Tuweke vyama pembeni, twendeni kwenye haki

chiefnyumbanitu

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
906
426
Tuwekeni vyama pembeni twendeni kwenye haki maana hata rais wetu tuliyempewa na Mungu anasema msema kweli ni mtu wa Mungu

Nape anakosa gani mpaka kutumbuliwa?Nape anakosa gani paka kushikiwa bastola na kuzaririshwa vile?

Nape si mwanachama mkubwa tu na ni mjumbe wa NEC ni kipi kilichohofiwa nape akiongea na wanahabari?

Ina maana mkuu wa mkoa ana umuhimu kuliko Nape? kwa nini wana CCM wasiungane kama walivoungana juzi vyombo vya habari na kuamua maamzi yao?

Tundu Lissu aliwahi kusema akimaliza kwetu atahamia kwenu sasa kama ndo hivi viwanda vitajengwa lini na vitaanza kazi lini?

MWISHO PAUL MAKONDA NI NANI NDANI YA WATANZANI AMBAO NI ZAIDI YA MILIONI 50, AMBAO WAMEPATA UHURU BILA KUMWAGA DAMU YEYE NI NANI?

Wazee wa taifa hili, maasikofu, vijana wenye busara, wasomi, wanasheria UKIMYA WENU UNALIGHALIMU TAIFA FUMBUWENI VINYWA VYENU.
 
Ni ivi mwenye macho aambiwi ona mwenye maskio aambiwi sikia dectator uchwara ndio alimtuma bwana zero kilicho bakia ni watanzania kuwa wamoja na kufanya maamuzi Unafiki mwiko
 
kuna maswali mengi sana hapa; kwanini RC hachunguzwi kwa tuhuma za vyeti? kwanini kitendo cha kuvamia station ya redio hakiongelewi hata na mkuu? kuna kitu hapa ni hiki kitakuwa kipimo cha uongozi uliopo sasa
 
Back
Top Bottom