wala haupo kwa ajili ya mtu flani... Ni kwa ajili ya jamii nzima kwani hili jambo lipo sana kwenye jamii... We hujaskia mtu anaitwa msiba
 
Ungekemea majina ya kizungu na kiarabu ungeonekana wa maana. Hata hayo ya kizungu mnayoitwa yana maana za namna hiyo. Na hakuna uhusiano wowote wa jina na tabia ama mafanikio ya mtu. Badili jina lako ujiite tajiri, watoto wako mmoja muite rais, waziri, balozi, mtakatifu, kadinali, nk. Halafu ungoje majibu.
 
Woga wako tuu.... Wala haupo kwa ajili ya mtu flani... Ni kwa ajili ya jamii nzima kwani hili jambo lipo sana kwenye jamii... We hujaskia mtu anaitwa msiba

Nimeishi naye street moja anaitwa "msiba" ila bonge la tajiri na ni hakimu.

"Ila naogopa huu Uzi!
 
Mie mwanangu Wa kwanza nilitaka kumpa jina ",mapesa" yaani nilikuwa chuo nikapata field shirika lina hela lile jamani wanaofisi wakanipenda kila wiki ni night tu yaani singida babati mwanza kote huko napewa hela ya nguvu, Wa pili niliugua sana... Ila nilijifunza kusali kwa imani... Na kweli niliposali kwa imani nilifanikiwa kujifungua kawaida bila uchungu na ndani ya dakika 40.. Nikasema mungu yu nami tena ni mwaminifu mno mno...

Mleta mada anaongelia jina la mtoto kuwa na effect kwa mtoto mwenyewe, sasa wewe unaongelea jina la mtoto kuleta effect kwa mzazi. Je, unaongezea kwa hypothesis nyingine au vipi?
 
Back
Top Bottom