Tuweke rekodi sawa: CUF iligoma kushirikiana na CDM katika kambi ya upinzani bungeni...

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,178
7,319
Ni miaka miaka miwili na nusu tu, lakini baadhi ya watu wanaanza kusahau. Sasa imekuwa kawaida kusikia baadhi ya watu wakisema kuwa CHADEMA iligoma kuishirikisha CUF kwenye kambi rasmi ya upinzani bungeni. Hii sio sawa na ni lazima tukumbushane au tuwaonyeshe kuwa hatujasahau...

Wakati bunge linaanza mwaka 2010, uongozi wa CHADEMA ukiongozwa na Mbowe walifanya juhudi kubwa sana za kuvitaka vyama vyote vya upinzani waungane ili waunde kambi rasmi ya upinzani bungeni. NCCR waligoma kutokana na mgogoro wa kisiasa ulioibuka kati ya mwenyekiti wao Mbatia na Mdee katika kampeni za ubunge Kawe, na Mbatia alikataa suluhu na kulipeleka suala lile mahakamani. TLP na UDP nao waliungana na NCCR.

CHADEMA haikuwa na jinsi zaidi ya kuiapproach CUF wakiamini kwamba kama chama cha tatu kwa ukubwa bungeni, wangekubali kishiriki katika kambi ile. CHADEMA wakiongozwa na Mbowe na CUF wakiongozwa na Hamad Rashid, walifanya majadiliano marefu lakini kwa masikitiko ya wengi CUF walikataa, wakishikilia msimamo kuwa CDM watafute suluhu kwanza na NCCR kama walitaka kushirikiana na CUF katika upinzani.

Huku NCCR waking'ang'ania mahakamani, na CUF wakilazimisha suluhu kwanza kati ya CHADEMA na NCCR, CHADEMA hawakuwa na jinsi zaidi ya kuunda kambi rasmi ya upinzani bungeni, huku Mbowe akiahidi kuwa pale wenzao watakapokuwa tayari basi watashiriki katika kambi rasmi ya upinzani bungeni.

CUF wakati huo wakiwa wametoka katika mashamsham ya mahusiano yao mapya na CCM huko Zanzibar, waliwaongoza NCCR, TLP na UDP kuungana na CCM na kubadilisha vifungu vya kanuni za bunge ili kuinyima CHADEMA mandate ya kuongoza zile kamati tatu za bunge.

Leo hii baada ya kugundua kuwa mshirika wao CCM hana nia njema nao, CUF wanatembea barabarani wakiilaumu CHADEMA kwa kukataa kuishirikisha kwenye kambi rasmi ya upinzani!!!

Mi nawashauiri warudi hukohuko kwa mshirika mwenzao, wakae wayamalize mambo yao ya ndani hayo. CHADEMA ilishasonga mbele na haihitaji tena msaada wenu, kwani kwa miaka miwili na nusu hii sapoti iliyopata kutoka kwa nguvu ya umma inatosha kuwawezesha kutetea rasilimali za nchi hii kwa nafasi yao...
 
Hii ndio tanzania, naomba ifahamike kuwa upinzan makin hujengwa kwa hoja dhidi ya serikali, sasa cuf si wameungana na ccm? Hao sio wapinzan,hata kama ni visiwan tu,lakin ni cuf ileile,wanajadil mambo na ccm then waje wajadil na vyama vingine kama cdm, hailet logic kwan siku zote upinzan unahitaji kukua kwa kuikosoa serikali, na kuwaonesha altenative way wananchi sasa cuf wamkosoe nani? Wakat wako ndan? Ni bora kuwapa tlp,nccr m. N.k kuongoza kambi kuliko kuongelea suala la cuf kutengwa,hao wamejitenga,nawashauri ili wawe wapinzan wavunje ndoa.
 
Mkuu Tuko, Mungu amepishilia mbali kuungana maana si unajua CUF ni WALIBERALI?
 
Last edited by a moderator:
Chama cha upinzani tz ni CDM pekee.Hawa akina TLP,UDP,CUF,etc. ni matawi ya CCM.
 
Nakumbuka walianzisha kambi yao isiyorasmi pembeni spika akaipiga chini.
 
CUF sio chama cha Upinzani cha UKweli.Lengo lao ni kutaka kuvuruga Wapigakura tu.Mwone Maalim Seif,yeye anahubiri Ubaguzi dhidi ya Watanganyika lakini kila Siku Kiguu na njia kuja Tanganyika.Ni Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar lakini analalamika sawa na Tambwe Hiza.Hana uwajibikaji wa pamoja na Viongozi wenzake Serikalini wala kutoa Maelekezo kwa wananchi kama Kiongozi.Mwone Prof.Lipumba,Kucha kutwa kiguu na njia Misikitini kuhubiri UDINI.Watu wenye malengo ya aina hii hawawezi katu kuungana na chama chochote Makini.
 
....Kwa mara ya mwisho kumsikia Nape au Kinana anataja CUF, au NCCR au TLP au UDP ni lini? hata Mh Rais nadhani ameitaja NCCR kwa mara ya mwisho alipomteua Mbatia kuwa mbunge viti maalum. Kuna sekunde hata moja inaweza kupita bila Nape na Kinana kuifikiria au kuitaja CHADEMA?
CHADEMA ni mpango wa Mungu! kujiunga na akina CUF, NCCR, TLP, UDP nk ni kuuchakachua mpango wa Mungu, na Mungu hakutaka mpango wake uchakachuliwe. Ndio maana hata akina Mbowe walipojitahidi Mwenyezi Mungu alipishilia mbali.
 
ya kale dhahabu....mwanadamu katika akili yake aliwekewa kipengele kiitwacho"sahau"na mpaka wazee wetu wakaja na kamsemo,"tusahau yaliyopita tugange yajayo"na wakati mwingine unakuta yaliyopita yalikuwa muhimu zaidi kuliko yajayo,all in all cuf wapesi wakusahau na kupanic wanapoambiwa ukweli
 
Back
Top Bottom