Tuweke ushindani katika majina!

siyabonga

Senior Member
Jan 25, 2012
125
35
Wakuu, inawezekana hapa ikawa si jukwaa sahihi sana kwa hii post.

Lakini nimeiweka kwa kuwa naamini michezo ni siasa, na pengine wazo hili linaweza kuchukuliwa na kupelekwa sehemu sahihi: Timu zetu za Taifa, tuanza na wa miguu! Majina, ni mepese mno!

Kilimanjaro Stars! Jina hili maana yake ni finyu sana, halibebei dhana nzima ya Umuhimu na uzito wa mlima huu mrefu kuliko yote barani Afrika.

Nyota { Stars? } ziko kila mahali: Isitoshe, si wote kwa kutaja tu kilimanjaro wanapata picha ya kuwapo kwa mlima huo!

Kwa nini wasiitwe, say KILIMANJARO CLIMBERS?

Tazama hii, Serengeti ni mbuga kubwa na ina wanyama wengi! Timu unaiita : Serengeti Boys? Kwa nini?!!!!!

Pengine ingekuwa bora zaidi kuiita: SERENGETI GAME RANGERS!

Majina haya ya kubweteka betweka yanatufanya tunakosa ushindani, tunafungwa, watu wanacheke! Badili hivi vitu, jina hubeba maana!
 
Halow safi sana hiyo imetulia -mambo mengi bila shaka hupangwa masebuleni hapa kwetu ndo maana tunakuwa na majina ya ajabu ajabu.
 
Nakubaliana na Kilimanjaro Climbers. Kwa upande wa Serengeti sikubaliani na neno 'game' hii ni national park, labda timu ya vijana hao ingeitwa Serengeti Dwellers au Serengeti Wild Warriors au Serengeti Tour Guiders au Serengeti Beasts etc.
 
Back
Top Bottom