Tuweke rekodi sawa, Deo Mwanyika alihukumiwa kwa kukwepa kodi

Katiba inasema hivi ikiwa mtu ametiwa hatiani kwa kosa la kutolipa kodi ya serikali katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya uchaguzi atakuwa amekosa sifa.

Na hiyo mwanyika kwa kukubali hayo mashitaka ikiwemo la kukwepa kulipa kodi ya serikali maana yake ni kwamba ametiwa hatiani kwa kosa la kutolipa kodi ya serikali,
Weka ushahidi wa hiyo hukumu.
 
Weka ushahidi wa hiyo hukumu.
Kakiri kosa, na sio hukumu ni agreement yake na DPP
Sina hiyo hukumu labda niutafute lakini fact ni kwamba kaachiwa baadaye ya kukiri kosa la kukwepa kulipa kodi ya serikali
 
Katiba Ni sheria mama.Lakini huyu Mwanyika alikuwa hajatiwa hatiani na mahakama.Labda hapo ndo pona yake

..amehukumiwa.

..plea deal maana yake ni kukubali makosa, kukubali kwamba una hatia.

..na plea-deal lazima iidhinishwe na hakimu na isajiliwe mahakamani.
 
Kitu kizuri ni kuwa kuna mtu kamuwekea pingamizi; kwa maana hiyo basi, Tume watatoa sababu kwa nini jina litakatwa au litaendelea kuwepo. Kikubwa hii issue inafanya watu wajiulize mara mbili kuhusu dhamira ya Magufuli ya kupambana na rushwa. Kama mtu amekiri kukwepa kodi kwa nini anachaguliwa kugombea ubunge?
 
FYI hakuhukumiwa kwa hiyo katiba haiingii hapo. Soma vizuri kilichoandikwa ndio sababu wakaita plea bargain. Unarekebisha mambo na unaondoka msafi mahakamani ie huna doa. (Why, kwa sababu ile kodi aliyokuwa anataka kukwepa umekubali kuilipa ie 1.5 billion). Simple as that! Kila mtu anaendelea na maisha yake na if I am not mistaken kuna period unapewa usirudie huo nchezo. Re: Kabendera saga, si na yeye alilipa na kaondoka msafi anaendelea na maisha yake bali asirudie tena. (I presume kuna kipindi wanapewa kutokurudia).
Acha kujitoa ufahamu eti ili mradi tu uweze kutetea udhalimu wa wa serikali na chama chako! Unatoka vipi msafi wakati umeshakiri kosa?!

Ukishakiri kosa, hapo tayari una hatia, na hiyo kulipa ni kutumikia adhabu ya hatia yako!

Sio hivyo tu, hata kwa mujibu wa sheria zetu, in particular, The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Act, tena ya mwaka 2019, Ibara ya 15 (b) inasema:-
“plea bargaining” means a negotiation in a criminal case between a prosecutor and the accused whereby the accused agrees to-
(a) plead guilty to a particular offence or a lesser offence or to a particular count or counts in a charge with multiple counts; or
(b) cooperate with the prosecutor in the provision of information that may lead to a discovery of other information relating to the offence or count charged, in return for concession from the prosecutor which may lead to a lenient sentence or withdrawal of other counts."
Utaona hapo sheria inasema wazi the accused agrres to plead guilty!

Na sheria hiyo inasema, hayo yote yakishafanyika, Plea Agreement inasajiriwa na mahakama!!

Sasa Mtuhumiwa anayekiri kosa anaondokaje akiwa msafi?!

Na kwa mujibu wa mleta mada, Deo Mwanyika alikiri kosa la ukwepaji kodi na ndio maana akalipishwa hicho kiwango! Na kwa mujibu wa sheria husika, unapo-plea guilty through plea bargaining, kinachofanyika ni kufutwa tu baadhi tu ya makosa au yote EXCEPT lile ulilokiri!

Na kwa mujibu wa katiba pamoja na sheria zetu, one of the greatest crime kwa Kiongozi wa Umma ni suala la ukwepaji kodi, na ndio maana, kwa mujibu wa katiba, Ibara ya 67(1)(c) inasema:-
Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge endapo katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi hakuwahi kutiwa hatiani katika mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali
And remember, according to sheria ya plea gargaining hapo juu, Ibara ya 194D (4) (b) inasema:-Where the court accepts a plea agreement; the agreement shall become part of the record of the court.

Na 194D (5) inasema:- Where a plea agreement entered into in accordance with sections 194A and 194B is accepted by the court, the court shall proceed to convict an accused person accordingly.

Kwa maana nyingine, hapo issue yake inakuwa tu imefanyika nje ya mahamakama but technically, anakuwa convicted!!

Remember, plea bargaining ya criminal case and not civil case.
 
..sasa kwanini na wewe usitupatie ushahidi usio na shaka ku-clear doubts tulizonazo?
Mkuu hoja zangu zipo wazi, uzi huu ulisema ameruhusiwa kugombea Ubunge ingawaje yeye ana makosa ya kutolipa kodi aliyohukumiwa na mahakama. Mimi nikauliza na kuwaambia mnafahamu maana ya plea bargain?..
Kakiri kosa, na sio hukumu ni agreement yake na DPP
Sina hiyo hukumu labda niutafute lakini fact ni kwamba kaachiwa baadaye ya kukiri kosa la kukwepa kulipa kodi ya serikali.
So, what is your point? Do you know what is being argued?

..amehukumiwa.

..plea deal maana yake ni kukubali makosa, kukubali kwamba una hatia.

..na plea-deal lazima iidhinishwe na hakimu na isajiliwe mahakamani.
..... NC

....... Unakubali kwamba una hatia, lakini hatia hiyo ni lazima iwe recorded according to the law (Plea bargain).

... Absolutely right.
 
Kitu kizuri ni kuwa kuna mtu kamuwekea pingamizi; kwa maana hiyo basi, Tume watatoa sababu kwa nini jina litakatwa au litaendelea kuwepo. Kikubwa hii issue inafanya watu wajiulize mara mbili kuhusu dhamira ya Magufuli ya kupambana na rushwa. Kama mtu amekiri kukwepa kodi kwa nini anachaguliwa kugombea ubunge?
Sheria zipo wazi na sio JPM kazi yake kuzitafsiri, mimi nilisema CCM sio wajinga wanafahamu wanavyofanya, sasa nyie kama mna ushahidi sheria zimevunjwa, si muende mahakamani mnangoja nini? Huko ndio kwenye suluhisho.

BTW nimeona CHADEMA wanalialia kutaka Diplomats wawasaidie wagombea wao walioshindwa kutimiza masharti. Sasa kama sio wendawazimu huo ni nini? Chadema si ndio walikuwa mstari wa mbele kutaka JPM asigombee kwa kutotimiza masharti? Hatukusikia kelele za hao wahamiaji? Waliwasha moto sasa hawawezi kuuzima.
 
Mkuu hoja zangu zipo wazi, uzi huu ulisema ameruhusiwa kugombea Ubunge ingawaje yeye ana makosa ya kutolipa kodi aliyohukumiwa na mahakama. Mimi nikauliza na kuwaambia mnafahamu maana ya plea bargain? Wote mkaanza kuokoteza ushahidi hadi tulipofika kwamba huwa kuna Agreement kati ya DPP na mshitakiwaji...

..angalau sisi tumekuwekea sheria inavyosema.

..kwamba plea-bargain ni kukubali makosa, na kwamba mshtakiwa ana hatia.

..ila wewe mwenzetu hoja yako ni kwamba kamati ya kuu ya ccm inajua sana kuliko kila mtu kwa hivyo tusiihoji.
 
..angalau sisi tumekuwekea sheria inavyosema.

..kwamba plea-bargain ni kukubali makosa, na kwamba mshtakiwa ana hatia.

..ila wewe mwenzetu hoja yako ni kwamba kamati ya kuu ya ccm inajua sana kuliko kila mtu kwa hivyo tusiihoji.
Sasa kama huna hiyo agreement utafahamu vipi kilicho ndani? Ndio majungu yenyewe. Leta ushahidi kama huna kaa kimya.
 
Serikali hii ni ya wahalifu.. wapo tayari kufa kwa kulinda uhalifu.
Huyu ni mhalifu aliye kubuhu na alikiri hadharani kui snitch nchi, alitakiwa sio kutimuliwa kwenye kugombea ubunge tuu bali kutandikwa mawe adi afe
 
Sheria zipo wazi na sio JPM kazi yake kuzitafsiri, mimi nilisema CCM sio wajinga wanafahamu wanavyofanya, sasa nyie kama mna ushahidi sheria zimevunjwa, si muende mahakamani mnangoja nini? Huko ndio kwenye suluhisho...
Kuhusu suala la jpm ccm mlikosea kabisa kumshauri hilo liko wazi
Kuhusu kwenda mahakamani kuhusiana na uamuzi wa suala la jpm hilo haliwezekani kwa sababu decision ya tume ndiyo final
 
Angekuwa mpinzani tu tayari ashaenguliwa ila kwasababu anayesema kakomesha rushwa ndiye kamptisha basi tume macho kodo
 
Angekuwa mpinzani tu tayari ashaenguliwa ila kwasababu anayesema kakomesha rushwa ndiye kamptisha basi tume macho kodo
 
Kuhusu suala la jpm ccm mlikosea kabisa kumshauri hilo liko wazi
Kuhusu kwenda mahakamani kuhusiana na uamuzi wa suala la jpm hilo haliwezekani kwa sababu decision ya tume ndiyo final
Mkuu sasa si ukawaambie CCM maoni yako? Sheria zenyewe hufahamu umebaki kulalama tu.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom