Tuwekeze kwenye michezo na sanaa ili kupunguza matatizo ya ajira

Mkola Tz

Member
Sep 10, 2021
15
14
Kuwekeza kwenye michezo na Sanaa kunaweza kupunguza matatizo ya ukosefu wa ajira kwa vijana hapa nchini. Siku za hivi karibuni kumekua na ongezeko la matatizo ya ajira hapa nchini hii Ni kwa sababu tunaangalia sekta moja na kusahau zingine. Kwa mfano sekta ya michezo na sanaa. Sekta ya michezo na sanaa hapa nchini Ni Kama imesahaulika hii inachangiwa na mamlaka husika, serikali na wadau kwa ujumla kwa kusahau sekta hizi kubwa mbili ambazo zinaweza kutengeneza ajira nyingi Sana kwa jamii yetu.

Kiwanda cha michezo; michezo Ni kiwanda ambacho kinaweza kutengeneza ajira nyingi Sana kwa vijana. Kiwanda hiki Kama kitaangaliwa kwa jicho la pili na kupewa kipaumbele kitaweza kutengeneza ajira nyingi Sana kwa vijana wetu hapa nchini, kwa mfano mchezo wa mpira wa miguu umeajiri vijana wengi sana, wakike kwa wakiume kwani wamekua wakijipatia vipato kupitia mchezo huu. Hivyo Basi ongezeko la michezo mingine Kama mpira wa Pete, mpira wa kikapu, mpira wa mikono, kuogelea, ngumi, riadha, mbio za baiskeli n.k, michezo yote hii inaweza kuzalisha ajira nyingi Sana.

Sanaa Ni kiwanda; hiki pia Ni kiwanda ambacho kinaweza kutengeneza ajira nyingi Kama kitapewa kipaumbele Kama sekta zingine, Sanaa Kama muziki, maigizo, uchoraji na uchongaji inaweza kuwa chachu ya maendeleo makubwa hapa nchini kwa kutengeneza nafasi nyingi kwa vijana wetu. Hivyo Basi Kama tasnia hii ya Sana itapewa kipaumbele zaidi inaweza kuwa mkombozi wa changamoto nyingi kwa vijana.

Leo hii tumeona mapinduzi makubwa katika michezo kupitia soka(mpira wa miguu) na muziki. Hivyo Basi wizara husika, wadau wa Sanaa na michezo wanapaswa kutoa kipaumbele kwa sekta hizi mbili, kwani bajeti sahihi kutoka serikalini inatakiwa kupangwa, miundombinu Bora ya michezo na sanaa kutengenezwa na kuzalisha wakufunzi Bora wa michezo. Hayo yote yanaweza kuchangia maendeleo ya michezo na sanaa hapa nchini.
 
Back
Top Bottom