Tuweke kumbukumbu zetu sawa, huu ndo uchumi wa Magufuli aliouacha, all facts! - Sehemu ya kwanza

Habarini wakuu…

Wakati bado tukiwa kwenye maombolezo, nimeona ni vema nifanye utafiti kidogo wa kumulika uchumi wa Hayati Magufuli, ili tuweke record zetu sawa, maana huku mtaani na kwenye vyombo vya habari kumekuwa na upotoshaji mkubwa sana.

Japo mimi sijawahi kuwa mshabiki wa Hayati Magufuli, ila leo ntajaribu kuwa objective sana, kwa faida ya watu wa pande zote mbili, wale wanaoponda na wala wanaosifia. Nataka tufike kwenye mizania ya kujua ukweli wa Magufuli, ili kama mtu unasifia ujue unasifia kitu gani na kama unaponda ujue unaponda kitu gani.

Leo ntagusia viashiria vichache ambavyo vinanguvu katika uchumi wa nchi yeyote. Na viashiria hivo vina uhusiano wa viwakilishi kwenye kanuni ya kutafuta zao la nchi yaani GDP.

(GDP = Consumption + Investment + Government Spending + Net export)

Viashiria ambavyo ntaviangalia ni hivi vifuatavyo

1) Credit growth (Ukuaji wa mikopo inayotolewa na benki za kibiashara) – Hiki kiashiria kinawakilisha performance ya sekta binafsi kwenye uwekezaji, ukuaji wa mzunguko wa pesa, private sector confidence, performance ya mabenki ya kibiashara, na pia ni kiashiria cha consumption. Unapokuwa na declining trend, kwenye credit growth maana yake hayo mambo yote niliyoyataja lazima yawe negatively affected.

Ni nini kina determine credit growth? (Ama ni nini kisababishi cha ukuaji wa mikopo kwenye mabenki ya kibiashara kwa sekta binafsi?) – Nadhani hichi ni kitendawili ambacho Hayati Magufuli na wanaomzunguka wameshindwa kukijibu kwa miaka karibu sita aliyokuwa madarakani.

Asilimia karibu 65% mpaka 75% ya uchumi wa Tanzania upo determined na sekta binafsi, na hiyo inayobaki 25% mpaka 35% ndo sekta ambayo ni government nikimaanisha ile sekta inayohusu ukusanyaji wa mapato na bejeti ya nchi.

Utawala wa Magufuli, ulikuja na uwekezaji na matumizi makubwa kwenye projects kama Kununua Ndege, Ujenzi wa flyovers, Ujenzi wa Madaraja, Ujenzi wa Makao Makuu Dodoma, Ujezi wa Bwawa la Umeme, Ujenzi wa SGR na vinginevyo. Kwa ufupi naweza kukadiria kwamba, kwa miaka 6 iliyopita kuna Trillioni 40 mpaka 60 ambazo zilienda kwenye hizi projects za utawala Magufuli. Binafsi sina tatizo na hii approach ya Magufuli kwenye miundo mbinu, kwanza ntazidi kumsifu kwenye hili suala.

Tatizo kubwa ambalo nililiona na ambalo ndo kitendawili alichoshindwa kukijibu Magufuli na utawala wake ni kwamba, mipango ya kutekeleza hii miradi haikuangalia uwezo halisi wa nchi wa kutengeneza mapato ya ku finance hii miradi ambayo ilihitaj kiasi kikubwa cha pesa na rasilimali za viwandani.

Matokeo yake, serikali ya Magufuli ikajikuta ipo kwenye stress kubwa ya kupata pesa za ku finance hii miradi ya mapesa mengi. Kwa hiyo option zilikuwa ni mbili 1) Aaache kutekeleza hii miradi ya mepesa mengi au 2) Afanye kila njia kupata pesa.

Haiba ya Magufuli ilimfanya atumie njia namba mbili ‘Kutafuta pesa kwa gharama yeyote’. Nadhani hii njia ndo imefanya mpaka leo tuna vilio kwa wafanyabiashara, wawekezaji, wafanyakazi, mabenki, kwa sababu hii njia ilikuja na action zifuatazo za kutafuta pesa.

a) Kikosi kazi cha kukusanya kodi – Fairness kwenye mfumo wa kodi ilipotea, hakukua na logic tena, naweza sema kwa miaka sita iliyopita nchi ilikuwa kwenye ‘Unyang’anyi wa kodi’ na sio ‘Ukusanyaji wa kodi’. Madam President ameongea vema sana jana kuhusu hichi kitu. Hichi ndio kikubwa ambacho kimeua confidence ya sekta binafsi, matokeo yake ikaathiri mzunguko wa pesa kwenye uchumi, kwasababu kumbuka sekta binafsi ndio haswa wateja wa mabenki ya kibiashara. Kwa kuthibitisha hilo angalia trend ya utoaji mikopo kuanzia mwaka 2010 enzi ya kikwete mpaka 2020. Enzi ya Kikwete sekta binafsi ilikuwa inakuwa kwa kasi sana n ahata unaweza kuona trend ya utoaji wa mikopo ambayo ilikuwa ni kwa wastani wa asilimia Zaidi ya 13% wakati ukuaji wa mikopo kwenye utawala wa Magufuli ni wastani wa asilimia 5.6% kwa miaka mitano iliyopita. So unaweza kuona ni kwa namna gani sera ya Magufuli kwenye kodi ilivoua sekta binafsi na ukuaji wa mikopo.

View attachment 1741641

View attachment 1741642

Kwa kuangalia data za ongezeko la ukusanyaji wa mapato kwa miaka 10 iliyopita pamoja na ongezeko la utoaji mikopo kwa sekta binafsi kama zilivo hapo juu, tunaweza kuwa na conclusion zifuatazo kuhusu uchumi wa Magufuli dhidi ya watangulizi wake.

  • Kwa miaka mitano ya mwisho ya utawala wa Kikwete, kwa ujumla aliweza kuongeza kodi kwa karibu asilimia 88% kwa kuangalia kodi iliyokusanywa 2011 na ile iliyokusanywa 2015, wakati huo huo, sekta binafsi ilikuwa ikifanya vizuri kwa kuangalia uwiano wa mikopo na zao ghafi la ndani, ilikuwa ikipanda kutoka 12.21% mwaka 2011 mpaka 14.47% mwaka 2015 alipotoka madarakani. (Key note: Utawala wa Kikwete uliweza kuongeza makusanyo ya kodi mwaka hadi mwaka, na wakati huo huo sekta binafsi ilikuwa inamea mwaka hadi mwaka – Economically hii ndio tunaiita positive
  • Kwa miaka mine ya Magufuli 2016 – 2019 (sikuweza kupata data za 2020), kwa ujumla aliweza kuongeza makusanyo ya kodi kwa asilimia 56% ndani ya miaka minne 2016 -2019, wakati huo huo mikopo kwa sekta binafsi ilianza kudorora kwa kuangalia uwiano wa mikopo na GDP ambao kwa miaka hiyo minne imekuwa ikienda chini kutoka ile peak iliyofikiwa na utawala wa kikwete ya 14.47% mwaka 2015 mpaka 12.05% mwaka 2019. Hii ki uchumi tunaiita growth ambayo ni negative, yaani GDP inakuwa lakini sekta ya mikopo inadorora, na unaweza kuona ni kipindi hichi hichi nchi ilikuwa na sera za kodi za unyang’anyi.

b) Kutokuongeza mishahara ya watumishi wa umma – ilikuwa pia ni lazima utawala wa Magufuli ufanye hichi kitu ambacho is unfair, kwa minajili ya kulinda pesa za kufanya miradi. Kwa miaka sita iliyopita, kipato cha mfanyakazi kimeporomoka karibu kwa asilimia 18% kutokana na kupanda kwa gharama za maisha na serikali kushindwa kuongeza mishahara.

c) Kuzuia fao la kujitoa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii – ambacho wengi hawajui ni kwamba katika harakati za kutafuta pesa za miradi, utawala wa magufuli ndani ya miaka 6, wamekopa Zaidi ya Trillioni 12 kwenye hii mifuko ya hifadhi ya jamii, kitu ambacho kimepelekea hii mifuko kuwa ni kama imefilisika na ndio maana ikabidi wazuie fao la kujitoa kwasababu mifuko imekaushwa na serikali.

d) Kukua kwa haraka kwa deni la serikali (madeni ya nje na ndani) – Hii ndo ilikuwa karata ya mwisho ya kupata pesa, kwa sababu njia zote tatu hapo juu ni kama hazikuzaa matunda. (Ntaelezea kwa mapana hichi kitu nyuzi zinazofuata)

Hayo ni baadhi ya mambo yaliyotokea kama sera za uchumi wa Magufuli ambao ntaendelea kuuchambua, ila kwanza nataka mnielewe taratibu ili tuweze kwenda sawa.

Kwa wale ambao wana mashaka na uchambuzi wangu kuhusu masuala ya kiuchumi naomba mpitie baadhi ya nyuzi zangu ambazo niliwahi kuandika kipindi cha nyuma na ambazo zitahusika moja kwa moja na uchambuzi kuhusu uchumi wa Magufuli. Naahidi kuwaletea vipande vipande na hoja chache chache ili msije kuchanganyikiwa na rundo la taarifa.

-----------------------------------------------------------------------------------------------------
1. Ukali wa maisha kwa watanzania - Serikali tafakarini kuongeza mishahara ya Watumishi wa Umma, ukali wa maisha ni bomu linaloua taratibu!

2. Kuadimika kwa saruji nchini - Serikali haiwezi kukwepa lawama ya kuadimika na kupanda kwa bei ya Saruji nchini. Waziri wa Viwanda ana kazi sana, kuna janga linatunyemelea

3. Uchumi bado upo kwenye mkwamo - ‘Namba zinanuka’ – kwanini nasema bado uchumi wetu upo kwenye mkwamo?

4. Serikali imedumaza mifuko ya hifadhi ya jamii - ‘Namba zinanuka’ – Serikali imechangia kudumaza mifuko ya Hifadhi ya Jamii

5. Uchumi wetu ni dhaifu - USHAHIDI: IMF hawajakosea, Uchumi wetu ni ‘DHAIFU’
Narrow view
 
Siwezi kuuelewa huu uchambuzi unless uniambie kwa nini viwanda vingi abavyo ni vya binasfsi na serikali vilikufa awamu zilizopita na vilianza fufuka awamu ya JPM. Swali lingine kama hali ilikuwa mbaya ya kiuchumi kwa nini tuliingia uchumi wa kati?

Wana wa Israeli walipokuwa wanatoka Misri kwenda Kanani walipitia misukosuko ya kila aina njiani, ilifika mahali wakaanza kumlamu Musa wakisema ni heri warudi kule walipotoka. Kwangu mimi Magufuli ataendelea kuwa Rais bora kuwahi kumshuhudia katika maisha yangu, kwasababu ya ujasiri wake hasa kwenye kutujengea misingi ya nchi yenye uchumi endelevevu kwa siku zijazo.

Kupanga ni kuchagua na ili kufikia maendeleo ya kweli lazima kuna kizazi kijotoe sadaka kwa ajili ya wengine. Wakiloni walivamia Afrika miaka hiyo bila kujali wanyama wakali na magonjwa wakachukua dhahabu na almasi wakaenda jenga nchi zao, leo wajukuu zao wanakula matunda ya jasho la mababu zao.

Ni kweli JPM hakuongeza mishahara na alitoa fao la kujitoa, aliongeza makato kwa wanufaika wa bodi ya mkopo nk, lakini wanachi tulimuelewa nia ya yake, sababu matokeo yake tuliyaona kila tulipo safiri ndani ya nchi hii.

Miradi mikubwa mikubwa kama SGR Dar to Moro takriban 7trill, Nyerere george 6.9trill, Daraja la busis 6.9bill zahanati, vituo vya afya na hospitali za rufaa kila mkoa, masoko na basi stend kila mkoa, ujenzi wa meli ziwa Victoria, Nyasa na Tanganyika, vyote hivi vilihitaji pesa. Kwa akili ya kwaida ukifikiria miradi mingi, ukiacha reli ya SGR ilikuwa inakamilika kabla ya 2024 na ndio maana hayat Rais Magufuli aliwaasa wafanyakazi wawe wazalendo na kwamba angeongeza mshahara kabla hajamaliza muda wake.

Miradi hii mikubwa aliyoianzisha JPM ndio ingeongeza ukusanyaji wa kodi kwa siku za mbeleni na ndio ikafanya nchi iweze kujitegemea. Narudia tena kusema Rais Magufuli alikuwa ni kiongozi mwenye maono makubwa sana tulichewa kumpata, tulipompata hajadumu. katuachia dira ya maendeleo ya taifa ambayo tukiifuata taifa linakwenda kujitegemea kwa kipindi kifupi.

Siku zote unapotatua matatizo kwa watu wengine unaweza kusababisha matatizo kwa wengine, hatotokea kamwe kiongozi atayewarisha wote. R.I.P JPM.
ndugu. huwezi kuitwa baba mzuri kwa kulisha watoto wako mlo mmoja eti unajenga nyumba nzuri waishi vizuri baadae. kila kitu tufanyacho lazma tukuwe na kias. mtoa mada hajaipinga miradi bali sera ya miradi yenyewe hesab zake ndo zimekuwa na side effects kubwa. kifua chetu kama nchi kilikuwa kidogo. hata mzee nyerere alipapenda dodoma lakin akapima kifua. hata roma haikujengwa kwa siku moja. nashawishika kusema jpm aliipenda hii mirad mikubwa akiwa na nia ovu! huwezi kutenda wema kwa kuvunja sheria, kanuni na taratibu!
 
Fungua macho utazame,

1. Unasema enzi ya JK pesa ilikuwa ni haramu, naomba ufafanue kivipi? wakati watu walikuwa wanafanya kazi na kupata pesa, kwani kipindi cha JK pesa zilikuwa zinagawiwa bure? Kwanini useme eti zilikuwa za haramu?

2. Yaani wewe uchumi kudorora, mzunguko wa pesa haupo ndo unasema huo kwako ndo uchumi halisi? Kuwa serious mkuu.. fungua macho utazame tena kauli yako.
Kwa JK watu walikuwa wakifanya kazi gani? wakati vijana wengi waligezwa mapunda ya kubeba unga, biashara haramu ilishamili enzi za Jk mpaka kuuza viungo vya arubino,kwenye builder Cheng ndio usiseme watu walikuwa wakifa fojali ya kuhalibu shiling yetu,toka Magufuri ameingia madarakani mbona hatusiki dora kupanda? Magufuri alikuwa kiboko wa Mafisadi na wazembe ni hilo tu.
 
Kuna watu wanatamani wakanushe ila sasa bandiko linaongea kwa takwimu na vithibitisho, yaani mkanushaji inabidi aje na data zake naye tumsikie, hii ngumu kumeza baba
 
Watu hawataki tu kusema ukweli, JPM alipenda miradi mikubwa ya ujenzi kwa kuwa huko kwenye miradi ya ujenzi ndipo Kuna ulaji wa bila kugutukiwa na ndo sababu ya JPM kutomtoa Mfugale Tanroads wanajua walivyokuwa wanapiga deal. Mimi binafsi sikuwahi kumkubali JPM kabisa. Alijivika Umungu mtu, katuharibia uchumi wetu, watu pekee wanaomsifu ni wanufaika wake. Hakuwa na quality za kiuongozi kabisa mfano hai ni jinsi alivyokuwa anatumbua watu majukwaani ili mradi tu ashangiliwe na wananchi . Unabania wafanyakazi kwa kisingizio cha kubana matumizi wakati yeye anasafiri kutoka chato mpaka dsm kwa msafara wa Ma V8 zaidi ya hamsini, kwanini asipande ndege kupunguza matumizi yasiyo ya lazima?.
 
Watu hawatski tu kusema ukweli, JPM alipenda miradi mi kubwa ya ujenzi kwa kuwa huko kwenye miradi ya ujenzi ndipo Kuna ulaji wa bila kugutukiwa na ndo sababu ya JPM kutomtoa Mfugale Tanroads wanajua walivyokuwa wanapiga deal. Mimi binafsi sikuwahi kumkubali JPM kabisa. Alijivika Umungu mtu, katuharibia uchumi wetu, watu pekee wanaomsifu ni wanafaika wake. Hakuwa na quality za kiuongozi kabisa mfano hai ni hindi alivyokuwa anatumbua watu majukwaani ili mradi tu ashangiliwe na wananchi . Unabania wafanyakazi kwa kisingizio cha kubana matumizi wakati yeye anasafiri kutoka chato mpaka dsm kwa msafara wa Ma V8 zaidi ya hamsini, kwanini asipande ndege kupunguza matumizi yasiyo ya lazima?.
Sijui anajisikiaje huko kaburini. Miaka 6 ya utawala wake amewanyima watumishi wenzake wa umma nyongeza ya mshahara.
 
Watu hawatski tu kusema ukweli, JPM alipenda miradi mi kubwa ya ujenzi kwa kuwa huko kwenye miradi ya ujenzi ndipo Kuna ulaji wa bila kugutukiwa na ndo sababu ya JPM kutomtoa Mfugale Tanroads wanajua walivyokuwa wanapiga deal. Mimi binafsi sikuwahi kumkubali JPM kabisa. Alijivika Umungu mtu, katuharibia uchumi wetu, watu pekee wanaomsifu ni wanafaika wake. Hakuwa na quality za kiuongozi kabisa mfano hai ni hindi alivyokuwa anatumbua watu majukwaani ili mradi tu ashangiliwe na wananchi . Unabania wafanyakazi kwa kisingizio cha kubana matumizi wakati yeye anasafiri kutoka chato mpaka dsm kwa msafara wa Ma V8 zaidi ya hamsini, kwanini asipande ndege kupunguza matumizi yasiyo ya lazima?.
Upo sahihi kabisa.
 
Siwezi kuuelewa huu uchambuzi unless uniambie kwa nini viwanda vingi abavyo ni vya binasfsi na serikali vilikufa awamu zilizopita na vilianza fufuka awamu ya JPM. Swali lingine kama hali ilikuwa mbaya ya kiuchumi kwa nini tuliingia uchumi wa kati?

Wana wa Israeli walipokuwa wanatoka Misri kwenda Kanani walipitia misukosuko ya kila aina njiani, ilifika mahali wakaanza kumlamu Musa wakisema ni heri warudi kule walipotoka. Kwangu mimi Magufuli ataendelea kuwa Rais bora kuwahi kumshuhudia katika maisha yangu, kwasababu ya ujasiri wake hasa kwenye kutujengea misingi ya nchi yenye uchumi endelevevu kwa siku zijazo.

Kupanga ni kuchagua na ili kufikia maendeleo ya kweli lazima kuna kizazi kijotoe sadaka kwa ajili ya wengine. Wakiloni walivamia Afrika miaka hiyo bila kujali wanyama wakali na magonjwa wakachukua dhahabu na almasi wakaenda jenga nchi zao, leo wajukuu zao wanakula matunda ya jasho la mababu zao.

Ni kweli JPM hakuongeza mishahara na alitoa fao la kujitoa, aliongeza makato kwa wanufaika wa bodi ya mkopo nk, lakini wanachi tulimuelewa nia ya yake, sababu matokeo yake tuliyaona kila tulipo safiri ndani ya nchi hii.

Miradi mikubwa mikubwa kama SGR Dar to Moro takriban 7trill, Nyerere george 6.9trill, Daraja la busis 6.9bill zahanati, vituo vya afya na hospitali za rufaa kila mkoa, masoko na basi stend kila mkoa, ujenzi wa meli ziwa Victoria, Nyasa na Tanganyika, vyote hivi vilihitaji pesa. Kwa akili ya kwaida ukifikiria miradi mingi, ukiacha reli ya SGR ilikuwa inakamilika kabla ya 2024 na ndio maana hayat Rais Magufuli aliwaasa wafanyakazi wawe wazalendo na kwamba angeongeza mshahara kabla hajamaliza muda wake.

Miradi hii mikubwa aliyoianzisha JPM ndio ingeongeza ukusanyaji wa kodi kwa siku za mbeleni na ndio ikafanya nchi iweze kujitegemea. Narudia tena kusema Rais Magufuli alikuwa ni kiongozi mwenye maono makubwa sana tulichewa kumpata, tulipompata hajadumu. katuachia dira ya maendeleo ya taifa ambayo tukiifuata taifa linakwenda kujitegemea kwa kipindi kifupi.

Siku zote unapotatua matatizo kwa watu wengine unaweza kusababisha matatizo kwa wengine, hatotokea kamwe kiongozi atayewarisha wote. R.I.P JPM.
Hupo sahihi sana, Kipindi cha JK waliokatamba wachache mno na ndiyo kipindi ambacho ujambazi na uporaji wa mali za umma ulipaa lakini hawa Word Bank unaweza kushangaa wanakuambia uchumi ndo ulikuwa lakini sishangai maana hawa watu ndo wale ambao ata pale Congo wanatorosha madini alafu wanakuambia uchumi unakua kwa kasi, lakini ukiyabana watakuamia uchumi unadorora.
Screenshot_20210402-194516.jpg
 
Kuna watu wanatamani wakanushe ila sasa bandiko linaongea kwa takwimu na vithibitisho, yaani mkanushaji inabidi aje na data zake naye tumsikie, hii ngumu kumeza baba
praise and worship team wame stuck. ukiwa na data na maelezo ya kutosha huwa wanakosa pa kuingilia.
 
Back
Top Bottom