Tuwe wazalendo, tuwajibike, tupende na tusiogope mabadiliko, Tanzania ni yetu sote | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuwe wazalendo, tuwajibike, tupende na tusiogope mabadiliko, Tanzania ni yetu sote

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mwakichi, May 25, 2011.

 1. mwakichi

  mwakichi JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2011
  Joined: May 14, 2011
  Messages: 420
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  WATANZANIA wenzangu huu ni waraka wangu kwenu, tuache ushabiki wa siasa na tuongelee kilicho na ukweli na kwa maslahi ya wote. Tangu Tanganyika imepata uhuru mpaka ikaungana na Zanzibar na kuzaliwa kwa TANZANIA, matatizo yetu bado yako pale pale pamoja na uhuru kutimiza miaka 50 matatizo yetu yamezidi kua makali.

  Jaribu kuangalia hali ya maisha ya mtanzania, chakula cha tabu, umeme tabu, petrol haishikiki, gas juu, mkaa haupatikani, mafuta ya taa juu, angalia shule alizojengewa hamna walim, madawati (wanafunz wanakaa chini), vitendea hamna.

  Njoo katika huduma za afya hamna madaktari na waliopo wana maslahi duni matokeo yake wanakimbia nchi, wauguzi hamna, hospital chache, madawa ndo kabisa. Barabara kama nyanja kubwa ktk kukuza uchumi wa taifa na mtanzania kwa ujumla ni mbovu, hata chache tulizokua nazo hazikidhi haja kutokana na uduni wake ktk ujenzi.

  Tunaambiwa kilimo kwnza power tiller za mgao kwa bei juu na kwa kujuana, leo katika karne hii mtanzania bado anaishi kwa jembe la mkono. Leo hii CCM ipo madarakan tangu na tangu, wanakiita chama tawala. Kimekua chama cha kutawala watu ila c kuhudumia watanzania na kuwaonyesha kama c kuwafikisha kabisa katk nchi ya asali na maziwa, wamedumisha amani kwel lkn mbona bado maskini sana sisi?

  Tuna kila kitu kinachoweza kutuletea maendeleo kuanzia mbuga, madini, mito, mabonde, milima, hali ya hewa, ardhi na vingine vingi lkn bado tunaelea katika dimbwi la umaskin. Napata mshtuko na kujiuliza tunakosea wapi?

  Je ni kuwapa CCM dhamana ya kutuongoza au sisi ni wavivu ktk safari ya asali na maziwa? Lkn nagundua watanzania sisi ni waaminifu, wasikivu na wajinga pia, ama mtu unampa dhamana ya kukuongoza kwa ahadi ya hospital anaposhindwa halafu anarudi tena unamsilkiiza wa nini?

  Hapa ndipo tunapokosea na tunakosea kwa ujinga na dhiki zetu, tunaogopa mabadiliko, unapewa kilo ya sukari na tshrt halafu anakuja tena baada ya miaka mi 5 kwa ahadi zile zile wakati sukar umeitumia kwa wiki 2 na tshrt imeshachanika na kuitupa, bado unampa dhamana ya kukuongoza kwa ahadi zile zile.

  Hapa tunakosea sana ndugu zangu, lakini nagundua pia viongozi tunaowapa dhamana ya kutuongoza ni wabinafsi, walanguzi, matapeli na wezi wa mali ya mtanzania.

  Wanaingia mikataba ya siri kwa maslahi yao na watoto wao,angalia RICHMOND,IPTL,TRL,NBC..kweli kiongozi aliepewa dhamana ya kuendesha nchi anauza nyumba za serikali wakati watumishi wapo na wataendelea kuwepo?

  Rais mstaafu wa awamu ya tatu amelikosea sana taifa letu, leo taifa linajenga tena nyumba za viongoz zilizouzwa kwa bei ya mshkaki badala ya kupeleka fedha katk shuke zetu, au hospitali zetu na kusaidia watanzania. Richmond kila mtu anaijua na gharama za kuweka mitambo nchini kwetu iwe imezalisha au haijazalisha.

  Afadhali analia na kumbuka hivi,EPA,RADA,NDEGE YA RAIS,MISAMAHA YA KODI,UWEKEZAJI WA MIGODI(buzwagi,nyamhongo),KIWIRA,UWEKEZAJI MBUGA YA WANYAMA,KUJILIMBIKIZIA MALI KWA VIONGOZI..,Tanzania haipaswi kua maskini katika kiwango kilichopo.

  CCM ni tatizo kwetu na lazima mabadiliko yatokee ili tuipate ile Tanzania tunayoitaka wengi, mwanzo kulikua na CUF leo imetugeuka imefunga ndoa na CCM, tutakimbilia wapi kama siyo CDM?

  Leo Dr slaa anazungumza hali halis ya MTz lkn kijana tulie mtegemea Nape anapingana na ukwel aliokua anauona kabla ya kua alipo sasa ni mchumia tumbo ka wengine tuu,TANZANIA LAZIMA TUKUBALI MABADILIKO KATIKA KUPATA NEEMA TA MTANZANIA..

  Kwa leo naomba niishie hapa


  Tanzania nakupenda, ntakupenda daima.
   
 2. cesallinho

  cesallinho Member

  #2
  Oct 20, 2013
  Joined: Jul 11, 2013
  Messages: 94
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 15
  Mimi naona wabongo hatuna uzalendo kwani tunalalamika serikali haiwajibiki lakini maana ya serikali ni watu,ya watu na kwa watu(abraham lincolin) sasa tumekuwa tukisikia au kuona baadhi ya viongozi wakitokea na kuwa bora na kufanya kazi zao vizuri katika hali ya kinufaisha taifa ila hawa viongozi wakigusa sehemu zenye maslahi ya watu wengine wakubwa huanza kuhujumiwa au hubadilishwa nafasi ile au wizara fulani...sasa tunakosa uzalendo pale kwa kushindwa kushinikiza au kumumuunga mkono huyo kongozi husika hatimaye anajiona yuko pekeyake na kuamua kurudi nyuma na kufanya mambo yake binafsi sasa ili serikali ibadilike sisi ndio tubadilike na tusimame maana tunaoathirika ni sisi na tusikimbilie sana kubadilisha labda chama cha siasa kitatuokoa ni sisi tukiweza kuwaonyesha,kuwahoji na kudai nini tunahitaji kutoka kwao tutaiendesha serikali ya nchi hii..
   
 3. Patrickn

  Patrickn JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2013
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 7,497
  Likes Received: 3,860
  Trophy Points: 280
  Vitu vingine vinaumiza hata kama unauzalendo gani...mamikataba ya kijinga jinga na wizi wa rasilimali unadhani yanavumilika? Bora hizo rasilimali zisiguswe tu
   
 4. Sanoyet

  Sanoyet JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2013
  Joined: Apr 3, 2013
  Messages: 1,328
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Muungwana utaanzia wapi iwapo kila sehemu wamefunga njia,Lete mgomo uone kichapo cha polisimagamba.
   
 5. M

  Mnasihi JF-Expert Member

  #5
  Oct 20, 2013
  Joined: Oct 9, 2013
  Messages: 3,320
  Likes Received: 1,678
  Trophy Points: 280
  Twahitajika kupigania uhuru wa taifa letu upya kwani baada ya Mwl kuwaondoa wakoloni wamekuja weusi ambao ni wabaya kuliko wale wa 19 kweusi. Elimu ya uraia muhimu kwa rika zote ili kuleta mabadiliko chanya.
   
 6. Msambichaka Mkinga

  Msambichaka Mkinga JF-Expert Member

  #6
  Mar 31, 2016
  Joined: Oct 22, 2015
  Messages: 1,399
  Likes Received: 2,261
  Trophy Points: 280
  Taifa lolote hujengwa na wananchi wake, hasa zaidi na wale wananchi wazalendo. Taifa pia linatakiwa kulinda misingi ya utaifa.Taifa letu la Tanzania, ni Taifa huru, linalostahili kulinda uhuru wake, na misingi ya utaifa wake ambao ni Umoja, Uhuru na haki za binadamu, na kuheshimu na kulinda misingi ya Demokrasia. Watanzania wote ni muhimu kuifia misingi hiyo, na hapo ndipo tunastahili kuonesha uzalendo wetu.

  Kama litatokea Taifa lolote jingine, liwe kubwa au dogo, likatupatia masharti kwa kigezo cha misaada, kututaka tuanze kubaguana kwa misingi yoyote ile, ikatokea Taifa lolote linatutaka tuanze kuwagandamiza raia wetu au kundi fulani la raia wetu, hapo ndipo pa kuonesha uzalendo wetu.

  Kama itatokea nchi yoyote iwe kubwa au ndogo ikatulazimisha tuanze kutokusikiliza matakwa ya wananchi wetu, tuanze kuvunja misingi ya demokrasia, hapo ndipo tunalazimika kuonesha utaifa wetu. Na kwa kweli kama tukilazimishwa kufanya hayo kama kigezo cha kupata misaada, basi ni aheri tuikose. Kama ni kuteseka aheri tuteseke.

  Juzi MCC wamesema wanasimamisha msaada wao kwa Tanzania kwa sababu ya Tanzania kukiuka misingi yake ya Utaifa kwa kugandamiza demokrasia, na kwa kuwanyima wananchi wake uhuru wa kutoa mawazo yao katika mitandao, yote yakiwa kinyume cha katiba yetu na kinyume na global citizenship human rights ambazo Taifa letu kama mwananchama wa umoja wa mataifa linalazimika kuheshimu.

  Kuna watu au kwa kutoelewa au kwa dhamira chafu, wanasema tuoneshe uzalendo, yaani tuoneshe uzalendo wa kuunga mkono matendo maovu ya serikali yetu ya kudidimiza demokrasia na uhuru wa raia wake. Hii ni ajabu ambayo sijawahi kuisikia kutoka kwa mtu yeyote mzalendo na mwenye akili timamu.

  Kwanza ukiukaji wa demokrasia huko Zanzibar, siyo Wamarekani waliokuwa wa kwanza kulalamika. Sheria udhibiti wa mitandaoni Tanzania, siyo Wamarekani waliokuwa wa kwanza kuilalamikia. Sheria mbaya ya Tanzania ya uhuru wa vyombo vya habari, tumeilalamikia wananchi wengi. Tume ya Jaji Nyalali pia iliitaja kama sheria mbaya.

  Kuna mambo ambayo mataifa makubwa yanagandamiza mataifa madogo lakini siyo katika hili la Zanzibar na sheria ya mitandao. Marekani katika hili imesaidia kuongeza nguvu ya sauti za Watanzania wanyonge ambao wameililia serikali yao lakini serikali yao haitaki kuwasikiliza.

  Watanzania wote wana haki na pale ambapo serikali yao inakataa kuwasikiliza, jumuiya ya mataifa inalazimika kuwasaidia. Haiwezekani leo hii serikali ya Tanzania ikaamua kuanza kuwatesa au kuwaua raia wake, halafu ikikemewa na mataifa mengine, tusimame na kusema mataifa hayo yanaingilia uhuru wetu.

  Ni uhuru upi tunaolalamikia kuingiliwa, uhuru wa kugandamiza haki za msingi za raia? Kama hayo ndiyo tunayoyaamini, kwa nini tunalaumu jamii ya kimataifa kwa kuchelewa kuingilia mauaji ya kimbali kule Rwanda? Kwanini hatusemi kuwa yalikuwa ni mambo yao ya ndani hayana uhusiano na jamii ya kimataifa? Huu ni unafiki mkubwa wa sisi Waafrika.

  Udidimizaji wa demokrasia katika Afrika umechangia sana umaskini wa bara hili. Wananchi wa Afrika wanapokufa kwa njaa kutokana na haki za wananchi kugandamizwa na utawala mbovu, tunakimbilia kwenye mataifa hayo hayo tunayoyalaumu kuingilia mambo yetu, kwenda kuomba chakula, mbona huwa hatusemi kuwa haya mambo ya njaa ni mambo yetu ya ndani, tusisaidiwe na nchi nyingine.

  Kwa hali ilivyo Afrika, ningependa jamii ya kimataifa ipewe uhuru zaidi juu ya Taifa lolote ambalo watu wake wanadhulumiwa, kugandamizwa au kuonewa na watawala wao. Uzalendo wetu tuuoneshe katika mambo yanayokiuka misingi ya Taifa letu lakini siyo katika uulinda uovu.
   
 7. justine lowasa

  justine lowasa JF-Expert Member

  #7
  Sep 5, 2016
  Joined: Aug 30, 2016
  Messages: 715
  Likes Received: 752
  Trophy Points: 180
  Watanzania wenzangu nawasalimu kwa jina la amani na mshikamano wa taifa letu uliowekwa thabiti na viongozi wetu waasisi JKN na AMK!

  Nimekaa muda mrefu nakutafakar jinsi gani tulivyo isahau nchi yetu na kujibebesha mzigo mzito wa vyama ya siasa mabegani mwetu tukawa kama watumwa kumbe sisi ni wana mfalme (tanzania) mwenye utajiri wa amani, rasilimal na vivutio vingi! Hebu tuikumbuke nchi yetu natuanze kumpinga yeyote anaejaribu kutuharibu akidhani chama chake au kikundi chake ni bora zaidi ya Tanzania yetu

  Ifike mahali kila raia ajue kuwa yuko responsible kulinda nakutetea katiba ya nchi na ikiwa viongoz tulio waweka kwa upendo wakitugeuka kwa kutokutii katiba na sisi tuwageuke kwa ajili tu ya usalama wa nchi yetu.

  Nimalize kwakusema no one is bigger than TANZANIA but TANZANIAN themselves!
   
 8. Frank Wanjiru

  Frank Wanjiru JF-Expert Member

  #8
  Sep 5, 2016
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 5,516
  Likes Received: 5,137
  Trophy Points: 280
  Wewe ndie Fredy mtoto wa Lowasa au ni jina tuu?
   
 9. mcubic

  mcubic JF-Expert Member

  #9
  Sep 5, 2016
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 10,165
  Likes Received: 4,195
  Trophy Points: 280
  Ila maisha ni siasa na siasa na maisha.

  Tusipokuwa na vyama siasa hainogi.

  Mungu ibariki Tanzania
   
 10. technically

  technically JF-Expert Member

  #10
  Sep 5, 2016
  Joined: Jul 3, 2016
  Messages: 7,084
  Likes Received: 16,681
  Trophy Points: 280
  Safi
   
 11. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #11
  Sep 5, 2016
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,576
  Likes Received: 12,860
  Trophy Points: 280
  awe au asiwe ni mtanzania kama wewe mimi jpm na jecha
   
 12. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #12
  Sep 5, 2016
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,576
  Likes Received: 12,860
  Trophy Points: 280
  halafu mtu anasimama jukwaani na kutoa kauli za kuzidi kuumiza i realy hate ccm na watu wake wote
   
 13. Kadhi Mkuu 1

  Kadhi Mkuu 1 JF-Expert Member

  #13
  Sep 5, 2016
  Joined: Feb 4, 2015
  Messages: 5,295
  Likes Received: 3,532
  Trophy Points: 280
  Samahani, wewe ni verified user, yaani mtoto wa E N Lowassa? Kama ndiye huu ushauri ulioutoa wa kuwageuka viongozi hata ENL ni kiongozi. Nashindwa ku comment zaidi maana isije ikawa hiyo ni fake ID.
   
 14. c

  chikurukutu JF-Expert Member

  #14
  Sep 5, 2016
  Joined: Jul 26, 2015
  Messages: 224
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Tatizo wengine wanaifanya nchi hii ni Mali ya ccm
   
Loading...