Hayati Dkt. Magufuli tutamkumbuka kwa kupambana na ufisadi na tutamlilia mbeleni

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,353
11,492
Moyo wangu umeanza kutahaharika. Kutokana na yale ninayoyaona. Mafisadi wote ndiyo wenye furaha kubwa ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania.

Hili limenifikirisha sana. Why asilimia kubwa ya wanaoonesha Furaha ni wale waliohujumu uchumi wa Taifa hili? Ni sawa wapo pia maskini na wasio mafisadi ambao nao walipata kuathirika kwa njia moja au nyingine na Utawala wa Magufuli. But Mafisadi wamefurahi zaidi.

Wasiwasi wangu umeanzia hapo. Na wasiwasi ni Akili pia. Why hawa Mafisadi wanaonesha kufurahishwa na kifo cha Magufuli?

Kipindi hiki kuna pesa nyingi Tanzania zitaibwa kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi wa 2025 tayari watu wameshaanza kujipanga na kupanga safu zao. Wakiamini kuwa Mama Samia hajui Fitna na hujuma za Kisiasa.

Kila kinachofanyika sasa ni Projection ya who is to be who and what in 2025. (Mnisamehe kwa Kiingereza changu kibovu ila nmeongea hivyo kuonesha msisitizo)

Hili suala la Kifo cha Magufuli si dogo kama ambavyo wengi wanadhania. Na athari yake haitoonekana leo.

MIMI NAAMINI ZIPO SIKU MBELE YETU WATANZANIA WATAKAPOLIA KUMLILIA MAGUFULI NA KUMWOMBA MSAMAHA KWA MATUSI WALIYOMTUKANA. SIKU HIZO ZAJA.

Kama Binadamu. Hakuwa Mkamilifu. Alikuwa na Madhaifu yake.

But TANZANIA TUNAYOIELEKEA TUTAMKUMBUKA NA KUTAKA RAIS KAMA YEYE.
 
Kwa hiyo unataka kutuaminisha wakati wote wa utawala wake hakukuwepo na vitendo vya ufisadi na rushwa! Ok.

Mimi nitamkumbuka kwa kutonipandisha daraja kwa miaka zaidi ya mitani sasa. Mwaka huu ilikuwa nipande kwa mara ya pili tena! Lakini katika hali ya kushangaza, hata ile mara moja tu, bado!
 
Mama Samia ana kibarua kizito sana. Namuonea huruma somehow.

Mungu ampe nguvu tu za kusimama.
 
Back
Top Bottom