Tuwekeni wazi Watanzania, mauaji ya raia na mifugo mkoa Kagera - serikali ipo likizo?


Ishaka

Ishaka

Member
Joined
Nov 1, 2011
Messages
74
Points
95
Ishaka

Ishaka

Member
Joined Nov 1, 2011
74 95
Wana JF, jana usiku ITV walionyesha kipindi maalum kikiripoti matukio ya askari wanyama poli kuua raia na ng'ombe wao kwa risasi za moto kupokea rushwa, viongozi wa serikali za vijiji wilaya za Ngara na Biharamulo kutumia vibaya madaraka, kuuza maeneo ya wafugaji kwa wahamiaji haramu toka nchi jirani za Rwanda na Burundi, uharibifu mkubwa wa mazingira (misitu na tembo).....na mengi mengineyo ya kutisha!

Kipindi hiki kimebainisha kuhusika moja kwa moja kwa uongozi wa juu wa Wilaya husika ambao wamekuwa wakinufaika na janga hili la kitaifa. Katika mahojiano baina ya wananchi (waathirika) na mwandishi wa habari, inaonyesha wazi migogoro hii imeanza kitambo sana na hakuna hatua za makusudi zilizowahi kuchukuliwa kumaliza tatizo hili la wafugaji na askari wa misitu ya hifadhi, na wavamizi haramu wenye ng'ombe wengi toka nchi jirani sababu viongozi wanaonufaika na kashfa hii wamekuwa wakitumia nafasi zao kuzuia, kuwatisha na hata kuwabambikia kesi waandishi wa habari ili isijulikane kinachoendelea huku watu wakiteseka.


Je, amani na utulivu inayoimbwa katika majukwaa ya siasa ni ipi au mkoa wa Kagera si sehemu ya Tanzania? serikali iko wapi na kama si ustaarabu wa watu wa mkoa huu kuheshimu sheria za nchi hali ingekuwaje kule! Inawezekanaje mgeni auziwe pori la malisho ya mifugo ya wanavijiji na kusababisha migogoro baina ya wakulima na wafugaji - wauwane wenyewe kwa wenyewe kisha alindwe na mamlaka za serikali ya kijiji.

Mkoa wa kagera umekumbwa na maafa mengi sana kihistoria; Kwanza ukimwi, pili ajali ya meli ( MV Bukoba), tatu mnyauko (ugonjwa wa migomba), nne mzigo wa wakimbizi toka nchi za Rwanda na Burundi, tano Ujambazi wa kuteka mabasi kuua na kuiba mali kwa kutumia silaha nzito za kivita, sita Wimbi la watoto yatima vijijini na mjini, saba Umaskini uliokithiri tokana na yote yaliyotajwaa hapo juu

 
NINSIMA

NINSIMA

Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
8
Points
20
NINSIMA

NINSIMA

Member
Joined Apr 2, 2012
8 20
Watu wa mkoa wa Kagera wanapitia kipindi kigumu sana.Matukio yaliyoonyeshwa na Kipindi cha ripoti maalumu ITV yanatisha na kusikitisha kwani watanzania wenzetu wanaishi maisha ya hofu kama wakimbizi. Naishauri serikali kuliangalia suala hili kwa jicho la tofauti na tupewe taarifa ya hatua zitazochukuliwa kwa wahamiaji haramu na maofisa wanyama pori waoomba rushwa na kuuwa mifugo ya wafugaji.
 
C

Chief

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2006
Messages
1,765
Points
1,500
C

Chief

JF-Expert Member
Joined Jun 5, 2006
1,765 1,500
Kipindi cha jana cha ITV kimenisikitisha sana. Hivi serikali yetu haioni maovu hayo? Viongozi wa kijiji wanamilikisha raia wa Rwanda na Burundi ardhi ya Tanzania? Tumefika pabaya kweli.
 
C

cham

Member
Joined
Dec 20, 2011
Messages
24
Points
0
C

cham

Member
Joined Dec 20, 2011
24 0
Inasikitisha kuona mtanzania kiongozi wa leo kukumbatia wageni na kudhalilisha wananchi wenye nchi. Hawa wageni walikuwa wanaongea kana kwamba wana haki hata ya kulindwa na serikali ya Tanzania !! Watu wa ajabu kabisa. Ni vyema watimuliwe warudishwe kwao na mifugo yao na hao viongozi uchwara waliowawezesha hao wageni kutamba wakamatwe na kuhukumiwa bila huruma liwe funzo kwa viongozi wasio na maadili kama hao.
 

Forum statistics

Threads 1,284,356
Members 494,038
Posts 30,822,629
Top